Godoro La Mtumba - 15-
ILIPIOSHIA :
Mjomba alitoka na kwenda kufungua mlango
Karibu sana dada
Asante.
Sasa ni hivi, nakupa hela sasa hivi ukanunue suruali ya jinsi kiuno saiziiii
mjomba alisema akiniangalia
Saizi ishirini na sita
nilidakia
Oke, ishirini na sita
halafu na kitop cha juu saiziiii
SASA ENDELEA
Yule mhudumu akadakia kuhusu kitop, akasema
Kuhusu kitop wala hakuna haja ya kusema, mimi nitajua mwenyewe.
Kwa sababu chini nilivaa raba, niliagizia na sendoz
Haya na sendzo, mcheki miguu yake kwanza, alisema mjomba, akatoa kitu kama laki moja hivi kwa ajili ya manunuzi hayo.
Nilimwona yule mhudumu akiachia tabasamu. Nilijua ilikuwa siku yake ya kuvuna maana laki moja zilikuwa nyingi, suruali ni kama elfu ishirini, kitop kama elfu kumi tu, sendoz sanasana elfu kumi na tano maana aliambiwa aende kwenye maduka ya kawaida.
***
Ndani ya nusu saa, yule mhudumu alirudi akiwa amefanikiwa kuvipata vile vitu. Moyoni nilijilaumu sana kwamba ni kwa nini nisingetoka na nguo za nyumbani kwenye begi la madaftari ya shule.
Nilipojaribu nilitoka bomba sana, kama si mwanafunzi vile. Nilipendeza pia.
Sasa sikia, tutoke, twende hoteli nyingine, mjomba alisema, tukajizoazoa, lakini kabla ya kufungua mlango simu ikapigwa tena
Haloo
wamekuja? Polisi kabisa polisi au wanamgambo? Oke, tunakuja, alisema mjomba.
Vipi baby? Nilimuuliza mjomba.
Polisi wamekuja!
Kweli?
Yes, nimeambiwa.
Na nani?
Si mtu wa mapokezi.
Sasa itakuwaje?
We twende tu.
Tulitoka chumbani, sare zangu za shule zilikuwa kwenye mkoba wa madaftari.
Tulipofika mapokezi, tulikuta polisi watatu, wawili wanaume. Walikuwa wakimtaka mtu wa mapokezi akawaonyeshe chumba tulichokuwemo
Sisi wale ni wateja wetu hatuwezi kufanya hivyo, kama mna shida nao basi subirini watoke, alisema mtu wa mapokezi huku akitukodolea macho wakati tunafika mapokezi
Zuhura Chanchandu alipotuona akadakia
Hawa hapa afande, wala usiende mbali.
Mimi na mjomba tuliendelea kupita kuelekea mlango mkubwa huku tukijifanya hatujui lolote linaloendelea
We mama si ulisema yupo na mwanafunzi tena ana yunifomu? afande mmoja aliuliza kwa ukali.
Atakuwa amebadili nguo lakini mimi nilimwona ana sare za shule.
Sisi wakati huo tulishafika nje kabisa kwa hiyo tulichokisikia mpaka mwisho tunamalizikia mlangoni ni atakuwa amebadili nguo lakini mimi nilimwona ana sare za shule.
Mpaka tunafika kwenye gari, nyuma yetu hakuna aliyekuwa akitufuata, tukaingia na kutoka zetu.
Yule mwanamke mjinga sana, alisema mjomba akiendesha.
Mimi kwa furaha, badala ya kumjibu nilijikuta namlalia mapajani licha ya kwamba alikuwa anaendesha, hilo sikulijali.
Baby sasa si utanizuia kuendesha hivyo unavyofanya?
Baby jamani, kweli? nilimuuliza nikiwa bado nimemlalia, nikamtania kidogo kwa kumshikashika eneo muhimu, kidogo apeleke gari kwenye mtaro...
Baby bwana, alisema, nikajiondoa.
Sasa sweet mi ninavyoona, tuingie dukani kwanza tununue nguo zangu halafu ndiyo twende hoteli, si umeona hizi zilivyochafuka na vumbi ya lile vurugu la Zuhura?
Kweli baby, umekuwa kama mtu wa kutoka shamba.
Mjomba alicheka kidogo lakini wakati huo tulishafika eneo la kuegeshea magari la duka moja la nguo.
Tulivyoshuka na mjomba ilikuwa kama tumeshuka mtu na mke wake, maana baada ya kushuka tu tulishikana mikono kwenda ndani ya duka hilo lililoandikwa Karibu Pamba za Ukweli.
Mjomba alinunua suruali za jinzi mbili, nyeusi na ya bluu, kisha akanunua na fulana mbili, nyeupe na kijani iliyoiva. Akaninunulia na kufuli tatu mimi. Nilimshukuru sana kwani zote tatu zilikuwa za bei mbaya.
Tulitoka hapo, katika hali ambayo hatukupanga, mjomba alisema twende Mlimani City tukapate juisi nzito kwanza kisha twende hoteli.
Mlimani City napafahamu sana, pana watu kibao, hata baadhi ya wanafunzi wenzangu huwa wanakwenda pale kama siku si ya shule. Halafu mwalimu wetu mmoja anaitwa Arnold naye anapenda sana kutoroka shule na kwenda hapo Mlimani City, sasa itakuwaje? Kumwambia mjomba tusiende ilikuwa ngumu.
Oke, twende baby, nilijikuta nakubali kwa ujasiri. Kwanza sikuwa na wasiwasi, hata kama Mwalimu Arnold angeniona angenifanyaje wakati mwenyewe anakwendaga hapo kwa kuibia.
Halafu kingine sikuwa na wasiwasi wa kupoteza shule kwani mjomba alishasema atanioa sasa shule ya nini kama nitaoelewa na mwanaume mwenye pesa zake kama mjomba Msafiri.
Tulifika Mlimani City, tukazama ndani mpaka kwenye maegesho. Kama tulivyoingia dukani, hapo pia tuliingia vilevile, tulishikana mikono na kutembea mwendo wa kubembelezana.
Nilihisi kitu...
Itaendelea kwenye Ijumaa Wikienda siku ya Jumatano ijayo...