Global Peace Index 2020, Kenya yaburuta mkia

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
TANZANIA YA SITA(6) KWA AMANI NA UTULIVU AFRIKA KENYA YA 119

Ripoti ya Global Peace Index ya mwaka 2020 inaonesha kwamba watu milioni 971 duniani wanaishi katika maeneo ambayo yana kiwango cha hali ya juu cha mabadiliko ya hali ya tabia nchi (Climate change). Kati yao watu milioni 400 sawa na asilimia 41% wanaishi katika nchi ambazo zina kiwango kidogo sana cha amani na utulivu hapa duniani.

Taarifa ineleza kwamba wananchi katika nchi zinazo tajwa kuwa na amani duniani wananchi wanajisikia amani hata wanapotembea pekee yao nyakati za usiku.

Pia wananchi wanaimani kubwa na majeshi yao hususani jeshi la polisi n.k. Ripoti inaeleza kwamba migogoro na machafuko ambayo yametokea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita yameanza kupungua ingawa mivutano mipya ya ndani na nje ya mipaka imeendelea kutokea duniani.

NCHI ZENYE KIWANGO KIKUBWA CHA AMANI AFRIKA.

1. BOTSWANA ya kwanza kwa amani na utulivu Afrika na ya 30 duniani

2. MALAWI ya pili kwa amani na utulivu Afrika na ya 40 Duniani

3. GHANA ya tatu kwa amani na utulivu Afrika na ya 44 Duniani.

4. ZAMBIA ya nne kwa amani na utulivu Afrika na ya 48 Duniani

5. SIERA LEONE ya tano kwa amani na utulivu Duniani na ya 52 Duniani

6. TANZANIA ya sita kwa amani na utulivu Afrika na ya 54 Duniani

7. SENEGAL ya saba kwa amani na utulivu na ya 58 Duniani.

8. LIBERIA ya nane kwa amani na utulivu Afrika na ya 59 Duniani

9. NAMIBIA ya tisa kwa amani na utulivu Afrika na ya 60 Duniani.

NCHI5 ZENYE VIWANGO VYA AMANI NA UTULIVU VYA HALI YA JUU DUNIANI

1.ICELAND
2. NEWZELAND
3. PORTUGAL
4. AUSTRIA
5. DENMARK
6. CANADA
7. SINGAPORE
8. SLOVENIA
9. JAPAN
10. CZECH REPUBLIC

NCHI 10 ZENYE VIWANGO VIDOGO KABISA VYA AMANI DUNIANI

1. AFGANSTAN ya 163 kwa amani Duniani.

2. SYRIA ya 162 kwa amani Duniani.

3. SOUTH SUDAN ya 161 kwa amani Duniani

4. YEMEN ya 160 kwa amani Duniani

5. IRAQ ya 159 kwa amani Duniani

6. SOMALIA ya 158 kwa amani Duniani.

7. JMHURI YA AFRIKA YA KATI ya 157

8. LIBYA ya 156

9. DRC ya 155

10. RUSSIA 156

KWA UPANDE WA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI.

1. TANANIA Afrika Mashariki ya 6 Afrika na ya 55 duniani

2. RWANDA katika nchi za Afrika Mashariki na nchi ya 79 kwa amani Duniani

3. UGANGA kwa nchi za Afrika Mashariki ya 105 kwa amani Duniani.

4. KENYA kwa nchi za Afrika ya Mashariki ya 119 kwa amani Duniani

5. BURUNDI kwa nchi za Afrika ya Mashariki ya 135 kwa amani Duniani.

6. SUDANI KUSINI kwa nchi za Afrika Mashariki na ya 161

HITIMISHO
Kenya nyie hakuna mnachoweza.

Link: https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjAMegQIARAB&usg=AOvVaw23MU5nuBpux26hCyiOsKuK
View attachment 1538061View attachment 1538063View attachment 1538064
 
Hata kwa Slums tupo juu
117944769_392147518424324_440453767193753600_o.jpg

Kwa ku-google Kenya Tanzania wameongoza
2484593_most.jpg
 
Mtu unatembea njiani ukihofia kutekwa na Alshabab huwezi kuwa na amani

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Mtu unatembea njiani ukihofia kutekwa na Alshabab huwezi kuwa na amani

Mungu Ibariki Tz - MITz
Sio alshabab tu, generally Kenya kuna Ujambazi mkubwa sana wa kutumia silaha na vibaka ni wengi mitaani, ni kawaida mtu kuvamiwa na vibaka uchochoroni huku watu wengine wakiona na kuendelea na shughuli zao kama kawaida bila kufanya lolote
 
Mtu unatembea njiani ukihofia kutekwa na Alshabab huwezi kuwa na amani

Mungu Ibariki Tz - MITz
Ila MK 254 ana amani Kwa kutumia njia ya kujitoa ufahamu!!! Anajitoa ufahamu halafu anaamini Marekani hakuna corona!!!! Lakini Tz kumejaa corona! Anaamini India hakuna corona Kwa hiyo hakuna kuwaweka wahindi karantini wakija Kenya! Pia anaamini Kenya hakuna corona ila Tz kuna corona!! Kwa kuamini hivyo MK254 ana amani sana!!! Japo ameshindwa kuishawishi dhamiri yake ikubali kuwa ana amani! Mh. *h* r* kadhalika.
 
Ila MK 254 ana amani Kwa kutumia njia ya kujitoa ufahamu!!! Anajitoa ufahamu halafu anaamini Marekani hakuna corona!!!! Lakini Tz kumejaa corona! Anaamini India hakuna corona Kwa hiyo hakuna kuwaweka wahindi karantini wakija Kenya! Pia anaamini Kenya hakuna corona ila Tz kuna corona!! Kwa kuamini hivyo MK254 ana amani sana!!! Japo ameshindwa kuishawishi dhamiri yake ikubali kuwa ana amani! Mh. *h* r* kadhalika.
Anamatatizo makubwa sana ya saikolojia mk 254 .msamehe bureeee mkuu
 
Back
Top Bottom