Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,778
- 730,066
Kutoka hapo ndio uumbaji ukaanza, kwa kutenga kiza na nuru...kwahiyo ikawa usiku(kiza)siku ya Kwanza.
Ukiacha kiza kinachofuata ni maji lakini leo hatujadili maji tunajadili kiza
Ni Kutoka kwenye giza ndio utenganisho wa vitu ukaanza rasmi
Kiza ndio kimekuwa ndio chanzo na asili yetu huu ndio ulimwengu wenye nguvu kuliko ulimwengu mwingine wa nuru.
Bara la afrika linapoitwa bara la giza... Kwa mtazamo hasi watu hawajui tu kuwa ule si mtazamo hasi, kiroho ni kitu kingine tofauti chenye nguvu kubwa --achana na mambo ya ulimwengu wa nuru mambo ya sayansi tech madaraka na siasa.
Hata historia inathibitisha kwamba binadamu wa Kwanza kuishi duniani alitokea Africa Tanzania black continent.
Kwahiyo wandugu kiza ndio kila kitu na matendo ya kiza sio matendo ya hiari huja na kuondoka kwa wakati wake.
Unapotaka usione kitu kitendo cha Kwanza cha haraka kinachokuja automatically ni kufumba macho ama kuyaziba, tendo la hiari la kugeuka hufuata baadae kabisa.
Lakini mwili Unapotaka kupumzika hujikuta bila kutegemea macho huwa mazito na baadae kulala kabisa, na huwezi kulala umekodoa macho ni lazima urudi kwenye asili yako...! Kizani! Unaweza kuwa bingwa wa kukesha ama hata kuwasha mataa mengi ili kufukuza giza lakini huwezi asilani. Kiza ni kiza na hakuna mwanga uwezao kufunika kiza chote.
La mwisho na la muhimu kujua ni kwamba mwisho wetu (kufa) ni kurudi kwenye asili na ndio maana hata ukifa umekodoa macho waliopo hukusaidia kukufunika.
Tafsiri yake ni moja.... Unaaambiwa rudi kwenye asili yako
Shetani mwenye nguvu sana na matendo yake yanayovuta mamilioni ndio mungu wa ulimwengu wa kiza... Unavutwa bila hiari bila utashi, unafanya kisha unajuta sana lakini unarudia yale yale ya giza. Usijilaumu sana KIZA NDIO ASILI NA CHANZO CHA UUMBAJI
Jr.!