Gharama za matibabu ya homa inayosumbua inakatisha tamaa, wanyonge hatutoboi

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Habari kuhusu gharama za matibabu kwenye mahospitali makubwa nchini kwa watu wanaodhaniwa kuwa na Nimonia kali ni kubwa sana, serikali inapaswa kumulika hospitali hizi kuona kama hizi gharama ni halisi au zinapandishwa na wamiliki.

Lakini pia ni muhimu kupata gharama elekezi kwa watu wanaopata changamoto ya upumuaji kuepusha kila hospital kujiwekea gharama zake.

Mfano unaambiwa mgonjwa kwa lisaa limoja oxygen na kuyeyusha damu isigande ni shs 100,000/=

Ni Mtanzania gani ataweza hizi gharama? Tuyajadili haya wazi tupate unafuu kuliko kukaa kimya.
 
Wazungu waliposema hiyo Nimonia Ikifika Africa watu watakufa na wengine kuokotwa barabarani walimaanisha matibabu ya gojwa hilo ni expensive na waafrica tupo hoehae...Chukua taadhali Kinga ni bora kuliko tiba. Regards...
 
Alafu kuna sindano iyo nasikia ni milioni 5 alafu hawa jamaa wa bima they don't cover.
 
Ndo mana unaambiwa chukua tahadhari!

Wa Tz wa ajabu, utakuta mtu kawekewa maji tiririka, sabuni bure kabisa lakini kunawa hataki maji anayakwepa mpaka awekewe na askari wa kumlazimisha kunawa. Huyo ndo MTz! Halafu kwa ulalamishi hajambo!
 
Mungu wetu atatutetea peke yetu hatuwezi maana wanakuga wenye mabilioni yao bank Nasema hivi jilinde na kumuomba Mungu.
 
Wataalamu walishasema tengezeni juice ya Malimao, Vitunguu saumu, Vitunguu Maji, Tangawizi na pilipili kichaa Kunywa mara tatu kwa siku, ila hamsikii.
 
Ndo mana unaambiwa chukua tahadhari!
Wa Tz wa ajabu,utakuta mtu kawekewa maji tiririka,sabuni bure kabisa lakini kunawa hataki maji anayakwepa mpaka awekewe na askari wa kumlazimisha kunawa! Huyo ndo MTz! Halafu kwa ulalamishi hajambo!
Watz waajabu sana, tii mashariti ya wataalamu bila shuruti
 
Nenda hospital ya serikali ukatibiwe kwa pesa unayotaka maana huko ndo hela yako ya kodi inapokwenda, alafu iyo serikali unayo omba ikusaidie imesema huo ugonjwa ambao mmeupachika jina la NIMONIA HAUPO.
 
Alafu kuna sindano iyo nasikia ni milioni 5 alafu hawa jamaa wa bima they don't cover.
... bima haijawahi ku-cover magonjwa ya mlipuko; elewa hilo. Maafa yana kitengo maalumu pale ofisini kwa PM huu ndio ulikuwa wakati wake.
 
Wako sahihi kabisa! Wanakomoa baada ya wananchi kushobokea kuwa Tanzania hakuna Corona.Gharama zinapaswa kuwa TZS 1,000,000/= cash kwa lisaa limoja.
 
Ndo mana unaambiwa chukua tahadhari!

Wa Tz wa ajabu, utakuta mtu kawekewa maji tiririka, sabuni bure kabisa lakini kunawa hataki maji anayakwepa mpaka awekewe na askari wa kumlazimisha kunawa. Huyo ndo MTz! Halafu kwa ulalamishi hajambo!
Serikali inasema takwimu yoyote lazima ithibitishwe na serikali vinginevyo utakamatwa na kufungwa. Serikali inasema hakuna ugonjwa wa Covid19 nchini, sasa mnaposema watu wanawe mikono kwa tahadhari, wanajihadhari ni kitu kisichokuwepo?
 
Back
Top Bottom