God created the world but Dutch created Holland

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
964
1,687
Wana historia yao kubwa sana kwenye uso wa dunia, wataalamu sana wa kuanzisha kitu kipya hawa waholanzi, kwenye Jiographia pale kidato cha pili si mlipitia Land reclamation, si ndio hawa jamaa waliodai God created the world but Dutch Created Holland.
.
Usisahau pia hata kwenye soka ni hawa Wadachi wanajiita wataaalamu wa kusample na kuibua vipaji, klabu zao zinafanya makubwa sana kwenye soka la vijana ila Ajax ni balaa zaidi, wanakwambia mpango wao ni kumsuka kinda kuwa mchezaji mkubwa.
.
Pale shuleni kwao walipita Daley Blind, Wesley Sneidjer, Frankie De Jong(fundi wa mpira), Christian Erriksen na mafundi wengine, hawa wote ni mashahidi ya kinachoendelea pale kwenye shule zao.
.
Unafahamu kuwa kwenye Academy wachezaji hupewa maswali (Questionnaires) kupima ufahamu wao, unafahamu kuwa kuna psychology test pale kwao na wajua kuwa walifanya utafiti wakagundua makinda wanaolelewa na mzazi mmoja pekee huwa wanakuja kuwa mastaa wa dunia, Huyo ndio Mdachi bwana.
.
Wakaja na TIPS Model hii ni kifupi cha Technique, Insight, Personality na Speed, waliamini framework hii italeta vijana bora pale, Technique ni ujuzi wa mchezaji, Insight ni Ufahamu kwamaana mchezaji atakuja na kitu gani kwenye hali ngumu uwanjani, Personality ni Tabia ya mchezaji hapo kijamii zaidi na mwisho ni Speed hapa waligawa kasi ya mwili na kasi ya akili kufikiri haraka.
.
Ukipita humo basi umefaulu mitihani yao kwakuwa utakuwa umeswitch kwenye mfumo wao, hao ndio Wadachi bwana, walimchukua Lassa Schone kiungo mmoja mzito, ila ndani ya mwezi kupitia hiyo Model kipengele cha Speed jamaa aliiva na kuwa mpya.
.
Ndani ya Ajax mchezaji hachezi tu mchezo mmoja pekee, hivi ulishawahi fahamu kuwa Cruyff alikuwa fundi sana wa Baseball, uliwahi jua kuwa Van Basten ni fundi wa table tennis, wao wanaamini michezo huchangamsha akili ya mchezaji.
.
Ajax ndio Uholanzi na Uholanzi Ndio Ajax, na huo ndio Mpira wa miguu no shortcuts.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom