Gharama za matibabu MOI juu mara tatu zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za matibabu MOI juu mara tatu zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, May 25, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  KATIKA hali inayoashiria mwendelezo wa mfumuko wa bei nchini, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi), imepandisha gharama za huduma zake kati ya asilimia 80 na 300. Ongezeko hilo la gharama za matibabu limekuja katika kipindi ambacho tayari, kumekuwa na ongezeko kubwa la gharama za maisha katika bidhaa muhimu za chakula yakiwemo mazao ya nafaka.

  Kutokana na ongezeko hilo, wapo wagonjwa walioshindwa kupata huduma ya matibabu kwasababu hawakuwa na fedha zinazotosheleza kupata huduma walizokuwa wakizihitaji. Jana, Ofisa Uhusiano msaidizi wa Moi Frank Matua alithibitisha kupanda kwa gharama hizo na kwamba jambo hilo ni utekelezaji wa sera za huduma za afya katika hosipitali hiyo. "Kweli gharama zimepanda, lakini, mchanganuo halisi bado haujapangwa," alisema Matua alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake jana.

  Matua alisema kwa sasa taarifa bado hazijawa rasmi na unahitajika muda zaidi wa kuandaa takwimu za kuonyesha mchanganuo halisi wa gharama hizo zitakavyotozwa. Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa ongezeko hilo linahusisha huduma zote zinazotolewa na taasisi hiyo.

  Miongoni mwa huduma hizo ni kumwona daktari ambazo zimeongezeka kutoka Sh2,000 za awali hadi Sh8,000, huduma ya X - ray kutoka Sh5,000 hadi Sh9,000 wakati gharama za matibabu zimepanda kwa viwango tofauti kwa kuzingatia aina ya ugonjwa.

  Kabla ya kupanda kwa gharama hizo za matibabu, uongozi wa Moi ulitoa tangazo ambalo limebandikwa kwenye ukuta ofisini kwa muhasibu likieleza kupanda kwa gharama hizo, lakini bila kuonyesha viwango vya ongezeko hilo. "Kuanzia Mei 21 mwaka huu gharama za matibabu zitapanda," inasomeka sehemu ya tangazao hilo lililopo kwenye ofisi ya mhasibu.

  Kauli za wagonjwa

  Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri matibabu ambaye alijitambulisha kwa jina la Abdallah Selemani, alisema ongezeko la gharama za tiba ni kikwazo kwa wagonjwa, kwani wengi wao hawana uwezo wa kumudu gharama hizo. "Wapo waliorudi nyumbani kwasababu ya ongezeko hilo ukizingatia kwamba imekua ghafla,"alisema Selemani.

  Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Debora Ramadhani ambaye pia alikuwa akisubiri matibabu, alisema licha ya ongezeko la gharama za matibabu pia dawa wanazoandikiwa bei zake zimeongezeka na kwamba watu wa kawaida hawawezi kuzimudu. "Baada ya kuandikiwa dawa na daktari unaambiwa ununue katika maduka yaliyopo katika eneo hilo, lakini wanauza dawa bei kubwa,"alisema Debora.

  Mmoja wa wagonjwa aliyongea na gazeti hili kwa njia ya simu, Yusuph Juma, aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya kutibiwa na kushindwa kupata huduma, alisema gharama hizo zimebadilika kwa asilimia 300 na kufanya wagonjwa wengi kushindwa kupata matibabu. Juma alifafanua kuwa awali wagonjwa waliokuwa wakitumia kadi za Bima ya Afya walikuwa wakilipa Sh21,000 kumuona daktari, lakini hivi sasa gharama hizo zimepanda kwa Sh 30,000.

  "Na bei hiyo niya majira ya asubuhi, kuanzia mchana malipo ni Sh40,000 hiyo ni bei halali kabisa na stakabadhi zinatolewa kwa wagonjwa waliofanya malipo,"alisema Juma. Aliendelea kusema kwa watu wanaolipa fedha tasilimu kumuona daktari ni Sh8,000 badala ya Sh 2000 ambayo ilikuwa ikitumika zamani.

  Akizungumzia huduma za mazoezi ya viungo alisema kuwa na huko pia gharama zimepanda kutoka Sh10,000 hadi sh 15,000. Alisema kuwa mabadiliko ya gharama hizo za matibabu yalikuwa yakiwagusa sana wagonjwa wanaotibiuwa kwa kutumia fedha tasilimu tofauti na wale wanaotumia kadi za bima.

  "Unajua wanaotibiwa kwa kadi wala huwa hawafanyi uchunguzi wa gharama wanazotumia tofauti na mgonjwa anayetoa fedha taslimu,"alisema na kuongeza: "Wiki moja waliyotumia katika kutoa matangazo ya gharama mpya za matibabu haikuwa inatosha kwani imeleta usumbufu kwa wagonjwa wanaotoka mikoani ukizingati sasa hivi kuna hali ngumu ya maisha".


  Gharama za matibabu MOI juu mara tatu zaidi
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  bora maisha kwa kila mtanzania
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  daladala zinapanda lini?
   
 4. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huduma za reli ya kati nazo nasikia zishapanda
   
 5. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bia nazo zimepanda sana,
  ila tunajitahidi ivo ivo wala hatulalamiki.
  Bia ya kwanza na ya pili ndo inakuwaga ghali zinazofuata nadhani kunakuwa na kadiscounti flani bcoz mtu unajisikia tu kuzungusha raundi
   
 6. l

  lemma New Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  daaaaaaa kweliiiii lkn tatzo si madokta tatzo tukale wapi kama fungu halifiki hapo hospitali
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii ni balaa
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Wacha inyeshe tuone panapovuja.
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​kweli tundu limetoboka
   
 10. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani suluhisho ni kuifanya NHIF kuwa active ili huduma za afya ziwe bure kwa kila mwananchi. Lakini sema ukiritimba na rushwa ilivyojaa Tanzania watu wanauharibu mguko wa NHIF na kuonekena mbaya. Mfano angalia Canada, wana mfuko wa aina hiyo na unafanya kazi vizuri sana.
   
 11. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa Basili Pesambili Mramba ndiye chief Economist wa NHIF
   
 12. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Sukari na mchele nao umepanda sijui tukaishi wapi?
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  NDUGU usindanganywe kabisa hii NHIF ndio shirika la bima lililo duni zaid kuliko jinine lolote lile licha ya kwamba wana wanachama wengi zaid kuliko yote. Kwanza kabisa pale moi ukiend ana ile brown card utambulia kupewa file umuone dr na kufanya x-ray ukilazwa au hata dawa lazima uende ukaunue tu. kasheshe ni kwenye operation kuna vipoint vyao huwa wanaviandika mar point 250 mara 300 hizi na zenyewe zinagharama sana. kwakua bima hii haitosh basi huwa unatakiwa u top up mwenyewe. ni vyema sasa mifuko ya bima ikawa imara zaid ili kuwahuduma wananchi.
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
   
 15. A

  AZIMIO Senior Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Viongozi wenyewe sjui kama wanaona na hii ndio point kubwa ambayo wapinzani wanataitumia na wananchi kuwaelewa kwa sababu wanafeel na wanaiona,sjui wazir wa afya atasemaje bunge lijalo.
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CCM hoyeeeeeee!!
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  PAwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!
   
 18. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  "Ukibebeshwa mzigo mzito kuliko uwezo,kama haulalamiki mbebeshaji ataujua ndo uwezo wako wakubeba"kama watanzania tutakaa kimya watawala wajua tuna uwezo wa kulipia huduma zinazopanda kila kuchao
   
 19. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Binafsi nadhani MOI wamefanya hivyo kwa nia njema,
  nayo ni ili waweza kufikia viwango vya kuwatibu waheshimiwa wanaokimbilia kutibiwa kwa gharama kubwa nje ya nchi.

  Big Up MOI!,
  Ila angalizo; muweke na ka-kitengo ka-kututibu sisi tusiokuwa na POCHI (POSHO)
  na tualipa KODI (mishahara yenu) Wao (Waheshimiwa) wana misamaa ya KODI.

  japo kwa Oparasheni za kichwa badala ya miguu,
  lakini kulazwa tu kutatupa MATUMAINI kuwa tunapata HUDUMA na tutapona.
   
Loading...