Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
16,975
Reaction score
9,580
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema " MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA "

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia " Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa " Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona " NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani " Only time will tell " wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya " Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema " TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA "

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)
 
Siku zote nasema CHADEMA kina mkono wa MUNGU...

Asante sana Mungu, asante sana MAKAMANDA woote, asanteni sana watu wa ARUSHA......asante sana CHADEMA....
 
Ukiweza nenda kaweke Kambi kule Mtwara...Ingawa najua watakuzuia ...Lakini najua wewe ni kamanda usieogopa bwana Lema
 
Watz wa a town wengi wa wanavuta ganja na lema sijui yumo """ nenda mtwara kama una ubavu
 
Lema, name ninakupongeza sana kwa ushauri uliowapatia wapiga kura wa Arusha wanaopenda Amani, kuwa pamoja na kuwa mlijua mnafanya Uchaguzi katika sintofahamu kubwa, uliwaelekeza wapiga kura wakubali kusukumwa mara ya kwanza, ya pili na ya tatu lakini ya nne inabidi kutegemea busara ya Mungu. Ninakubaliana na hoja yako, watu wengine wanaotaka tuwavumilie wajue tuna uvumilivu wa kutosha lakini sisi nao ni binadamu, na ubinadamu sio Umungu, uvumilivu huisha.

Tunashukuru walitusukuma mara ya kwanza, ya pili na ya tatu tu, kila waliposogea wapiga kura waliimba Amani kwa Arusha, tunataka mabadiliko na Uhuru wa kweli. Wametuvika heshima. Arusha Mungu awabariki sana. Wote waliopigania ufanisi huo kwa kila hali hata waliojitolea naomba Mungu awabariki. Arusha sasa ni zaidi ya darasa kwa watanzania.
 
Watz wa a town wengi wa wanavuta ganja na lema sijui yumo """ nenda mtwara kama una ubavu

1002316_555828297812696_2004089766_n.jpg
 
G.Lema asante hata kwa kukumbuka kutoa neno la shukrani,
siyo kawaida kwa mwanasiasa kurudi na neno la 'ASANTE'

.........Asante zangu zikufikie kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Tanzania.

Asanteni sana wana Arusha wote kwa moyo wa ujasiri mlio nao, siyo rahisi
kwa mtu wa kawaida kupigwa bomu na bado ukazidi kuwa jasiri kama wana
Arusha.

Nilikuwa namshangaa sana Arushaone aliposema anasimamia wapiga kura
kweli nilimwambia 'take care yourself'. Lakini Mungu aliwapigania na zoezi
likaisha tena kwa mafanikio makubwa.

Natamani kuona Tanzania ikiwa chini ya chama cha CHADEMA, natamani kuiona tena
Tanzania inayoongozwa kwa haki.
 
Last edited by a moderator:
Ok sasa Mh Lema,nakuomba uhamasishe watu wajiandkishe kupiga kura hasa vijana na pia uwafundishe majimbo yote Tanzania mwaka 2015 tufanye mabadiliko ya kina na yenye tija kwa taifa,ili tutokomeze umaskini Tanzania
 
Najivuna sana kwamba sikupiteza kura yangu,najivuna kuwa na mbunge mwenye akili, najivuna kuwa na mbunge ambae nulishiriki kupiga kura na kulinda kura pale halmashauri hadi tukatangaziwa mshindi, hywa najisikia furaha ninapikuwa sehemu yoyote ya Tanzania kujitambulusha natoka A town na Mbunge wangu ni G Lema.

Huwanajisikia amani sana kujitoa kwa ajili ya Cdm, chama cha watu, hatuna bunduki, hatuna mabomu, hatuna polisi, a tuna MUNGU na pia Tuna WATU.

Naomba Ccm jifunzeni ilu muje kuwa wapinzani wazuri wa Chadema kwani anguko lenu ni dhahiri hamuwezi kulipinga hilo,
Badala ya kuendelea kutukana watanzania kuwadharau hata kufikia kuwaua kqa mabomu na risasi zilizonunuliwa kwa kodi zetu, kaeni na kutafakari mnapotaka kulipelwka hili Taifa. Kwani mwisho wa uvumilivu ni hatari.

Lema Mungu akulinde sasa na hata milele.

Kila mwenye nia mbaya na wewe umrudie yeye na kizazi chake chote.
Freedom is comming Today
 
Back
Top Bottom