Gharika CCM: Viongozi na wanachama 1,005 wahamia CHADEMA Kagera

Neno la yule Bwana likanijia tena, "Unaona nini?'' Nikajibu, "Ninaona vyungu vinne vinavyochemka vikiwa vimeinama midomo yake ikielekea upande wa kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi.''. Yule Bwana akaniambia,

Kutoka
pande zote nne za nchi hii, maandamano makubwa yatatokea na maafa yatamwagwa kwa wale wote watendao maovu na kufisidi mali ya UMMA. Mwenyezi Mungu atatoa hukumu yake kwa serikali hii kwa sababu ya uovu wao wa kuwasahau wananchi na kutanguliza matumbo yao na ya familia zao. Polisi wao watakuja na silaha zao, kuzunguka pande zote nne za miji ili kuwalinda na Ghadhabu ya UMMA, lakini hawatawashinda, kwani Mungu wenu atakuwa pamoja Nanyi
 
Neno likanijia kusema, “Je, Entrepreneur unaona nini?’’ nami nikajibu, “Naona mwamko mpya wa kisiasa na uamsho mpya wa kiroho, ukiwahamisha wanaCCM kwenda CHADEMA.’’ Yule Bwana akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba nimelitimiza.’’

Sugu kasema mkisema huu ni upepo tu si kweli kama ukishindwa kung,oa nyumba basi utaweza kung,oa paa na mabati yake
 
Neno likanijia kusema, “Je, Entrepreneur unaona nini?’’ nami nikajibu, “Naona mwamko mpya wa kisiasa na uamsho mpya wa kiroho, ukiwahamisha wanaCCM kwenda CHADEMA.’’ Yule Bwana akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba nimelitimiza.’’

Ha ha ha ha ha ha ha!

Ewe Kiamutwara, Kiziba, Ihangiro, Kihanja, Bugabo, Maruku, Missenye; nchi zile magharibi mwa Ziwa lile Kuu. Je, sikuwachagua ninyi kutuliza kiu yenu katika mto ule mkuu ambao nabii wangu Musa alizaliwa humo na kuyanywa maji yake?

Je, haikuwapasa kuwa dira katika taifa lenu kwa kusimika wakuu katika wakuu ambao wangelitiisha taifa langu na watu wangu na mazuri yote niliyoyaweka katika udongo na maji yaliyo humo? Sikuwapa babu zenu taifa hilo kuwa urithi wenu?

Kwa kuwa mmegeuza mioyo yenu kwa kuwachagua wenye haki, nimebadili kusudio la nafsi yangu bali mkikengeuka tena hakika mtaangamia; asema Mwenye Kumiliki Mbingu na Ardhi.
 
Neno la yule Bwana likanijia tena, “Unaona nini?’’ Nikajibu, “Ninaona vyungu vinne vinavyochochemka vikiwa vimeinama midomo yake ikielekea upande wa kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi.’’. Yule Bwana akaniambia,

Kutoka
pande zote nne za nchi hii, maandamano makubwa yatatokea na maafa yatamwagwa kwa wale wote watendao maovu na kufisidi mali ya UMMA. Mwenyezi Mungu atatoa hukumu yake kwa serikali hii kwa sababu ya uovu wao wa kuwasahau wananchi na kutanguliza matumbo yao na ya familia zao. Polisi wao watakuja na silaha zao, kuzunguka pande zote nne za miji ili kuwalinda na Ghadhabu ya UMMA, lakini hawatawashinda, kwani Mungu wenu atakuwa pamoja Nanyi

Mkuu wangu unanimaliza
 
pipoziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
KATIBU wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Byarushanje kata ya Katoke, wilayani Muleba, Kagera, Evelina Eladius (36), amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uamuzi wa katibu huyo umetokana na wanakijiji 1,005 waliokuwa wanachama wa CCM kukihama chama hicho hali iliyompa wakati mgumu katika utendaji wake hususan kazi za chama hicho.

Evelina alitangaza uamuzi huo hivi karibuni wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji mdogo wa Izigo ambapo katibu huyo na mumewe Eladius Theobald walipokea kadi za CHADEMA kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Bukoba mjini, Victor Sherejei.

“Kujiunga kwetu CHADEMA ni kama tumechelewa kwani kati ya watu wazima wakazi wa kijiji chetu wapatao 2,620 CHADEMA imevuna wanachama 1,005 nina imani kwamba baada ya sisi kuondoka CCM wengine wengi watatufuata,” alisema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Byarushanje Leonidas Bayona alisema nguvu ya CHADEMA ni kubwa kwani miongoni mwa wajumbe 25 wa serikali ya kijiji hicho 20 wanatoka CHADEMA.

Kwa mujibu wa Evelina ameondoka CCM baada ya kuchoshwa na uongo wa miaka 50 ya chama tawala ambapo huwajali viongozi na wanachama wake wakati wa uchaguzi ili kutafuta kura.

Alisema amebaini ubovu wa CCM baada ya miaka tisa aliyoitumikia kwa nafasi ya katibu wa tawi UWT na miaka sita aliyokuwa katibu wa CCM kata ya Katoke.

Mkutano huo ulihutubiwa pia na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Bukoba Mjini, Renatus Kilongozi, Diwani wa Rwamishenyi Dismas Rutagwelera (CHADEMA) na Katibu wa CHADEMA jimbo la Muleba Kaskazini, Salehe Mashaka.

Source: Tanzania Daima

huo ni moshi tu moto unakuja ccm/magamba kaa chonjo
 
Hiki ndicho chama kilichoitwa cha uchaguzi but now siyo cha uchaguzi tena ila ni chama cha siasa chenye lengo la kushika dola inshala!!!!!!!!!!!!!!! mungu atajalia
 
Tatizo ni jinsi serikali ilivyoshukughulikia taarifa za kamati mbalimbali katika bunge lililopita, lakini hatua mwafaka zikichukuliwa imani ya watu kwa chama tawala inaweza kurejea tena. vinginevyo hata viongozi wa ngazi za wilaya na mikoa wanaweza wakaanza kuondoka. Hii ni hatari sana kwa usalama wa taifa kwani ni sawa na tatizo linapotokea kwenye meli halafu nahodha na mabaharia wote wanajitosa baharini wanawaacha abiria peke yao.:crying:
Kama wameanza kuondoka huku chini, hao wa Wilaya na Mkoa watasimama vipi! CCM kwishney!
 
KATIBU wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Byarushanje kata ya Katoke, wilayani Muleba, Kagera, Evelina Eladius (36), amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Uamuzi wa katibu huyo umetokana na wanakijiji 1,005 waliokuwa wanachama wa CCM kukihama chama hicho hali iliyompa wakati mgumu katika utendaji wake hususan kazi za chama hicho.
Evelina alitangaza uamuzi huo hivi karibuni wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji mdogo wa Izigo ambapo katibu huyo na mumewe Eladius Theobald walipokea kadi za CHADEMA kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Bukoba mjini, Victor Sherejei.
“Kujiunga kwetu CHADEMA ni kama tumechelewa kwani kati ya watu wazima wakazi wa kijiji chetu wapatao 2,620 CHADEMA imevuna wanachama 1,005 nina imani kwamba baada ya sisi kuondoka CCM wengine wengi watatufuata,” alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Byarushanje Leonidas Bayona alisema nguvu ya CHADEMA ni kubwa kwani miongoni mwa wajumbe 25 wa serikali ya kijiji hicho 20 wanatoka CHADEMA.
Kwa mujibu wa Evelina ameondoka CCM baada ya kuchoshwa na uongo wa miaka 50 ya chama tawala ambapo huwajali viongozi na wanachama wake wakati wa uchaguzi ili kutafuta kura.
Alisema amebaini ubovu wa CCM baada ya miaka tisa aliyoitumikia kwa nafasi ya katibu wa tawi UWT na miaka sita aliyokuwa katibu wa CCM kata ya Katoke.
Mkutano huo ulihutubiwa pia na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Bukoba Mjini, Renatus Kilongozi, Diwani wa Rwamishenyi Dismas Rutagwelera (CHADEMA) na Katibu wa CHADEMA jimbo la Muleba Kaskazini, Salehe Mashaka.

Source:Tanzania Daima
CDM hata ikivuna vidagaa wote ccm bado itakuwa imara
 
Neno likanijia kusema, “Je, Entrepreneur unaona nini?’’ nami nikajibu, “Naona mwamko mpya wa kisiasa na uamsho mpya wa kiroho, ukiwahamisha wanaCCM kwenda CHADEMA.’’ Yule Bwana akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba nimelitimiza.’’

i like this,...
 
Back
Top Bottom