Godbless Lema; unajua utakosea wapi? Mimi najua Muslim brotherhood walikosea wapi

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
3:24 AM
Kuna jambo limenikosesha usingizi na nikatamaani kushare na kamanda Lema na ma - great thinkers wote kwa pamoja.

Kamanda Lema pole sana kwa unayopitia kisiasa, hakika ni magumu kwa sasa na kwangu, hayana dalili za kuwa mepesi kwa siku za mbele.
Kuna watu ndani ya CCM , tena wenye nguvu na mamlaka wanaoonyesha waziwazi kwamba hawakutaki kama mbunge wa Arusha.

Wanafanya mengi kabla ya uchaguzi 2020 na watafanya maajabu hiyo 2020, my soul is a witness!
Kamanda, akumulikaye mchana, usiku atakuchoma!
Siandiki kukuogopesha, wala siandiki kukupa taarifa zozote mpya sana. Naandika nikisukumwa na wasiwasi wa kukusihi uwe na mbinu mbadala zaidi ya moja na nguvu ya umma iwe mbinu ya mwisho kabisa kwenye mpangilio na kwa umuhimu.

Kumbukumbu ya mauaji ya kihalaiki huko Rabaa inatoa mwangaza juu ya makosa makubwa ya kimkakati ya Muslim brotherhood huko Egypt kufuatia mapinduzi ya 2013 ya Mohamed Morsi.

August 14, 2013 ilikuwa siku ya machafuko zaidi katika historia ya karibuni ya Egypt. Majeshi ya ulinzi yalisambaza kikatili mno maandamano huko Rabaa al- Adawi square na Giza al- Nahda square kaskazini mwa Cairo.
Mamia ya waislam waliokuwa wakiandamana kupinduliwa kwa Morsi , rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Egypt, waliuawa.
Waangalizi wa haki za binadamu wanasema zaidi ya raia 800 waliuawa.

Lakini, mauaji ya Rabaa, kama yalivyokuja kutambuliwa, yalikuwa shule kwa jambo jingine: yalionyesha kushindwa kabisa kwa mikakati ya muslim brotherhood baada ya Morsi kung'olewa. Tokea hapo muslim brotherhood haijaweza kupata nafuu katika harakati zake kidini, kisiasa, wala kijamii. Wamebaki ndugu, kaka, ila si ndugu au kaka tena katika uislam~ muslim brotherhood.
Miaka karibuni minne sasa, mamia zaidi katika brotherhood wameuawa na taasisi ya Muslim brotherhood sio mdau mwenye nguvu tena katika harakati za Egypt.

MUSLIM BROTHERHOOD WALIKOSEA NINI?
1. Waliliamini Jeshi.
Viongozi wa brotherhood waliwaambia wanachama wao kuwa jeshi liko pamoja na Morsi, kitu ambacho hawakuwa na uhakika nacho.

2. Walipuuza uwezo wa Jeshi.
Pamoja na jeshi kuwa na ziada ya silaha, mafunzo na uwezo, Brotherhood waliamini kwa dhati wangeshinda mapambano.

3. Imani potofu.
Brotherhood waliamini kuwa ni majenerali wachache waliosupport kuangushwa kwa Morsi na hivyo mgomo wao ungefanya jeshi litawanyike na hivyo kurahisisha Morsi kurudi madarakani.

Brother Lema, umekuwa chachu na hamasa kwa vijana na umma kwa ujumla katika kudai haki. Umefanya mengi kwa mfano!
Umeonyesha kuwa uko tayari kushuka kwenye ndege ya vita katika uwanja wa mapambano wakwanza na kupakia wa mwisho.
Natamaani kukuona muda mrefu zaidi kwenye siasa za Tanzania ila kuwa makini na hawa wanaoomboleza kupitia twitter!
 
Mimi naamini sisi wananchi hatujui tunachokitaka . Hao jamaa wa Twitter wanapata nguvu zao ki katiba , katiba ambayo wananchi walikataa lakini hawapiganii kupata katiba mpya ya wananchi. Bora kina Lema wana ujasiri wa kukemea na kupambana lakini wananchi wanajuwa wanyonge sana kudai haki zao (Katiba yao, Tume huru)

Elimu ya wananchi katika haki na wajibu wao juu ya serikali yao inatia mashaka na ndiyo loophole wanayotumia watawala katika kukandamiza matakwa yao eg Zanzibar
 
Unyonge ukikithiri huzalisha uoga,kasi ya kuelimisha utambuzi si ndogo kama tudhaniavyo,iko siku ukandamizaji ambao ndiyo ugonjwa sugu nchini mwetu utapatiwa dawa,uvumilivu una kikomo
 
Haki gani haipo? Haki inaletwa na sheria

Sio kila Sheria ni Sheria ,nyingine zilitungwa kwa ajili ya Watu (kikundi) kwa manufaa yao kwa kufuata utaratibu/kanuni/na miongozo na sisi kutakiwa kuzifuata kwa shuruti..Sio Sheria zote zinatoa 'Haki' ndio sababu ya kufanyika kwa mabadiliko ya Sheria hizi ili kuendana na wakati uliopo..

Umeelewa ?..
 
Sheria inaleta haki?! Nani kakwambia hivyo? Kwa taarifa yako kitu pekee kinachopata kwa haki sisi binadamu ni kifo tu

Sawa

Sio kila Sheria ni Sheria ,nyingine zilitungwa kwa ajili ya Watu (kikundi) kwa manufaa yao kwa kufuata utaratibu/kanuni/na miongozo na sisi kutakiwa kuzifuata kwa shuruti..Sio Sheria zote zinatoa 'Haki' ndio sababu ya kufanyika kwa mabadiliko ya Sheria hizi ili kuendana na wakati uliopo..

Umeelewa ?..

Sijaelewa, naona unaongelea hisia badala ya facts.

1. Isingekuwa sheria, usingekuwa na haki kupiga kura (kuchagua ama kuchaguliwa).

2. Isingekuwa sheria usingekuwa na haki ya kulipwa nauli ya kwenda likizo (kama wewe ni mwajiriwa)
 
Bado hauja nielewa,rudia tena kusoma(unazoziita hisia) kwa makini utanielewa Mkuu.
 
Nina uhakika sana kwamba bwana Font Ford atamkalia Lema kooni kwa nguvu zote alizonazo.
Lema kura atapata tena sana, japo ya Kafulila yaweza kujirudia.
 
tatizo watanzania wenyew hamjaamua kama mkiamua sisi hatuna la kufanya
 
Nina uhakika sana kwamba bwana Font Ford atamkalia Lema kooni kwa nguvu zote alizonazo.
Lema kura atapata tena sana, japo ya Kafulila yaweza kujirudia.
Hivi huyo LEMA Mlishampitisha kama mgombea wa kudumu huko chama cha demokrasia hakuna tena kura ya maoni ?
 
Amani bila haki ni ubwegwe.unakuaje na amani ingali haki zako zinaminywa.bora ungesema utulivu na subira,maana hivyo ndo tulivyonavyo
Hata ninyi mkipata madaraka mtafanya mabaya zaidi ya hao waliopo tena bila utaratibu wa kiungwana kwendeni zenu manyumbu
 
3:24 AM
Kuna jambo limenikosesha usingizi na nikatamaani kushare na kamanda Lema na ma - great thinkers wote kwa pamoja.

Kamanda Lema pole sana kwa unayopitia kisiasa, hakika ni magumu kwa sasa na kwangu, hayana dalili za kuwa mepesi kwa siku za mbele.
Kuna watu ndani ya CCM , tena wenye nguvu na mamlaka wanaoonyesha waziwazi kwamba hawakutaki kama mbunge wa Arusha.

Wanafanya mengi kabla ya uchaguzi 2020 na watafanya maajabu hiyo 2020, my soul is a witness!
Kamanda, akumulikaye mchana, usiku atakuchoma!
Siandiki kukuogopesha, wala siandiki kukupa taarifa zozote mpya sana. Naandika nikisukumwa na wasiwasi wa kukusihi uwe na mbinu mbadala zaidi ya moja na nguvu ya umma iwe mbinu ya mwisho kabisa kwenye mpangilio na kwa umuhimu.

Kumbukumbu ya mauaji ya kihalaiki huko Rabaa inatoa mwangaza juu ya makosa makubwa ya kimkakati ya Muslim brotherhood huko Egypt kufuatia mapinduzi ya 2013 ya Mohamed Morsi.

August 14, 2013 ilikuwa siku ya machafuko zaidi katika historia ya karibuni ya Egypt. Majeshi ya ulinzi yalisambaza kikatili mno maandamano huko Rabaa al- Adawi square na Giza al- Nahda square kaskazini mwa Cairo.
Mamia ya waislam waliokuwa wakiandamana kupinduliwa kwa Morsi , rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Egypt, waliuawa.
Waangalizi wa haki za binadamu wanasema zaidi ya raia 800 waliuawa.

Lakini, mauaji ya Rabaa, kama yalivyokuja kutambuliwa, yalikuwa shule kwa jambo jingine: yalionyesha kushindwa kabisa kwa mikakati ya muslim brotherhood baada ya Morsi kung'olewa. Tokea hapo muslim brotherhood haijaweza kupata nafuu katika harakati zake kidini, kisiasa, wala kijamii. Wamebaki ndugu, kaka, ila si ndugu au kaka tena katika uislam~ muslim brotherhood.
Miaka karibuni minne sasa, mamia zaidi katika brotherhood wameuawa na taasisi ya Muslim brotherhood sio mdau mwenye nguvu tena katika harakati za Egypt.

MUSLIM BROTHERHOOD WALIKOSEA NINI?
1. Waliliamini Jeshi.
Viongozi wa brotherhood waliwaambia wanachama wao kuwa jeshi liko pamoja na Morsi, kitu ambacho hawakuwa na uhakika nacho.

2. Walipuuza uwezo wa Jeshi.
Pamoja na jeshi kuwa na ziada ya silaha, mafunzo na uwezo, Brotherhood waliamini kwa dhati wangeshinda mapambano.

3. Imani potofu.
Brotherhood waliamini kuwa ni majenerali wachache waliosupport kuangushwa kwa Morsi na hivyo mgomo wao ungefanya jeshi litawanyike na hivyo kurahisisha Morsi kurudi madarakani.

Brother Lema, umekuwa chachu na hamasa kwa vijana na umma kwa ujumla katika kudai haki. Umefanya mengi kwa mfano!
Umeonyesha kuwa uko tayari kushuka kwenye ndege ya vita katika uwanja wa mapambano wakwanza na kupakia wa mwisho.
Natamaani kukuona muda mrefu zaidi kwenye siasa za Tanzania ila kuwa makini na hawa wanaoomboleza kupitia twitter!
Sio kweli muslim brotherhood walipotwaa madaraka wakawahovyo zaid kuliki utawala wa mubarak hivyo wananchi wakisaidiwa na jeshi lao wajawaondoa madarakani.hivyo hivyo nyunbu lema akioata serikali atakuwa hovyo zaidi na wanchi haohao watamuondoa
 
Nina uhakika sana kwamba bwana Font Ford atamkalia Lema kooni kwa nguvu zote alizonazo.
Lema kura atapata tena sana, japo ya Kafulila yaweza kujirudia.
Nilijua utafika kusema Lema atapokwa kura. mara nyingi margin za ushindi Arusha ni kuanzia kura 10,000. Najiuliza ni adjustment kubwa kiasi gani itafanyika kumpoka mtu ushindi huku kata aidi ya asilimia 90 zikichukuliwa na upinzani. Ni kichaa peke yake anaweza fanya hivyo na kama ikitokea basi waliopiga kura bado watapiga kelele tu
 
Back
Top Bottom