GE2025 Gombo Gombo: Mkichagua CUF tutakomesha utekaji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chama cha Wananchi CUF kimesema endapo kitaingia madarakani kitahakikisha kinapambana na utekaji wa watu nchini ikiwemo na kuhakikisha kinaimarisha vyombo vya ulinzi na usalama.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mwanza mgombea urais kupitia CUF Gombo Samandito Gombo amewaomba watanzania kukichagua chama hicho ili kiweze kuimarisha ulinzi.

Katika hatua nyingine Gombo amesema chama hicho kinajitosheleza na kimejipanga vizuri kukitoa chama cha Mapinduzi CCM madarakani.
 
Watu wanajinadi kweli kweli 🤣🤣🤣.
Mwaka wa uchaguzi huu
Kama hautaki ni wewe.
 
Hv hawa wagombea wanadhani bado tupo miaka ya 90..sahv wasomi ni wengi... kwahyo unapotunga uongo basi ufananie na ukweli kwa mbaali...unaposema utakomesha utekaji kwa kuimarisha ulinzi ina maana ulinzi wasasa haupo imara...sasa tueleze njia gani utazozitumia kuimarisha ulinzi ambapo kwasasa zinafeli...kweli siasa ni utapeli wa kifikra.
 
Chama cha Wananchi CUF kimesema endapo kitaingia madarakani kitahakikisha kinapambana na utekaji wa watu nchini ikiwemo na kuhakikisha kinaimarisha vyombo vya ulinzi na usalama.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mwanza mgombea urais kupitia CUF Gombo Samandito Gombo amewaomba watanzania kukichagua chama hicho ili kiweze kuimarisha ulinzi.

Katika hatua nyingine Gombo amesema chama hicho kinajitosheleza na kimejipanga vizuri kukitoa chama cha Mapinduzi CCM madarakani.
Mtuonyeshe nyomi anayohutubia
 
Back
Top Bottom