A
Anonymous
Guest
Goba bana kero ya maji kwenye hii mitaa yetu ni kero kubwa sana jamani, maji tunapata mara moja kwa mwezi na sio ya uhakika, tumeshalalamika mno, kiangazi ndo inakua balaa kabisa wakati huu wa mvua tukahisi kutakua na unafuu lakini wapi...
Tumeshalalamika mpaka kwa enzi za Naibu Waziri Mkuu Bwana Biteko ila wapi, waziri Aweso hana habari na sisi wala nini, tumezungukwa na kata zinazopata maji masaa 24 ila Goba ni kipengele sana, mpaka tunahisi mradi wa maboza yakuuza maji ni ya viongozi ndomana hawataki kututalia tatizo la maji Goba.
Labda tukiweka hadharani namna hii watasikia na kutupa suluhisho, bills wanakusanya tu ila huduma hafifu sana, ni hudhuni kubwa kwakweli.
Acha tu nitoe lawama maana hakuna matumaini kabisa.