GE2025 Gombo: Nikiwa Rais namwachia huru Tundu Lissu,Atengeneze katiba mpya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mhe. Gombo Samandito Gombo, ameahidi kumuachia huru mwanasiasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, endapo atashinda uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Septemba 4, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Shinyanga, Gombo amesema taifa la Tanzania haliwezi kuwa na amani ya kweli bila haki kutendeka kwa kila mmoja, amesisitiza kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha Tundu Lissu anaachiwa huru pamoja na kuunda kamati maalum ya kutengeneza katiba mpya.

Vipaumbele vingine alivyovitaja ni pamoja na kufuta kikokotoo cha mafao ya wafanyakazi, kutoa huduma za afya bure, kufuta mikopo ya elimu ya juu na kutoa msamaha wa madeni ya wanafunzi waliokopeshwa na serikali, ili kila Mtanzania awe na nafasi ya kupata elimu.

Kwa upande wake, mgombea mwenza wa urais kupitia CUF, Husna Mohammed, amesema rasilimali zilizopo mkoani Shinyanga hazilingani na hali halisi ya maisha ya wananchi, hivyo amewasihi wakazi wa mkoa huo kufanya uamuzi sahihi siku ya uchaguzi ili kuleta mabadiliko ya kweli.
 
View attachment 3465149
Wakati nasoma Lugha ya Kiingereza na nikiipenda sana, hiyo kauli ya Gombo tulikuwa tukiita "Conditional Sentence Type Three" which is hypothetical.
 
Hawa waigizaji wa hiki chama cha CUF, Mgombea wao Urais na mwenza ,wanaambatana pamoja, hii nchi ilivyokubwa hivi wataimaliza leo??..au ili mradi tu waonekane na Landcruiser jipya,account zisome
 
Akizungumza na watanzania juzi balozi polepole alibainisha kwamba ... kundi la wanamtandao likiongozwa na JAKAYA MRISHO KIKWETE Ndilo lililopanga njama za kumuua ndugu JOHN POMBE Magufuli
Pia alibainisha kwamba utekaji na mauaji nchini yanafanywa na mtoto wa raisi bwana ABDUL
na akasema kuna mtu mmoja aliingia ikulu na kupiga picha za namna gani na mgombea.
 
Kwa siasa hizi unazofanya, zitaifanya CCM itawale nchi hii milele hadi pale mtakapokuwa na akili ya kufanya siasa za kweli. Waulizeni Kiiza Besigye wa Uganda, Julius Malema wa Afrika Kusini na Mondlane wa Msumbiji. Siasa zao za kipumbavu kama zenu zinawagharimubna watakufa hawajaingia Ikulu labda kunywa juizu na pipi kama viongozi wenu! Nyambafu!!
 
Ivi wewe Gombo kwa unavoona CUF inaweza kushinda uchaguzi kwa nafasi ya urais?

Siwakatishi tamaa ila chama chako bado hakuna watu.

Mfano wewe unafikiri ligi ya mpira wa miguu Tz ikiwa bila simba au yanga itanoga?
Kwa Tz CCM Bila chadema ni uwongo mzee Gombo.

Timu za mpira zinafanya usajiri wa wachezaji wa viwango kwaajili ya kupata ubingwa dhidi ya wapinzani wao kwahyo viongozi wa CCM hawawezi kufanya maendeleo makubwa na yenye viwango ikiwa hakutakuwa na wapinzani wenye viwango vya juu kama tundu lisu.

Binafsi siwezi kusema kwamba tundu lisu hana kosa na siwezi kusema kwamba hawezi kufanya makosa ila nampongeza kwakuwa na uthubutu na uhodari kwenye siasa ya nchi yetu.
Yani mtu huwezi kusema wewe ni mpinzani harafu umepoaa kiasi kwamba watawala Wala hawakuwazi na hawakuogopi.

Yani mim nataka CCM wawepo watu wa viwango, CUF wawepo watu wa viwango vya juu pia, CHADEMA pia wawepo watu wa moto, ACT pia wawepo watu hatari yani kiujumla Kila chama kiwepo na watu wa maana ili tutengeneze serikali yenye mchanganyiko wa watu wenye viwango kutoka katika vyama tofauti tofauti. Hii nchi ni ya watanzania Kila mtu atakufa na ataiacha kwahyo Mimi binafsi nataka siasa imara na nashauri kama mtu hawezi siasa basi akalime au akafanye shughuli zingine.

Muhimu: mtu yeyote akivunja Sheria za nchi basi aadhibiwe kama Sheria inavotaka.

Tuache ball litembee, mambo ya kukatana katana na mchezo wa rafu unaharibu Radha ya mpira wa miguu.
 
Hawa waigizaji wa hiki chama cha CUF, Mgombea wao Urais na mwenza ,wanaambatana pamoja, hii nchi ilivyokubwa hivi wataimaliza leo??..au ili mradi tu waonekane na Landcruiser jipya,account zisome
wamepewa mapaka ulinzi wa kufa mtu wapuuzi hao
 
Hawa wagombea wanaigiza tu, hawana nia ya kweli. Kuna mmoja wa chama cha kokoliko yuko kama katuni, anafanyia kampeni kwenye vijiwe vya kahawa na drafti
 
Kule zanzibar kuna wagombea wanapiga mkwara wagombea wenzao ambao pia ni wapinzani wenzao! Hawa wagombe wengi ni magumashi matupu kuzuga wananchi wenye uelewa na uwezo mdogo wa akili za kuchakata uongo na ukweli siasani
 
Back
Top Bottom