Godbless lema: Historia itakukumbuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Godbless lema: Historia itakukumbuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Nov 3, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwako Mheshimiwa Lema

  Tukio la tarehe 31/October, 2011 la wewe Kukataa Dhamana hivyo kulazimika kwenda rumande katika Gereza la Kisongo kwa siku 14 limezungmzwa na Watu wengi sana na mpaka sasa limekuwa ni Gumzo sehemu mbali mbali za nchi yetu. Wapo waliokupongeza kwa uamuzi wako na wako waliokupuuza kwa Uamuzi wako kila mmoja akitoa sababu zake.

  Tukio ulilolifanya tarehe 31/October, 2011 limenifanya nikumbuke tukio lililotokea tarehe 16/October, 1953 katika Viunga vya Mji wa Havana Cuba kipindi cha Utawala Dhalimu wa Dikteta Fulgencio Batista. Ilikuwa ni Siku Fidel Castro alihukumiwa kwenda jela kwa Miaka kumi na tano kwa kosa la Uhaini. Katika kuhitimisha Speech yake ndefu aliyoitoa Mbele ya mahakimu waliokuwa wanamhukumu Fidle Castro alisema

  Maneno hayo ya Fidel Castro yamebeba ujumbe sawa kabisa na Maneno haya katika speech yako

  Ni maneno ambayo kama CCM na Serikali yake wangejua kwamba utakataa dhamana na kutoa huo Ujumbe basi usingepata Bahati ya kukamatwa. Nasema Bahati maana Tukio la kukamatwa kwako limekuwa Bahati Mbaya kwa Watawala na hakika Mtawala yeyote angejua nini kilikuwa kichwani mwako Angekupuuza wala asihangaika na wewe.

  Umekataa KUONEWA, umekataa DHULUMA, Umekataa MANYANYASO, Umetoa Ujumbe kwa wale wote wanatishwa na Magereza kwamba Hakuna Mahabusu inayoweza kuhifadhi UMMA kwa Pamoja, kwamba DHULUMA ikizidi sana BINADAMU anaweza akamfata hata Polisi mwenye Silaha. Nakumbuka wakati Red Indians wanadai uhuru kutoka kwa Mwingereza, walilala kwenye Reli Kupinga MANYANYASO na kudai UHURU na Haki na hata Dereva wa Treni wa Mwingereza alipopita Juu ya MIILI yao hakuna aliyeondoka reline hata Pale Derava alipoona kwamba Asingeweza kuwasaga Wote na Kusalimu Amri.

  Wengi wanaokuponda eti wanadai wewe ni mkorofi, Umefanya Maandamano bila Kibali, Ni wapuuzi tu maana wanafikiri Watanzania na wana Arusha hawakuona wale viwavi jeshi wa CCM a.k.a UVCCM walipofanya Mikutano na Maandamano Haramu chini ya OCD Fedhuli Zuberi, wanaokuponda wengi wetu ni Wasomi ambao wanafurahia hii AMANI feki ilihali Mama zetu

  wanajifungua kwa shida, Watoto zetu wanasoma katika mazingira Magumu, na Vijana wengi wanazidi kukosa Ajira na Maisha ya Mtanzania yanazidi kupanda.

  Nakupa Moyo Mh. Lema kwa Sababu UNAUNGWA MKONO na kundi ambalo halina Cha Kupoteza, Unaungwa Mkono na Makundi ya Watanzania waliopigika Kimaisha, Kundi ambalo Wapondaji wako akina Ngongo wanaliita ni Kundi la Jobless, kundi la wavuta Bangi , kwamba wote wanakuunga Mkono ETI WANAITWA Wavuta Bangi, lakini nikutie Moyo tu kwamba Hata Yesu alipokuja Duniani alisema
  “Sikuja duniani kwa ajili ya Watakatifu bali wenye Dhambi ili wapate kuokoka”, Kwa hiyo unapoona kwamba Unaungwa mkono na Wavuta bangi wengi, Jobless wengi usihudhunike maana hiyo inaashiria kwamba saa ya Ukombozi I Karibu Maana hata waliomng’oa Gadaffi au Mubarak walikuwa ni Jobless na Wavuta bange kama wapinzani wako wanavyowaita.

  Moto Uliouwasha ni Mkubwa na Kwa Kweli serikali ijiandae kujenga Mahabusu Nyingi maana watu sasa Hawataogopa Mahabusu, hawataogopa Risasi.

  Mungu Akuabriki sana

  Wako Katika Mapambano, Albedo

  Please Mod: naomba kwa heshima na Taadhima msiiunganishe hii thread maana nimeiadress kwa Mheshimiwa Lema. asante
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Lema ni santuri mpya kama kawaida..

  Mkuu impact yake ni ndogo sana wala haiwashugulishi serikali..

  Kwasababu mantiki ya mgomo hakuna kabisa..ni kero not well thought move above all nonsense.

  Huwezi kulinganisha na castro..castro kile kichwa kizuri ajabu..na mgomo wake ulikuwa na mantiki na well thought.
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri kama Serikali inaamini hivyo
   
 4. m

  marembo JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu Topic ni mfululizo wa watu mizigo kwenye JF. Tunahitaji kutoa mawazo na chachu mpya siyo kulaumu bila kujau sababu halisi za wanaharakati sio kutumiwa tu bora siku iende. hata kama ni hivyo visent vichache vya pilau na kofia, kanga chukua kiustaarabu basi bila kutoa pumba.
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hongera Lema jina lako lipo tayari kwenye kumbukumbu za watanzania wanaopigania amani na haki ya kweli.
   
 6. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  huna lolote ww nenda kahangaike na MoU na kanisa na mdini,mbaguzi mjenga chuki mwenzako muhamed said.
   
 7. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  hongera kamanda lema!
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nakuumiza sana mkuu wangu pole sana..

  Mimi napiga kotekote MoU, hapa nitakuwepo tu..

  Mdini ni wewe jitazame ulivyo bwabwaja ili kuni-provoke..kuwa mstaarabu acha udini tujadili kwa raha
   
 9. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwani Lema amefungwa pamoja na umma wa Arusha?last time i checked kuna watu walijaribu kuandaaa mgomo kuwahusisha wananchi wote wa Arusha lakini wananchi wa Arusha wakawapuuza na sasa wanaendelea na kazi zao kama kawaida bila kujali Lema amelala wapi.

  Sasa ni uamuzi wa Lema kama tarehe 14 tena atataka aendelee kulala within bars au atarudi nyumbani kwake, ni uamuzi wake na ni haki yake kufanya hivyo.
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ninaamini ule ujumbe wa Lema umebeba MUZIKI MKUBWA!!
  Muziki ambao jamii ina KIU ya kuucheza kama itasimamiwa vizuri. Jamii ya Tanzania kwa sasa imekadamizika hata karibu inapoteza utambulisho wake wa Utu na Ubinaadamu. Hizo ni nyaja za hatari sana kama akitokea mtu anayejua jinsi ya kushika Spana zake na kufungulia vuguvugu kupitia mfumo huo wa kijamii.

  Simuoni Kiongozi yeyote wa Kiserekali Mwenye UTU na UBINADSMU wa kutosha kuuelewa NGUVU iliyoko kwenye ujumbe ule. Muache Lema kama Mtu na jinsi unavyotak kumtafsiri. Jaribu kusikiliza ule Muziki kwenye waraka wake. Tafakari umebeba nini? Tatizo ni kuwa inabidi uwe na angalau hata kidogo tu punje ya utu na ubinadamu ili kuanza kuelewa jambo hili. LAKINI kwa sababu karibu wote wamepotoka, Utu wa familia, jamii na Taifa umetupiliwa mbali .. Viongozi wengi watafanyia mzaha jambo hili na kufikiri ni mzaha mwingine wa kufungia mwaka na hapo ....ndipo..ALBEDO .... anaposema Moto Uliouwasha ni Mkubwa na Kwa Kweli serikali ijiandae kujenga Mahabusu Nyingi maana watu sasa Hawataogopa Mahabusu, hawataogopa Risasi. Lakini. binafsi ninaamini hatutafikia hapo kwani serekali na jamii ya kitanzania ina Misingi ya Utu na ubinadamu ingawa kwa sasa inaporomoka kwa kasi .. HENCE Ujumbe wa LEMA!!
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kitu alichofanya Lema ni Ujumbe tosha kwa Wapambanaji kwamba Jela si Mahala pa kuogopa kwa mtu anayepigania haki. Kuhusu watu wa Arusha dah... Butola unanishangaza kwelilkweli hapo kwenye Blue Hivi hujui kama ni Nguvu ya Dola ndiyo ilitumika kuzima ule Mgomo? Watanzania tu Waoga sana hili sikatai ila Wanapotokea watu kama akina Lema inaleta hamasa na Ujasiri kwa watu. Hivi unaweza kukumbuka kwamba si Miaka mingi sana Watanzania walikuwa wanawaogopa sana Mabalozi, Sungusungu na Migambo? Unahisi watanzania watarudi huko? Unahisi watanzania ni binadamu wa Tofauti sana ulikinganisha na Wamisri, walibya, watunisia? kwamba wao wanaweza kuvulia mateso ya Milele, Manyanyaso ya Milele?

  If you are in that line of thinking naamini utakuwa ulizamia Kitambo Marekani na huna makaratasi
   
Loading...