Kwanza kwa sheria za nchi hii wewe na yeye mna kesi ya kujibu mahakamani kwa kuwa mlighushi.
Pili kaa mbali naye kwani kwa kukupotezea amekusaidia; mngekuwa na ukaribu angechukua cheti chako na kusepa nacho forever.
Tatu ukitenda wema usisubiri kulipwa wema. Wapo walotenda mema wakalipwa mabaya zaidi ya hayo ulolipwa wewe. Fikiria angekugeuka akakupa fake na yeye akabaki na original ingekuwa vipi?
Ndio binadamu wengi walivyo mkuu, hata wengi wetu tuanocoment hapa usimpe nasi hatuna tofauti sana, sema ukiangalia picha na avatar ni za kuvutia na huwezi jua.
One thing, wewe una utu, Nakushauri uangalie risk kubwa iloko hapo, kama ni kubwa sana uamue mwenyewe, ila kutokuwa na shukrani ni janga la kitaifa ndugu yangu.
Yamenikuta mengi mabaya sana kwa kuamini na kusaidia wengine ila pia nimepata mengi sana ya faida ambayo sikuyatarajia, lakini kama hakuna risk kubwa, help him learn his mistakes though he seems verry arrogant.
Kuna jamaa hivo hivo alitoa cheti kwa mtu cha form four, huyo mtu akafanyia issue zake akarudisha.Sasa si kazini wakataka original baada ya miaka saba na jamaa alikuwa keshafika level ya management. Alichokifanya alenda kwa mganga akamuua rafiki yake na akawaendea wazazi kuwaomba cheti kwa kuwa sasa mumiliki amekufa na wala wazazi walikuwa hawajui kinachoendelea kama jamaa ndie aliemwendea kwa karumanzila,so kuwa makini ndugu yangu
Tized nashukuru kwa ushauri wako. Ila lazima iwepo risk. Fikiria huyu bwana anakitaka kwa ajili ya kwenda kujidefend yeye na ajira yake. Uwezekano mkubwa ni kwamba atakapokipata, hatokaa akirudishe na tena itakuwa ugomvi mkubwa. Mi naona ili kuepuka huo ugomvi, ni heri kukaa kimya au nimchane live kwa nini nimemchunia. Hii itampa fundisho zaidi kuliko kukaa kimya.
Btw, nashukuru sana kwa ushauri wako mdau.