Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 62,452
- 104,621
Kuna watu wengi(wafanyabiashara na wafanyakazi) wananununua bodaboda na kwawakabidhi vijana kwa mkataba ambao huwaletea makusanyo kila siku au kila wiki. Hawa hawawezi kukubaliana na Lema kamwe.
Kuna watu wengi wana wafanyakazi wa kusaidia kazi(house girls na houseboys) majumbani kwao kwa ujira wa unyonyaji, malipo ya kujikimu tu. Hawa pia sio rahisi kukubaliana na hoja ya Lema.
Kuna watu wengi na kampuni wanaajiri vijana katika biashara zao, kampuni, viwanda au mashamba. Wengi wa hawa vijana wanalipwa ujira mdogo sana na kuwafanya wengi kufa wakiwa katika lindi la umaskini hata kwa kufanya kazi miaka mengi. Hawa hawawezi kukubaliana na Lema.
Ukiacha wale ambao wanaona bodaboda ni ajira nzuri tu na haina shida yoyote, Wengine wengi wanampinga Lema kwa nguvu zote kwa sababu wasingependa kuingia katika "slippery slope" na "contradictions".