Gharama za kusafirisha mzigo kwa ndege toka Dar es Salaam hadi Oman

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,807
6,303
Kuna fulsa nimeiona Oman, ya Chakula, Mbogamboga na Matunda, nafikilia kuanza kupeleka bidhaa tajwa hapo juu kila week, kwa kuanzia ntakua nasafirisha Tani 1 kila week.

Kama unafanya kazi kwenye Kampuni za Ndege hasa zinazoruka direct toka Dar es salaam to Muscat, au unafanya biashara Kama hii hata iwe ni kwa other Gulf countries, uzoefu wowote, ntashukuru ukitoa uzoefu wako.

*Napenda kujua gharama za kusafirisha mzigo.
*Changamoto n.k

Shukrani!
 
Kwann usiende kwenye ofisi za hizo ndege wanazosafirisha mizigo nafikiri huko utapata info zote muhimu na kwa ufasaha zaidi
Kama kwel uko makini na biashara yako fanya hivyo mkuu
Hiyo ipo kwenye ratiba zangu mkuu! But hapa naweza kupata uzoefu zaidi ya kujua gharama!
 
kusafirisha tani moja kwa ndege ni gharama kubwa sana.. hata mengi au tajiri kama bakhressa hawez fanya huo ujinga.. na haiwez kukulipa kamwe..

kwenye international business rules ni hivi.. mzigo wowote mzito wenye kg nyingi.. unapakiwa kwenye meli sababu meli haziangalii uzito wao ni cbm tu..

na mzigo mwepesi wowote ndio unapanda ndege...

maana gharama za ndege kwa 1 kg tu ni usd 10 mpaka usd 30.. sasa piga hesabu tani moja itakuwa kiasi gan??
 
Unawezaje kuuita ujinga mkuu!?? Hujui Kuna watu wanapeleka vyakula na hata nyama ya Mbuzi huko Gulf Countries? Tofautisha gharama ambazo unalipa uko over weight wakati wa kusafiri na Commercial Cargo cost!
 
nafanya kazi kwenye logistics industry... nakuelekeza unapanik...

mimi nimekupa rate ya airfreight cargo.. huwezi pakia mzigo tani 1 ambayo ni kg 1000 kwenye ndege ya abiria... mimi nakueleza wastani wa bei kwa rate za ndege za mizigo

Sitaki hata kujua unafanya wapi! Nachofanya Ni kukusanya Details za kutosha, unawezaje kuita Ujinga kusafirisha Tani 1 ya Cargo kupeleka Gulf Countries? Cha ajabu kipi? Haimaanishi sina nnachojua, nataka kupata information zaidi.

juzi niliunganishwa Na mtu yeye anapeleka Nyama Mbuzi Dubai! Kila wiki Mara 2, means Tani 2 kila wiki, wewe unamwita mtu Kama huyu mjinga?

Acha kashfa...!
 
tatizo lako unapanik tu.. ujinga sio kufanya biashara.. ujinga ni kusafirisha mzigo mzito kwa ndege.. wafanyabiashara wengi wanatumia meli sababu inawalipa.. ukitumia ndege cost zinakuwa juu na hata price yako itabidi iwe juu na hapo kuna ushindani.. lazima u cut cost..

kuna makontena special kwa ajili ya kusafirishia vyakula yapo kama mafriji kabisa... hayo ndio wafanyabiashara wa vitu vya kuharibika wanayatumia...

Lugha yako haikua nzuri Mkuu! Kusema ni Ujinga kusafirisha mzigo kwa Ndege sio Lugha yenye staha, nikakupa mfano wa mtu anayepeleka Mbuzzi Dubai kwa Ndege mmara 2 kwa wiki, kwa njia ambayo unasema ni ujinga! Unaweza kuwa Na hoja but ukiingiza lugha mbaya haileti maana!
 
Hata tungekuwa na nia ya kukusaidia, hatuwezi kufanya hivo maana unaonekana huna unalotaka kujua. Kupanick sio suluhisho na kama unajua sana umeuliza ili iweje
Unadhani Lugha ya Ujinga mdau alotumia Ni sawa!?? Kama angesema kutumia ndege wakati unaweza kusafirisha kwa Meli (Sio sawa) unadhani angepungukiwa Na nini?
 
nafanya kazi kwenye logistics industry... nakuelekeza unapanik...

mimi nimekupa rate ya airfreight cargo.. huwezi pakia mzigo tani 1 ambayo ni kg 1000 kwenye ndege ya abiria... mimi nakueleza wastani wa bei kwa rate za ndege za mizigo
Kuna mtu namfahamu anasafirisha tani kadhaa za madini kupeleka Thailand, mara zote husafirisha kwa kutumia ndege.

Usimkatishe tamaa mwenzio, unaweza ukawa kwenye sekta husika lakini usijue kila kitu.
 
madini yana kilo 1000???? mi nimempa bei halisi ya ndege ilivyo.. aamue yeye.. na je faida ya madini ni sawa na mboga mboga.. sokoni??
Ni hivi mkuu, nimekaa Oman miezi 6 hivi, nimerudi Mara moja, Huko Kuna Mfanyabiashara mmoja Ana Min Super Market akiuza Chakula, Mboga na Matunda Tu! Binafsi pia nilikua mteja wake nikienda kununua mchele, matunda na Mboga mboga, anashusha mzigo kila wiki, lakini mzigo wake unatoka moja ya nchi za East Africa (Sio Tanzania).

Siku nikamuuliza, kwa nini asichukue Mzigo toka Tanzania? Coz tuna utitiri wa matunda, mboga mboga na matunda ambayo yapo kwa wingi kuliko nchi zingine za east Africa, akanambia anatamani siku nyingi, lakini Hana connection Tanzania so akipatikana mtu wa kumwandalia mzigo na pia kukawa na unafuu kuliko kule anapoagiza sasa, yupo tayari kuchukua mzigo Bongo, coz Kuna baadhi ya Vyakula, Matunda, Mbogamboga Wateja wanataka na hapati huko anapochukulia mzigo, ila anajua Tanzania vinapatikana.

So Mimi ntamuandalia mzigo, yeye atalipia Shipping cost kwa ndege, coz ni mwaka wa 2 huu anafanya biashara hii, na sasa anaagiza Tani 1 kila week, that's why nipo katika kutafuta details zaidi, Japo ntaenda kuuliza bei mwenyewe kwenye mashirika ya ndege!

Sasa nnapoongea juu ya kusafirisha Tani 1 ya Chakula, ni matakwa ya mteja, wewe unapokuja na story zako kuwa haina faida wakati Kuna watu wanafanya nashangaa, Wateja wanataka vitu fresh.

Mwenyewe anaagiza mpaka Achali Ile ya kutengeneza kwa mkono, Asali, Vitunguu n.k....Unataka wote wafanye biashara ya Madini?
 
Usikatishwe tamaa, me nafikiri unahitaji tu kufanya research in details kwa kujaribu kuwasiliana na mashirika ya ndege tofauti tofauti ili kuangalia uwezekano pia unaweza kupata ushauri mzuri huko, ila naamini inawezekana...

Vipi mkuu OMAN oppurtunities zimekaaje hasa za ajira kwa wataalamu upande wa engineering nk..??
 
Sure mkuu! Ntafanya hivyo but Kama unavyojua JF imebeba watu wenye uzoefu tofauti, so nikasema ngoja niweke huu Uzi hapa Ili kupata uzoefu zaidi toka kwa wadau!

Kuhusu fulsa kwa fani yako fulsa ni nyingi sana, sio tu kwa Oman but ni kwa nchi zote za Gulf countries, wenzetu sio wafanyaji kazi, wafanyakazi wote hasa sekta binafsi wanatoka nje, kuanzia kazi ambazo hazina professional mpaka kwa watu wenye professional, kuanzia kwa watu ambao hawajui kusoma Na kuandika mpaka kwa wenye High education level! Wapo Engineer wa Kibongo wanafanya mambo makubwa Sana Dubai!

Sometimes huwa nashangaa nikiona Waalimu wakilalamika hapa, wakati Oman Kuna fulsa mpaka ya kufundisha KISWAHILI.
 
kusafirisha tani moja kwa ndege ni gharama kubwa sana.. hata mengi au tajiri kama bakhressa hawez fanya huo ujinga.. na haiwez kukulipa kamwe..

kwenye international business rules ni hivi.. mzigo wowote mzito wenye kg nyingi.. unapakiwa kwenye meli sababu meli haziangalii uzito wao ni cbm tu..

na mzigo mwepesi wowote ndio unapanda ndege...

maana gharama za ndege kwa 1 kg tu ni usd 10 mpaka usd 30.. sasa piga hesabu tani moja itakuwa kiasi gan??
Hata ndege za kusafirisha mizigo pia ni ghali mkuu???
 
Back
Top Bottom