Kazi kuuubwa kabisa na ya msingi sana na ya kishujaa ambayo Mheshimiwa Godbless John Lema ameifanya hapa Arusha na kupitia jimbo hili; katika NJI nzima ni kuleta UKOMBOZI WA FIKRA na MWAMKO WA kujiamini; Kujitambua na Ujasiri wa kuzijua haki zao na kuzitetea kwa hali na mali pale inapobidi miongoni mwa wananchi.
Hii ni sawa na kazi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; RIP; alizozifanya kati ya mwaka 1953 na mwaka 1961; UKOMBOZI WA FIKRA; KUJITAMBUA; KUJUA UTU WAO NA KUJENGA UJASIRI MIONGONI MWA RAIA na kuwawezesha kukabiliana na wakoloni mpaka Uhuru ukapatikana. Mwalimu Nyerere hakufanya kazi ya kujenga barabara, zahanati wala shule katika kipindi cha vuguvugu la ukombozi; kazi hizo alizianza mara tu baada ya Tanganyika kujipatia uhuru na baada ya miaka 10 ya uhuru aliwakaribisha wakoloni akiwemo gavana wa mwisho wa mwingereza Sir Richard Turnbull mwaka 1971 waje kujionea hatua tuliyofikia katika kipinda kifupi tu cha miaka 10; moja ya vielelezo vikubwa ni uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.
Bravo GJL; Tutakuchagua kwa kishindo Kamanda uendelee na kazi ya kuongoza mapambano dhidi ya mkoloni mweusi CCM