Gigy Money afungiwa miezi 6 na BASATA

Faith Luvanga

Member
Sep 7, 2020
7
45
Baraza la Sanaa nchini Tanzania (BASATA) limemfungia kwa muda wa miezi sita (6) msanii wa Muziki wa Bongo Flava Gift Stanford Joshua maarufu kama Gigy Money, kwa kile kinachodaiwa kuwa msanii huyo alipanda jukwaani kutumbuiza katika tamasha la Wasafi Tumewasha Tour lililofanyika Jijini Dodoma Uwanja Jamhuri, kisha akavua gauni (dela)na kubaki na vazi ambalo lilikuwa linaonyesha maungo yake mwili na hivyo kuudhalilisha utu wake na kubughudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya Tanzania.

Adhabu hiyo imetolewa na Baraza hilo kupitia Taarifa yake kwa Umma ikieleza kuwa Kitendo hicho alikifanya huku akifahamu kuwa tukio linarushwa mubashara na televisheni ya Wasafi na kuonwa na watu wa rika mbalimbali na hivyo kwenda kinyume na Kanuni za Baraza za mwaka 2018.

Baraza limesema kuwa limejiridhisha kuwa msanii huyo alikiuka maadili ya kazi za sanaa kwenye Tamasha husika na kukiuka kifungu 4(L) cha Sheria NO. 23 ya mwaka 1984 (Re:2002), Kanuni 25 (6) (9) ya kanuni za Baraza za mwaka GNN.43/2018 na taratibu za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini.

Baraza limefafanua kuwa msanii huyo alishaitwa mbele ya Baraza na kuonywa mara kadhaa kwa vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kuahidi kutorudia tena. Kutokana na ukiukwaji huo wa Sheria, Kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza limemfungia kujihusisha na shughuli za sanaa kwa kipindi cha miezi sita(06) ndani na nje ya nchi na kulipa faini ya shilingi za Kitanzania Milioni moja (1,000,000/=) kwa kosa hilo. Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1) (a)-(i) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018.

Mwisho wa taarifa yake Baraza hilo limewakumbusha wasanii wote nchini kufanya shughuli za Sanaa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,678
2,000

Hehehehe
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
17,065
2,000
Wameuliza watu kuwa tumebugudhiwa au tumependa.. waulize waone kama watu hawajajibu liwe zoezi endelevu..😂
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
53,525
2,000
Wameuliza watu kuwa tumebugudhiwa au tumependa.. waulize waone kama watu hawajajibu liwe zoezi endelevu..😂
mimi nimebugudhiwa na na zile ndala kifuani mixxer still wire za hovyo kabisa yana rangi ya kahawia.
 
Kapumpuli

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,082
2,000
Mwenye picha jamani tulioko kisaki na sisi tumjue
Hii hapa Mkuu... Ichunguze alafu utoe maoni yako
Screenshot_20210105-182255~2.jpeg
 
Jensen salamone

JF-Expert Member
Sep 28, 2019
312
1,000
Basata waache uonevu na ushamba....

Kama wameamua kusimamia hicho wanachokiita 'maadili' waanze na hawa...

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,240
2,000
SASA HAO BASATA WALITARAJIA TUTAIONA VIPI ILE MIKUNJO YA PAPA YA GIGY MONEY??
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
23,252
2,000
Haya mambo yaruhusiwe.

Show iwe branded haifai kwa walio na umri chini ya 18 kama sigara.

Show zirushwe kuanzia usiku tunaoamini under 18 wamelala.

Tunafungiana kwa mambo ambayo tungeweza kukaa chini na kusolve kama watu tuliostaarabika tunaolenga sanaa imsaidie msanii.

Huko basata toeni hao mababu tuajiriwe vijana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom