Gharika CCM: Viongozi na wanachama 1,005 wahamia CHADEMA Kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharika CCM: Viongozi na wanachama 1,005 wahamia CHADEMA Kagera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Apr 25, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  KATIBU wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Byarushanje kata ya Katoke, wilayani Muleba, Kagera, Evelina Eladius (36), amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Uamuzi wa katibu huyo umetokana na wanakijiji 1,005 waliokuwa wanachama wa CCM kukihama chama hicho hali iliyompa wakati mgumu katika utendaji wake hususan kazi za chama hicho.

  Evelina alitangaza uamuzi huo hivi karibuni wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji mdogo wa Izigo ambapo katibu huyo na mumewe Eladius Theobald walipokea kadi za CHADEMA kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Bukoba mjini, Victor Sherejei.

  “Kujiunga kwetu CHADEMA ni kama tumechelewa kwani kati ya watu wazima wakazi wa kijiji chetu wapatao 2,620 CHADEMA imevuna wanachama 1,005 nina imani kwamba baada ya sisi kuondoka CCM wengine wengi watatufuata,” alisema.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Byarushanje Leonidas Bayona alisema nguvu ya CHADEMA ni kubwa kwani miongoni mwa wajumbe 25 wa serikali ya kijiji hicho 20 wanatoka CHADEMA.

  Kwa mujibu wa Evelina ameondoka CCM baada ya kuchoshwa na uongo wa miaka 50 ya chama tawala ambapo huwajali viongozi na wanachama wake wakati wa uchaguzi ili kutafuta kura.

  Alisema amebaini ubovu wa CCM baada ya miaka tisa aliyoitumikia kwa nafasi ya katibu wa tawi UWT na miaka sita aliyokuwa katibu wa CCM kata ya Katoke.

  Mkutano huo ulihutubiwa pia na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Bukoba Mjini, Renatus Kilongozi, Diwani wa Rwamishenyi Dismas Rutagwelera (CHADEMA) na Katibu wa CHADEMA jimbo la Muleba Kaskazini, Salehe Mashaka.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. D

  DOMA JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  M4c viva chadema moto huu huu
   
 3. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Tunawakaribisha sana
   
 4. b

  boaz ngara Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwa hilo bando huku kwetu ngara maana naona hawa magamba hawataki kuvua
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hivi huu ni UPEPO tu unapita ama ndiyo SUNAMI yenyewe.
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Neno likanijia kusema, "Je, Entrepreneur unaona nini?'' nami nikajibu, "Naona mwamko mpya wa kisiasa na uamsho mpya wa kiroho, ukiwahamisha wanaCCM kwenda CHADEMA.'' Yule Bwana akaniambia, "Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba nimelitimiza.''
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Big up mkuu ulivyoandika.Nimeipenda sana
   
 8. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  waitu nyegera mawe.

  hii ni move nzuri kwa maana walikuwa wakisema kuwa cdm iko mijini tu. Naona hiyo ilikuwa ni wapi pa kuanzia lakini kama ndio kimeingia huko, kazi ya ukombozi karibia itakamilika.
   
 9. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CDM hata ikivuna vidagaa wote ccm bado itakuwa imara
   
 10. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu aendele kutupa umoja.

  2015 ifike salama.

  M4C.
   
 11. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ukiona mpaka dagaa wanavunwa ujue samaki walishavunwa zamani!
   
 12. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Peeeeeeeeeoooooppppllllleeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzzzzzz.................PPPPPOOOOOOOOOOOOWWWWWWWWWWEEEEEEEEERRRRRRR.
   
 13. w

  wamwala Senior Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viva CDM, natazama mbele yangu naona neno UKOMBOZI UMEWADIA likiwa bolded
   
 14. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,162
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  tunavuna tulichopanda!
  M4C
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Hivi ndivyo Kikwete anavyoshika kichwa. CCM wanapumulia Mashine ICU
   
 16. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huu mchaka-mchaka kuna wakuuzima jaman....! Hongereni kwa kufanya maamuz ya busara, waachen wafu.........
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kumbe M4C ni Tsunami. Sasa najua kwamba CCM imo matatani.
   
 18. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  teh teh, sure mkuu!
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani hamna safari nyingine, Kupanga ni kuchagua, kushika kichwa au kupaa.
   
 20. D

  Deofm JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo ni jinsi serikali ilivyoshukughulikia taarifa za kamati mbalimbali katika bunge lililopita, lakini hatua mwafaka zikichukuliwa imani ya watu kwa chama tawala inaweza kurejea tena. vinginevyo hata viongozi wa ngazi za wilaya na mikoa wanaweza wakaanza kuondoka. Hii ni hatari sana kwa usalama wa taifa kwani ni sawa na tatizo linapotokea kwenye meli halafu nahodha na mabaharia wote wanajitosa baharini wanawaacha abiria peke yao.:crying:
   
Loading...