Godbless Lema ataka wabunge wa CUF walioondolewa bungeni warejeshwe

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
lema.jpg

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutumia busara kuwaondoa bungeni wabunge nane walioingia bungeni kuziba nafasi za wabunge nane waliokuwa wamevuliwa uanachama wa chama cha CUF Julai 24.

Lema ametumia mtandao wake wa kijamii kuandika ujumbe huo ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananch CUF mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa.

“Mh Spika anapaswa, kuzingatia kwa busara uamuzi uliotolewa na mahakama kwa kuwaondoa wale Wabunge wa Lipumba ndani ya Bunge na kuwarejesha Wabunge halali sasa, Mpaka hapo haki itakaposhinda zaidi,”ameandika Lema
 
View attachment 629263

Lema asimfundishe spika kazi yake!!
 
..Lema ni mbunge wa Arusha mjini aliyechaguliwa kwa kura za wana nchi wake...hizo fitna zenu hazina tija siku hizi....mmeishiwa hoja mmebaki kupiga risasi watu wenye mawazo tofauti nanyi.... Hoja hapa ni wabunge walioshinda kesi kurudi bungeni....jadili hoja acha ubashite...

Huyu Lema si ndo yule anayetuhumiwa kuwa mwizi wa magari au ?
 
Ni aibu kubwa sana kwa kiongozi aliyetapika hadharani kuyarejea matapishi yake tena kwa amri simply because ulishupaza shingo kubeba ajenda fulani.
 
Walishafukuzwa uanachama kabla ya mahakama kutoa hiyo amri,na wengine walishaapishwa sasa hilo la kuwaondoa Bungeni wale walioapishwa na kuwarudishà wale waliofukuzwa linawezekanaje wakati kesi ya msingi bado haijatolewa uamuzi?,Ni kwanini walishindwa kuweka zuio Bungeni ili hawa wapya wasiapishwe?
 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma na Dodoma walihamishwa baada ya kuapishwa...
 
Back
Top Bottom