Gharama za urafiki.

Gharama za urafiki.

msnajo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
3,066
Reaction score
1,143
Wakuu salaam.

Kama heading itakuwa tofauti na mada hapa chini, naomba mniwie radhi.

Kwa kifupi sana, miaka ya 2000 mwanzoni kuna jamaa mmoja alikuwa rafiki yangu na enzi hizo ndo tulikua tanamaliza kidato cha nne.
Kwa bahati mbaya mwenzangu alipata matokeo ambayo sio mazuri. Ila mimi niliendelea na kidato cha tano. baada ya miaka miwili ya A'level, rafiki yangu aliebaki kijijni alinijia na kunieleza shida yake, na kwa uelewa wangu wa kipindi hicho niliamua kumsaidia.

Naweka wazi kwenu wadau mnipe ushauri. Shida yenyewe ni kwamba alikuwa akihitaji cheti cha kidato cha nne kwa ajili ya kwenda kusomea kozi ya fulani, ambayo ilimchukuwa miezi sita kukamilisha. Baada ya hapo Mungu saidia alipata kazi Mkoani na kwa masharti ya kazi likizo hazipatikani kirahisi kwa waajiriwa wapya.
Nashukuru nilikichukua cheti changu mapema.
Sasa basi, baada ya jamaa yangu kaondoka 2002 kwenda kazini hatukuwasiliana tena kwa namna yeyote hadi leo. Taarifa zake nilizipata kwa watu kwa kipindi hicho chote. Kwa kuwa aliniacha bado mchakato wa kazi haujakaa vizuri, nilisota mtaani kidogo, na huenda ndo ilikuwa sababu ya yeye kupotea mbele ya uso wangu. Mungu mkubwa nilipata nafasi ya kuendelea kusoma na baadae nikapata kazi mjini katika mkoa wangu wa kuzaliwa. Kutoka mjini nilipo hadi kijijini tulipotokea ni takribani km 45. Na huezi kuelekea kijijin ukitokea mikoani bila kupita mjini nilipo. Jamaa yangu baada ya miaka kama miwli alipewa likizo, na alikuja kijijni na taarifa zangu alizipata kupitia kwa watu kama mimi ninavyopata taarifa zake kupitia kwa waengine. Akijua wazi kuwa nipo mjini na kwake aliekuja haikuwa vibaya kujuliana hali, alinipotezea na baada ya mwezi mmoja wa likizo zake alirudi kazini.

Maika ilipita, siku zikasogea, umri nao ukakamata kasi. Jamaa yangu alikuja kijijni akafunga harusi na baada ya likizo yake akarudi kazini. Kwa kila mwaka toka 2005 hadi mwaka jana amekuwa na likizo ambazo zilimruhusu yeye kufika kijijini kuwaona ndugu zake, ila mimi sikuwa miongoni mwa ndugu zake wala jamaa zake.

Juzi jumatatu tar 25-March, nilipigiwa simu na mdogo wangu akidai kuwa yule jamaa anatafuta namba yangu ya simu, je ampe?? Bila hiana, nilimwambia ampe namba labda amekumbuka alikotoka. Baada ya Mdogo wangu kumtumia namba ya simu, jamaa alinitext ujumbe unaosomeka hivi "vp mkuu mbona umepotea sana, nilikuwa na shida na kile cheti kuna maswala nataka nirekebishe". Kwa kuwa mdogo wangu alimpa namba, nilisoma ujumbe na kuu-delete instantly.
Baada ya muda mchache akapiga sikupokea na hadi leo ninavyoandika huu ujumbe sijapokea simu yake na sidhani kama nitapokea. Madai yake, kuna ukaguzi ofisini kwao na original certificates zinatakiwa so wanatakiwa wa-submit ili kudhibitisha uhalali wao..

Kwangu mimi rafiki anaekukumbuka wakti ana shida yake binafsi, sio rafiki bali ni mzushi tu na wala hawezi kukusaidia utakapokwama.

Wadau kama nina makosa mtasema.

Nawasilisha.
 
A friend in need is a friend indeed huyo hakufai anakutafuta wakati wa shida tu hiyo inareflect ana roho mbaya kwako aweza hata kukupotezea cheti chako makusudi shutka mkaka usije sema ningejua.... when it's too late.
 
Mpotezee, kama alikuwa anakumbuka ulivyomsaidia asingekusahau kiasi hicho, achana nae, kila mtu aendelee na maisha yake, atakuja kuwa na adabu, badilisha na number ya simu kabisa
 
Mkuu mpotezee moja kwa moja maana hapo sidhani kama na wewe utakuwa salama kuruhusu tena cheti chako kitumike
Na urafiki wa aina hiyo mimi ndo maana huwa nauchinjia baharini sitaki mambo ya kutafutana kwenye shida aise
 
usimpe kabisa wala usimjibu..ukurasa wenu alishaufunga mwenyewe
 
Mkuu isije ikawa huyo rafiki yako ni MULUGO naibu waziri wa elimu!! Maana katika Tz ndiye anayeongoza kufoji vyeti.
 
Kwanza kwa sheria za nchi hii wewe na yeye mna kesi ya kujibu mahakamani kwa kuwa mlighushi.

Pili kaa mbali naye kwani kwa kukupotezea amekusaidia; mngekuwa na ukaribu angechukua cheti chako na kusepa nacho forever.

Tatu ukitenda wema usisubiri kulipwa wema. Wapo walotenda mema wakalipwa mabaya zaidi ya hayo ulolipwa wewe. Fikiria angekugeuka akakupa fake na yeye akabaki na original ingekuwa vipi?
 
sikia... mwambie aje umpe...then mkamulie live akajipake mwenyewe.......tena ukiweza kawahi kuripoti polisi kuwa kuna mtu aalikwibwa cheti yako mazee.....coz likifumuka huko...na ww unalo...
 
Duu pole sana.... Sasa mkuu ukikaa kimya ataona una fitna na chuki binafsi... We mchane kwanza yaliyokukera, alafu mwambie akijirekebisha arudi tena kuomba... kama mbwai basi mbwai tuu...
 
Anatukana mamba wakati hajavuka mto, mwambie ,"we nani mbona sikukumbuki jombi!"
 
na mimi natafuta cheti nikasomee ualimu naomba nisaidie.
 
Kwa sasa ni vigumu kutumia cheti cha m2 kusomea, tumekomesha baada ya kuanzisha usajiri wa picha.

bado sana,mi nina ndugu yangu huko we nipe cheti tu mengine ntajua mm.
 
Ndio binadamu wengi walivyo mkuu, hata wengi wetu tuanocoment hapa usimpe nasi hatuna tofauti sana, sema ukiangalia picha na avatar ni za kuvutia na huwezi jua.

One thing, wewe una utu, Nakushauri uangalie risk kubwa iloko hapo, kama ni kubwa sana uamue mwenyewe, ila kutokuwa na shukrani ni janga la kitaifa ndugu yangu.

Yamenikuta mengi mabaya sana kwa kuamini na kusaidia wengine ila pia nimepata mengi sana ya faida ambayo sikuyatarajia, lakini kama hakuna risk kubwa, help him learn his mistakes though he seems verry arrogant.
 
bado sana,mi nina ndugu yangu huko we nipe cheti tu mengine ntajua mm.

Wacha longolongo; vyeti vyote kuanzia 2009 vina picha za wahusika na si picha za kubandika; sasa utatumiaje sura ya m2 mwingine hata kama huko kuna ndg yako?
 
Alijua amemaliza, block namba yake hata akikupigia asikupate wala sms zisiingie, shwaini huyo, alianza sasa wewe maliza
 
Wacha longolongo; vyeti vyote kuanzia 2009 vina picha za wahusika na si picha za kubandika; sasa utatumiaje sura ya m2 mwingine hata kama huko kuna ndg yako?

akili kumkichwa we hata ikiwa na picha ya queen Elizabeth haina shida, TZ kajamba nani ndo wanafuatiliwa,wale wa juu ni vimemo ndo vinaongea(hawaongei na mfuga mbwa bali mwenye mbwa)
 
Kuna jamaa hivo hivo alitoa cheti kwa mtu cha form four, huyo mtu akafanyia issue zake akarudisha.Sasa si kazini wakataka original baada ya miaka saba na jamaa alikuwa keshafika level ya management. Alichokifanya alenda kwa mganga akamuua rafiki yake na akawaendea wazazi kuwaomba cheti kwa kuwa sasa mumiliki amekufa na wala wazazi walikuwa hawajui kinachoendelea kama jamaa ndie aliemwendea kwa karumanzila,so kuwa makini ndugu yangu
 
Back
Top Bottom