Gharama za simu kupanda kuanzia Julai Mosi

Gharama za simu kupanda kuanzia Julai Mosi

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazitoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.

MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.

Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni; "huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia," imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel

MOAT imesema eneo mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala siyo kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine zikiwemo za Afrika Mashariki. "Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na mawasiliano ya simu."

Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40. Aidha, MOAT imeongeza kuwa, "mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine. Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.

"Tunaelewa kuwa serikali inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kusaidia kwenye huduma za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya kwamba sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo wateja watalazimika kuubeba mzigo wa ongezeko hilo," ilihitimisha taarifa hiyo ya MOAT.

http://www.wavuti.com/4/post/2013/0...andisha-gharama-julai-mosi.html#axzz2Wo29J9f1
 
Vipi ule mkonga wa Taifa, tuliambiwa utapunguza gharama za Simu.?
 
Vipi ule mkonga wa Taifa, tuliambiwa utapunguza gharama za Simu.?

Mimi huwa nashangaa sana kwamba huko kushuka kwa gharama, na hiyo kasi kubwa iko wapi? Wengine wakasema ooh mkonga ukija wataweka huduma a wireless sehemu mbalimbali za miji ambapo tungeweza kupata net ya wireless.....mpaka sasa sielewi kabisa mpango wao. ANAYEJUA ATUJUZE
 
Vipi ule mkonga wa Taifa, tuliambiwa utapunguza gharama za Simu.?

Mi nadhani kunavitu vingine serikali inaroka hata haiijui inaambiwa inakubali tu ndo hilo la mkonga wa taifa. hivi matumizi ya sim ni sawa na uvutaji sigara? sms moja tufanye ni tsh 50 na kampuni x inawateja wanaotumia mtandao wao 3,000,000,na wote watume sms 10 jumla nishilingi 1,500,000,000 na bado kupiga. hadi inafika hatua wanapiga promo ya sms 250! kwanini wakipandishiwa kodi na wao wanapindisha wakati nauhakika wanatengeneza super profit? kwanini serikali inakubali hili? watu wengi tu wana simu hawavuti fegi? gharama zetu za sim ni kubwa sana sana. Bora TTCL irudishe kizakendo zaidi,hatuwezi kuendeshwa na wageni ka mazuzu.
 
Mimi huwa nashangaa sana kwamba huko kushuka kwa gharama, na hiyo kasi kubwa iko wapi? Wengine wakasema ooh mkonga ukija wataweka huduma a wireless sehemu mbalimbali za miji ambapo tungeweza kupata net ya wireless.....mpaka sasa sielewi kabisa mpango wao. ANAYEJUA ATUJUZE

mkuu tunaendeshwa kipropaganda zaidi.
watu wanatengeneza 10% tu. hivyo usishangae kusikia huo mkonga haufanyi kazi.!!!
 
Iyo mitandao haipaswi kuongeza gharama wanapata sana faida wakati mwingine wanakata pexa ata pasipo sababu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
mkuu tunaendeshwa kipropaganda zaidi.
watu wanatengeneza 10% tu. hivyo usishangae kusikia huo mkonga haufanyi kazi.!!!

Mambo mengine yanatia hasira sana katika nchii hii
 
Sisi waletimiajo wa internet ndio tutakaobebeshwa mzigo mkubwa. Kama mjuavyo, kuna watu wapo zama za analogy, wanaoona ya kwamba internet ni anasa. Nitanunua bundle refu mwisho wa mwezi, ila litakopoisha...........
 
Kwa usalama wa afya yangu siruhusiwi kusoma wala kucomment thread kama hii.
 
Mimi nashindwa kuelewa kabisa.

Katika ripoti za hivi karibuni katika nchi za Afrika Mashariki kama sikosei Tanzania ndio iliyokusanya kodi ndogo kwenye mitandao ya simu. Ukiuliza kodi zinazotozwa ni almost sawa na nchi nyingine za Afrika Mashariki vipi katika makusanyo ya kodi tuko wa mwisho????

Leo hii wameongeza kodi kupita nchi nyingine za jirani lakini bado utakuja kusikia Tanzania wamekusanya kodi kidogo licha ya kutoza kodi kubwa ukilinganisha na nchi za jirani.

Mwananchi wa kawaida unaumizwa na malengo ya kuendeleza Taifa kutokana na kodi hizo hayapo sijui tunakwenda wapi???

Kotekote ni maumivu. Nakumbuka ile signature ya mwana JF mmoja alivyoandika "Waswahili tumerogwa na aliyeturoga ameshafariki" naikumbuka sana hii kauli na sasa ndio naona ni wakati wake...

😡😡
 
Back
Top Bottom