kwanza si kweli kwamba Mubarak hakuua Waandamanaji, zaidi ya Wamisri 300 walikufa katika maandamano yale.
pili waandamanaji wa amani hawawi na silaha za kulipua vifaru, silaha za kulipua ndege, n.k
Tatu azimio la kulinda wananchi wa libya inaonekana Nchi za magharibi wanalitumia kusapoti waasi wakati hawatakiwi "kutake sides". hii inaonyesha malengo yao yanakwenda beyond kulinda civilians, bali kutoa air cover kwa waasi ili wamng'oe Gadafi. na hii kusema kweli ni precedence mbaya sana, next time watatumia excuse hiyo hiyo ya kulinda Civilians ili kutoa kipondo kwa nchi hasimu zao kama Iran na nyinginezo.
Kwa mtu yeyote mpenda Uhuru wa Kujitawala hana budi kulaani kitendo cha nchi hizi kuconspire kuipiga Libya. na ili kujua unafiki wa nchi hizi, hawataachia waasi kuichukua Tripoli kwa nguvu , watalazimisha mazungumzo baina yao na Gadafi, ili Gadafi asije akacollapse kienyeji kienyeji na hatimaye kusababisha Chaos ya Civil war ambayo lawama na Gharama zitawarudia wao. hii air operation wanayoifanya ni kujaribu kuwa na "upper hand" kwa wote, waasi na Gadafi, kwa waasi watahakikishiwa mikataba minono ya mafuta, na kwa gadafi atawahakikishia anaondoka salama, ili kuwapoza wafuasi wake wasiendeleze armed struggle, iwapo Gadafi atakamatwa na majeshi ya waasi au hata kuuawa. wewe Subiri uone.