Good expectations vs Reality: Wakuu msaada wenu hii biashara siielewi

kenge 10

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,448
2,362
Habari Wakuu,

Baada ya ban ya mifuko ya plastic, wajasiriamali wengi walichangamkia fursa ya mifuko mbadala. But mimi kama mjasiriamali pia kuna gap nililiona, kwa sababu mifuko ya plastic ilikuwa multipurpose kuanzia kubebea bidhaa, kuwashia moto uswahilini na baadhi ya abiria kutapikia au kutema mate wanaposhikwa na kichefu chefu wawapo safarini.

Gap ambalo niliona limesahaulika ni hilo la hao abiria wenye travel sickness. Basi Mzee kwa kuzingatia ile principle ya solve tatizo kwenye jamii upate hela nikajitosa Alibaba nikaagiza mzigo wa pieces 2,500 wa travel sickness bags ile inayotumika kwenye ndege na meli, na kuzingatia hapo kati pindi nasubiria mzigo uje nilizidi hamasika baada ya member humu anaeitwa TODAYS kuliongelea hili tatizo.

Mapicha picha yalianza baada ya mzigo kufika na kuanza kutafutia masoko, nilianza kuomba tender ya kusupply kwenye baadhi ya makampuni ya mabasi, but bei wanayotaka ndogo sana hii kwa sababu mpaka kufika Tanzania 1bag inacost sh. 264/- but wao wanataka kwa bei ya sh. 200/- halafu wanataka iwe na logo zao.

Nikaona sio kesi nikaacha kutafuta tender nikazama Ubungo Terminal kujaribu kuuza jumla kwa wafanyabiashara wa mule, but wakawa waoga ukizingatia wengine hawajawahi kuiona hata kwenye movie so ugeni ulichangia. Nikachage strategy nikampa jamaa mmoja mule Ubungo Terminal yeye huwapa wafanyabiashara wadogo wa mule UBT vitu kama mikate, cakes na maji kwa mali kauli then jioni wanaleta hesabu na kukata chao.

But nao pia wanasuasua sababu ya profit ndogo compared na vitu vingine wanavyouza then hii mifuko (travel sickness bags) ni migeni kwa watu wengi so inabidi watumie na muda wa kuwaelewesha wateja, mwisho wa picha inakuwa complications kwao wakati bidhaa zao wanazouza siku zote kama mikate na maji haviitaji mambo mengi.

Sasa wakuu naombeni mnishauri chochote cha kupush zaidi, maana naona kichwa kime-stuck.

Loss is a part of Game ☺
KENGE.
 
Biashara yako itaenda kwa kufanya yafuatayo.
1;andaa promotion itakayo elezea bidhaaa yako kuanzia matumiz yake,faida zake na umuhimu wake kwa muhitaji.
2:fanya promo yako Kwanza kwa vituo mbali mbali vya wasafiri hata wa dala dala na redio. Iki fahamika happy ndipo utaona wateja wanavyo kuja.
3;tumia mitandao ya kijamii kwa faida ya kuandaa tangazo na kuomba watu wenye page kubwa wakupostie kwa ajil ya ushawishi hapo pia uta win
4; andaa specific supplier ambao wao watapatikana periodly kwa maeneo yote ya wasafiri hasa tageted place.
5; bei yako iwe inaendana na uchumi wa wahitaj. Kwa kutotaka faida kubwa then Jenga brand yako na ukue sasa
Kila lakheri. Mkuu
 
Komaa Hata Miezi 6 Kwanza.

Usitake Kuanza Kwa Faida Wakati Hao Unaowauzia Hawajajua Hata Umuhimu Wa Hiyo Bidhaa Yako.

Ndio Maana Wanakupangia Bei Kwa Kuwa Wanaona Kama Wanakusaidia, That They Can Survive Without Your Product.
 
Anza kuingia kwenye mabasi wewe mwenyewe kuitangaza hiyo bidhaaa yako. Asubuh unawahi ubungo basi wakati linaondoka wewe unapanda namifuko yako unaanza kutoa elimu yako huku basi linayoyoma ukianza kutoka njee yamji unashuka unashuka unapanda basi jingine lakurudi ubungo vilevile unaendelea kutoa elimu mpaka watakusoma2
 
Ndugu wakati unaagiza mzigo ulaya, jaribu kutembelea kiwanda cha SSB kinachozalisha vifungashio onana na meneja uzalishaji kwa undani juu ya wazo lako.

Wao wanatengeneza ile inayotumika kwenye 🚣 boat zao, so unaweza kugain in business...
kenge 10
 
Hiyo ni moja ya changamoto ya kuwa wa kwanza sokoni...first mover disadvantage. Usikate tamaa.

Unachotakiwa kufanya ni kuwazoesha watu kwanza. Weka vijana wako pale ubungo wauze on commission. Tumia vijana wapya kabisa ambao wanauza bidhaa hiyo tu.

Pia endelea kutoa elimu.
 
Biashara yako itaenda kwa kufanya yafuatayo.
1;andaa promotion itakayo elezea bidhaaa yako kuanzia matumiz yake,faida zake na umuhimu wake kwa muhitaji.
2:fanya promo yako Kwanza kwa vituo mbali mbali vya wasafiri hata wa dala dala na redio. Iki fahamika happy ndipo utaona wateja wanavyo kuja.
3;tumia mitandao ya kijamii kwa faida ya kuandaa tangazo na kuomba watu wenye page kubwa wakupostie kwa ajil ya ushawishi hapo pia uta win
4; andaa specific supplier ambao wao watapatikana periodly kwa maeneo yote ya wasafiri hasa tageted place.
5; bei yako iwe inaendana na uchumi wa wahitaj. Kwa kutotaka faida kubwa then Jenga brand yako na ukue sasa
Kila lakheri. Mkuu
Good advice
 
Anza kuingia kwenye mabasi wewe mwenyewe kuitangaza hiyo bidhaaa yako. Asubuh unawahi ubungo basi wakati linaondoka wewe unapanda namifuko yako unaanza kutoa elimu yako huku basi linayoyoma ukianza kutoka njee yamji unashuka unashuka unapanda basi jingine lakurudi ubungo vilevile unaendelea kutoa elimu mpaka watakusoma2
Nakubaliana na ushauri wako kwa mtoa mada. Akifikiri wenye mabasi watakubali kum- support anajidanganya. Abiria wenyewe hasa wenye watoto akiwauzia kwa 300 wanaweza kununua
 
Nakubaliana na ushauri wako kwa mtoa mada. Akifikiri wenye mabasi watakubali kum- support anajidanganya. Abiria wenyewe hasa wenye watoto akiwauzia kwa 300 wanaweza kununua
Ndio hivyo yeye mwenyewe anatakiwa aigeuze hiyo bidhaaa kama yake yaani afikirie kama vile bidhaaa mpya anaiingiza sokoni, watu wakishaizoea nakuipenda wataihitaji wakishaihitaji walanguzi lazima atawapata2 iwe isiwe. Mwanzo mgumu hasa unapoamua kubuni bidhaaa mpya bila kuwaiga wengine
 
Back
Top Bottom