Gharama za kusoma Canada zipoje?

Mkuu sasa kusomea Plumber Welder etc lazima usomee bongo kabla ya kuomba kazi Canada au unaweza kuomba kusoma Canada
Alberta ni province nzuri kuanzia maisha wana privilege nyingi toka serikalini. Unafuu wa kodi....
Ukisoma huko Bongo itanachukua process nying kuweza kufanya kazi Canada vizuri ni kusomea Canada tu
 
Nashukuru sana Mimi sio mwanafunzi nilikuwa nataka kujua tu na kusaidia watu. Mimi nipo Texas 20 years sasa! next summer nataka nije tena Toronto nilikuja 2014 kutembea. Ningependa kuonana na Watanzania wenzangu huko tuongea mambo ya maendeleo na jinsi ya kusaidiana hasa kwa vijana wetu
 
Mkuu shukurani kwa ufafanuzi ila ningependa utusaidia maelezo kidogo kwa mtu anayetaka kuja uko kusomea hizo fani
 
Baada ya Ulinzi na Usalama kinachofata ni Afya na Elimu bila kuwa na elimu bora na huduma bora za afya ndani ya Taifa ,lazima taifa lako litakua ni taifa la wapumbavu na wagonjwa
mkuu vipi kwa course ya dental lab technology kwa Canada haiko more considered Sana?? Nieleweshe mkuu
 
mkuu vipi kwa course ya dental lab technology kwa Canada haiko more considered Sana?? Nieleweshe mkuu
Sijajua unachotaka kujua juu ya course hii lakini ni moja ya course nzuri na yenye kipato kizuri yani kuanzia $ 49,412 kwa mwaka au $ 25 kwa saa huku kwa anaeingia kazini huanza na $ 35,000 wakati wafanyakazi wenye ujuzi au uzoefu wengi hupata $ 69,000.kwa mwaka Meno na Wanyama ni big deal sana yani Dental Technologist na veterinarian
 
Mmmh are you sure? mbona MUNF sio bei kubwa mkuu? kua visa ya canada inaizidi Australia? anyway huo ni ufahamu wako
 
Na je, kwa anayehitaji Kwenda kufanya Masters hasa za ICT/Computer Science fursa zipo? Na scholarship je?
Kwa Australia utapeta zaidi aisee, tafuta student visa kwa internationa student unatakiwa kuwa na dollar 18,100 kwenye acc yako na ada ya semester moja (around aud4500) na health insurance ya mwaka mmoja, gharama ya visa ni kama aud610. So roughly ukiwa na Tsh 40,000,000 unaweza fanikiwa kusoma masters yako ya IT na ni demand course unapewa mwaka mmoja kuishi na kutafuta kazi kwa kutumia bridging visa...IT lazima ufanikiwe aiseeee mark my words
 

Mkuu kwa course ya Veeriary laboratory technology je, kwa mtu mwenye diploma kuja huko kusoma inakuaje na kupiga deal la ambalo sio professional je?
 
Inawezekana kweli ni ngumu kupata kazi ya professional maana Dr slaa na PhD yake alikuwa anauza supermaket
 
samahani sana mkuu kwa kipindi hiki kwa canada kwa njia raisi ya kufika huko utumie njia gani
 
Dah bro umefafanua vizur sana aise sasa kwa mimi apa na elimu yangu ya form four esabu nilizungusha zero, inakuwaje? Naweza ku apply?
 
Mkuu upo vzuri nitakutafuta pm
 
Vijana changamkeni ukiweza kusoma vizuri Software kama SAP na Oracle unaweza kupata kazi hata ukiwa Tanzania na ukalipwa kuanzia $55,000-$80,000 au hata zaidi kama una uzoefu. Hizi ndiyo pesa wanalipwa wahindi waliopo India. Na masomo unaweza kupata kwa search kwenye google na YouTube ni kujituma tu.

unatakiwa kuwa na internet nzuri na siku hizi naona kuna improvement
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…