SI KWELI Godbless Lema amekiri CHADEMA imekufa kisiasa

SI KWELI Godbless Lema amekiri CHADEMA imekufa kisiasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna Habari Mpya Kuhusu Kauli ya Godless Lema

LEMA..19SEPT2025.jpg



LEMA.19SEPT2025.jpg


LEMA19SEPT2025.jpg
 
Tunachokijua
Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa grafiki za Jambo TV na Millard Ayo zikinukuu ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Godbless Lema kwenye mtandao wa X kuwa amekiri CHADEMA kufa kisiasa.

Je, ujumbe ulionukuliwa ni halisi?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu yaani (Key Word Search) umebaini kuwa ujumbe ulionukuliwa si halisi, bali ni wa kutengenezwa na wapotoshaji kwani haujachapishwa na Lema katika ukurasa wake kwenye mtandao wa X kama inavyoonekana.

Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo, ni za kughushi, kwani hazijachapishwa na (Jambo TV, Millard Ayo) kama inavyoonekana bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa potofu. Mfano grafiki iliyotumia utambulisho wa Millard Ayo muundo wake haufanani na machapisho rasmi kutoka kwenye chanzo hicho.​
Wakuu

Ni kweli kwamba Lema amesema CHADEMA imekufa kisiasa au ni uzushi tu?
 
Back
Top Bottom