Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuacha kuwashambulia wananchi wanaojitokeza kuonesha hisia zao katika masuala yanayohusu maisha na mustakabali wa taifa.
Golugwa ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya viongozi wa CHADEMA yaliyofanyika kupitia mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu, yakijadili mada isemayo “Uchaguzi na uhalali wa Kidemokrasia kukabiliana na udanganyifu katika uchaguzi Tanzania.”
“Ninatoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama viwalinde raia. Ni vibaya sana kuwa na vyombo vinavyowapiga watu wanaodhihirisha hisia zao za nini wanakitaka. Hii inaleta hatari zaidi inapokuwa wazi kwamba vyombo vya ulinzi vinagombana na wananchi. Tunazungumza katika mazingira ya kiraia,” amesema Golugwa.
Ameongeza kuwa wananchi wanahitaji kwanza demokrasia kabla ya miundombinu mingine, akisisitiza kuwa maendeleo yanapaswa kwenda sambamba na uhuru wa kujieleza na kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa.
Kauli ya Golugwa ilikuja saa chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwadhibiti wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika katika viunga vya Mahakama Kuu, Masijala ndogo ya Dar es Salaam, kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Kulingana na mashuhuda na video zilizochukuliwa na wanahabari katika viunga hivyo, baadhi ya wafuasi waliipigwa virungu na mateke kufuatia taharuki iliyozuka baada ya ukumbi wa Mahakama kujaa na wafuasi waliokuwa nje kuanza kusukumana na askari.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, Jumanne Muliro, lilieleza kuwa vurugu hizo zilianza baada ya baadhi ya wafuasi kuanzisha fujo na kujaribu kuwashambulia askari, hali iliyowalazimu polisi kujihami na kutuliza vurugu.
“Baadhi ya wafuasi waliokuwa nje ya Mahakama walianzisha fujo na kujaribu kuwashambulia askari, ambao walijihami na kutuliza fujo hizo haraka,” taarifa ya Polisi ilisema.
Polisi wametoa onyo kuwa hawatasita kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote atakayewachokoza askari au kuhatarisha usalama kwenye maeneo ya kimahakama.