Gharama za kupiga simu kupungua:

Gharama za kupiga simu kupungua:

Zimeshukaaa kweli nimeongea na mtandao mwengine kwa sh 37 kwa sekunde
 
Gharama za muingiliano, interconnection charges zimepungua tangu jana Na upo uthibitisho. Ieleweke kuwa ni gharama za muingiliano, yaani gharama anazotozwa mteja kwa kupiga mtandao mwingine. Hakuna kampuni itakayoweza kutopunguza kwani Mamlaka hufanya ukaguzi na kampuni ikibainika kutoza nje ya maagizo ya Mamlaka, kampuni itapewa adhabu kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa fidia kwa wateja, faini, kupokonywa leseni nk.
 
napata kigugumizi hapa cha kuelewa... Na watu bado wanalalamika ingawa binafsi situmii mtandao wa hapo kwa sasa. Kwa mfano; voda kwanda airtel kwa dakika moja ni Tsh 400 au pungufu kidogo, (vat & other charges inclusive).. Hebu nieleweshe hapa kinachopungua ni ni kiasi hiki kutoka 400 had sh 34 kwa dakika, au ni ile charge iliyo ndani ya hiyo 400?.
Angalizo... Kwa nini hizi charges haziko wazi, yaani haijulikani ni % ngapi hutozwa?. Asante.
 
Zingatia tunazungumzia termination rate, kama uko Airtel, kuna gharama za ndani ya mtandao na unalo toka ndani ya mtandao, simu yako inapotua, ndio zitakuwa gharama za muingiliano. Aidha gharama hizi hulipwa Na kampuni husika baada ya mteja wake kupiga simu. Zamani gharama ilikuwa cent 25 ya dola Na zimeendelea kushika hadi kufikia sh 112 Kwa dakika. Shilingi 400 umepata wapi Na kivipi?

Mteja akipiga simu ndani ya mtandao, inategemea gharama zikoje Na vile vile mara nyingi makampuni ya simu yamekuwa yakitoza au kutoa offer hata sh. 1 Kwa sekunde. Vilevile ni vizuri kufahamu kuwa bei inayotajwa haihusishi VAT Na Excise duty, hivyo Kwa mfano dk moja Kwa sekunde inakuwa shs 60 + 18% VAT + 12 Excise duty.

Kwa hiyo, Kwa sasa mtu analipa termination rate 34.92 (kutoka 112 ya zamani). Ukisoma haijapungua, si kweli. Ni vizuri kufanya uchunguzi Na kubaini ukweli halisi. Mamlaka ya Mawasiliano haiwezi kufanya kazi zake Kwa hisia. Upo utaratibu Wa kuhakikisha maagizo yake yanayekelezwa Na ikiwa vinginevyo, sheria iko wazi.
 
Back
Top Bottom