Gharama za matibabu anajilipia mwenyewe?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,109
Posted Date::10/27/2007
Gavana BoT bado amelazwa hospitalini Marekani
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

UONGOZI wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) umesema Gavana wa benki hiyo, Daud Balali, amelazwa hospitali ambako anapata matibabu ya jeraha la upasuaji.

Balali yuko nchini Marekani ambako alikwenda miezi mitatu iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya.

Awali uongozi wa BoT ulithibitisha Balali kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi, lakini ikisema ulikuwa ni uchunguzi wa kawaida.

Kauli hiyo mpya ni ya kwanza kutolewa na BoT kwa kuthibitisha kuhusu Balali kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili i ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni , Naibu Gavana wa BoT, Juma Reli, alisema siku zote Balali alikuwa akipata matibabu akiwa nyumbani.

Kwa mujibu wa Reli, Balali ingawa amelazwa hospitali bado afya yake inaendelea vizuri.

"Sasa hivi amelazwa hospitali, amefanyiwa upasuaji lengo ni kuona nini kinachomsumbua, " alisema Reli na kuongeza:

"Lakini nanichoweza kusema ni kwamba, anaendelea vizuri na matibabu na afya yake pia".

Alipoulizwa ni matibabu hayo ni ya muda gani na lini hasa Balali atatoka hospitali na kurejea nchini, alijibu "maradhi huwezikusema mtu atatoka lini, lakini cha msingi anaendelea vizuri," alisisitiza Reli.

Reli aliongeza kwamba, kuweza kujua lini atatoka ni hadi atakapomaliza matibabu na madaktari kutoa idhini na pia akasema ni mapema kutaja hospitali ambako amelazwa.

Kuhusu taarifa kwamba, Balali anaumwa kisukari na magonjwa mengine ya ndani ya tumbo , alisema, "hapana, hilo halijathibitishwa uchunguzi bado."

Siku za hivi karibuni kumekuwa na utata kuhusu afya ya Balali, tangu alivyoondoka nchini kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya.
 
he is still alive akila gud tym us nasi twadanganywa yuko hospitalini..ushahidi?
 
Anapumzika na kufaidi pesa zetu walizotuibia. Huyu jamaa na wenzake inatakiwa wawe wanakula sembe Keko
 
Lakini kama walivyosema hapa kama ana uraia wa USA matibabu yake yanalipiwa na walipa kodi wa USA.
 
Ninadhani kuna kitu kinaendelea ndani ya BoT. Maana hili siyo swala la kawaida. Wanakaa kimya kwa muda halafu wanaibuka tena just kutukumbusha kwamba Gavana bado yupo ofisini. Au atapona pindi report ya uchunguzi wa fedha zilizotafunwa itakapokamilika na kutamka wazi kwamba hakukuwa na ubadhirifu. Hiki ni kiini macho kwa kweli ... mazingaombwe kwa kwenda mbele!

Sijui nimwamini Mwafrika wa Kike kwamba Ballali ndo kakimbia nchi au wamemuweka mafichoni ili asiingilie uchunguzi?
 
Lakini kama walivyosema hapa kama ana uraia wa USA matibabu yake yanalipiwa na walipa kodi wa USA.

USA matibabu sio bure hata kwa wenye nchi, sio kama hapa UK. Anatumia pesa za Watanzania kujipumzisha. Kama anajilipia mwenyewe bila insurance miezi mitatu kwa USA ni pesa nyingi mno!
 
USA matibabu sio bure hata kwa wenye nchi, sio kama hapa UK. Anatumia pesa za Watanzania kujipumzisha. Kama anajilipia mwenyewe bila insurance miezi mitatu kwa USA ni pesa nyingi mno!

Kwanini ajilipie mwenyewe wakati bado ni Gavana wa BoT? Kwa kifupi ni kwamba hata kama hana Health Insurance inayom-cover hata akiwa nje ya nchi, basi hizo gharama zote za matibabu zinalipwa kutoka kwenye kihenge cha walipa kodi. On top of that, pia inategemeana na Policy ya Bima ya Afya aliyo nayo, policy nyingi huwa zina limit ya malipo na nyingine mna-share gharama up to a certain limit. May be kwa kuwa yeye ni kibosile na huwa hawaendi kwenye hosp uchwara za bei poa inawezekana dau analolipiwa na BoT likawa kubwa sana kiasi kwamba anaweza kujichagulia mwenyewe atibiwe hosp gani. Lakini lazima BoT inalipa hela nyingi sana kwa ajili ya matibabu yake. Miezi mitatu si mchezo na hasa kama mtu anakuwa hospitalized!

Kwa hiyo kihenge kinaendelea kubunguliwa na dumuzi. Swali langu bado liko pale pale, BoT haitaki kusema kalazwa hospitali gani, kwani yeye ni nani mbona Nyerere tuliambiwa kalazwa wapi, BWM alipoenda Uswiss tuliambiwa kalazwa hosp gani? Huo usiri wa BoT unatokana na nini? Au ndo kama Mtanzania anavyosema kwamba anajipumzisha kwa kutumia hela ya walipa kodi wa Bongo? Nina uhakika hata kama ni mgonjwa akiwa nje ya hosp anaishi hotelini na yule jamaa anavyojua kuishi maisha ghali bill yake kwa siku anajua mwenyewe!
 
USA matibabu sio bure hata kwa wenye nchi, sio kama hapa UK. Anatumia pesa za Watanzania kujipumzisha. Kama anajilipia mwenyewe bila insurance miezi mitatu kwa USA ni pesa nyingi mno!

Hivi unafahamu experts wengi hasa Africa huwa wana mikataba ya kulipiwa Health Insurance? Chunguza BUPA na makampuni mengine ya hiyo sector utaniambia.

Hata hapa UK ni mburu kenge tu ambao hawana health insurance wanategemea ya dezo kutoka NHS kwa foleni.
 
Back
Top Bottom