Godbless Lema: Kuna vichaa wengi mitaani

Godbless Lema: Kuna vichaa wengi mitaani

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
ARUSHA JOTO la Uchaguzi linazidi kupanda mjini hapa, baada ya vijana takribani 1,000 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Jimbo la Arusha Mjini, kutangaza kutomsaidia Mbunge wao Godbless Lema wakati wa kampeni.

Vijana hao wakiongozwa na aliyekuwa dereva wa kwanza wa Lema ambaye pia alikuwa mratibu wa mawakala katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Rashidi Shuberti, wamekutana mjini hapa na kutangaza kupambana na mbunge huyo.

Wakati kundi hilo la vijana wakitangaza uamuzi wa kumwangusha Lema, Katibu wa Lema, Innocent Kisanyage aliliponda kundi hilo na kudai kuwa ni wahuni waliofukuzwa ndani ya Chadema siku nyingi.

Akizungumza na vijana hao jijini hapa jana Shuberti alidai alikuwa mstari wa mbele kwenye Kamati ya ushindi ya Lema mwaka 2010.

Alisema pamoja na kuongoza mapambano ya ushindi kwa kuwaongoza vijana wa Arusha Mjini sasa umefika wakati wameamua kupambana kuhakikisha Lema hashindi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktiba mwaka huu.

“Kwa bahati mbaya vijana wenzangu tuliaminishwa na kuanza kuhubiri Injili tusiyoijua ndani ya Chadema, kwani katika Injili hiyo wapo waliokufa, ndoa zao kuvunjika na wengine kupigwa risasi,” alisema Shuberti na kuongeza:

“Injili ile ya Chadema ilikuwa ni kupinga mfumo wa Chama cha Mapindizi (CCM), uliolazimisha haki na kanuni zivunjwe ili kuhalalisha mtu mmoja kuwa Meya wa Jiji la Arusha kinyume na kanuni na sheria,” alisema.

Alisema katika kupinga udhalimu huo alipewa jukumu la kuratibu maandamano ya kupinga matakwa ya CCM yaliyofanyika Januari 5, 2011 na kusababisha mauaji ya vijana watatu na majeruhi kadhaa. “Baadaye madiwani watano walifukuzwa katika chama kwa kumuunga mkono Meya Gaudence Lyimo.

Lakini miaka minne baadaye chama hicho hicho kikaa mezani kubariki mfumo kilioupinga na kusababisha vifo vya watu,”alisema Shuberti na kuongeza: “Nimetafari na vijana wenzangu tulivyopambana kumfikisha Lema alipo leo, tumehatarisha maisha yetu kwa asilimia 100.

Sasa kwa niaba ya wenzangu natangaza Lema hawezi kuwa Mbunge wa Arusha,”alisema . Shuberti alisema atahakikisha anashiriki kwa kiwango kile kile alichoshiriki kuhakikisha anamuangusha Dk. Batilda Burian aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CCM ili kuhakikisha Lema anashindwa uchaguzi.

MTANZANIA ilipomtafuta Lema kwa simu hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu na kuulizwa kama anamfahamu Shuberti alisema.

“Fedha ya CCM inaweza kutumika na vichaa wengi lakini haiwezi kuwasaidia CCM, Arusha hakuna CCM ila kuna bendera za CCM na muhimu CCM ifanye jitihada za kumpata mgombea ubunge, atakayeshindwa tena. “… kwani najua hawawezi kushindana na chama changu wala mimi hata kidogo kuna vichaa wengi mitaani,” alisema Lema
 
Haya bana ngoja tuweke akiba ya maneno na tuhifadhi huu Uzi hadi October sio mbali sana
 
Lema lazima tumuondoe Arusha, Hadhi ya Jiji la Arusha imepotea kabisa
 
hv hii habari imeandikwa kwenye GAZETI au KIPEPERUSHI? ama kweli kuna baadhi ya wandishi wenye njaa kali sana.
 
Lema lazima tumuondoe Arusha, Hadhi ya Jiji la Arusha imepotea kabisa

Unaota tu. Nakushauri kula fedha za ccm lkn Mbunge wetu ni Lema. Kwa juhudi za Lema huyo meya sasa ni bendera tu kwani hawezi kufanya lolote bila madiwani wa Chadema ambao ni wenyeviti wa kamati zote nyeti.
 
Na kweli kutokana na maelezo ya huyu dereva naamini kuwa kweli kitaa kuna vichaa wengi.
 
Kitakachomfanya Lema ashinde Arusha ni kura za Wanawake, Lema anapendwa sana na kina mama! Ambao wengi ndo wapiga kura.
 
Tuna macho tunaona.mkakati wa kumwondoa lema arusha ni mkakati wa ccm.mnaojidai ni chadema kumpinga ni vibaraka tu.

Hatakama ni chadema sana sio hivo mkuu . Nadhan kwa arusha lema inatosha halafu anatuita vichaa baada ya kuwa mbuge wew unaona Sawa tu
 
Kitakachomfanya Lema ashinde Arusha ni kura za Wanawake, Lema anapendwa sana na kina mama! Ambao wengi ndo wapiga kura.

Mimi siyo mwanamke lkn nampenda kwa ujasiri wake wa kuwaambia ukweli viongozi wa serikali wazembe,wanyanyasaji hasa polisi. na wabadhirifu.
 
Back
Top Bottom