Global Fund msilete fedha za dawa za Malaria( ALU) wala Dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs)

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,599
3,647
Nawasihi wahisani (Global fund) wajitoe kuleta fedha za dawa za malaria na dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi kwani Tanzania tunafedha za kutosha mpaka tumeamua kugawana kama njugu. Malaria ni ugonjwa hatari sana tena unaua kwa haraka, Ukimwi ndiyo hivyo tena. Sasa ili serikali hii ikose pesa za kufuja, nawasihi wahisani msilete fedha hizo, kwani baada ya hapo ALU itauzwa Tshs 15,000/= kwa dose moja, ARVs zitauzwa kopo moja Tshs 90,000/= kwa dozi ya mwezi mmoja. Naamini Watanzania tutapukutika (kufa) kwa kasi ya ajabu {MUNGU atusamehe}. Ila baada ya hapo labda Wale wenye mahaba na CCM ndiyo wataelewa kuwa hiki chama hakifai kwa maslahi ya umma inabidi kiondolewe.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom