Gharama za kujifungua kulikoni?

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,267
2,000
Nianze na salamu kwenu wana JF

Nikiwa kama mwanaume ambae nimeoa na kubarikiwa watoto wa 2 niseme tu naheshimu hali ya ujauzito kwa mwanamke kwan mateso ya uchungu nimeyaona

Na pia nawapongeza madaktari kwa kazi kubwa wanazofanya kutusaidia kulete viumbe hivi duniani vikiwa salama kwa uangalizi wao wa karibu

Kero kubwa ambayo kama taifa inabidi tuifanyie ufumbuzi ni hizi gharama za kujifungua kwa upasuaji na kawaida baadhi ya hospital ambacho kiwango ni laki moja mpaka laki mbili na nusu

Tuone namna ya kuliweka liwe bure kwani nimeona wamama wengi wakilalamika

Nikiwa kama mtumishi wa umma na bima ya afya pamoja na familia yangu ningeomba kiasi fulan cha pesa ninachokatwa kipelekwe kwenye account binafsi ili wamama hawa waweza kuhudumia bure.

Pia kwa wale wanaharakati wa wanawake pazeni sauti ili uzazi iwe bure na sio kikwazo kwa wanawake ,kwan sio wote wanaweza lipia hizo gharama kwani mimba inapatikana popote na wengine hutelekezwa na wenza wao hivyo kutomudu gharama na pengine wengine huona bora kutoa mimba .

Naiomba serikali yangu iliangalie hili.na pia naomba kuwe hata na kampeni ya kuchangia uzazi ili hawa wanawake ambao ni mama zetu, wake zetu, Dada zetu wahudumiwe bure

Okoa maisha ya mama mzazi ,ajifungua salama na awe na uzazi wenye furaha kwa kutoa maoni yako yanayojenga ....nini kifanyike?
 
Peppapig

JF-Expert Member
Oct 29, 2020
731
1,000
Kufanya iwe bure kabisa ni changamoto as serikali bado inahitaji ela kulipa wauguzi,manunuzi ya vifaa na mengineo
Kinachotakiwa ni kupunguza costs especially za kujifungua kwa operesheni!inatakiwa nusu achangie mgonjwa nusu serikali ichangie!
Pamoja na yote ukienda Muhimbili kuna exemption policy ambayo iko active toka enzi za jk,kwa yule aliejifungua alafu ikaonekana hana uwezo kabisa wa kulipia huyu anapewa msamaha wa deni lote!
Kuna yule ambae anaonekana ndugu wanaweza kumchangia kiasi fulani,basi maafisa ustawi uhamasisha ndugu wachange wanachoweza then kilichobaki anapewa msamaha
Sijajua kwa hospitali zingine kama ni hivi au lah!
 
Kweli ni changamoto lakin naimani ni suala dogo sanaa ambalo linahitaj ufumbuzi na kuliwekea kipaumbele

Mfano tukiweka sh.30 kwa kila vocha unayonunua au kila mafuta unayonunua au kwa kila ushuru tunaolipa ,lazima tutafanikiwa
 
Peppapig

JF-Expert Member
Oct 29, 2020
731
1,000
Kweli ni changamoto lakin naimani ni suala dogo sanaa ambalo linahitaj ufumbuzi na kuliwekea kipaumbele

Mfano tukiweka sh.30 kwa kila vocha unayonunua au kila mafuta unayonunua au kwa kila ushuru tunaolipa ,lazima tutafanikiwa
Sio rahisi na ukumbuke hii ni developing country not developed
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,128
2,000
Serikali ihakikishe vifaa vya kujifungulia vipo vya kutosha kila hospitali na vituo vya afya, siyo mama mjamzito anaambiwa apeleke gloves, unakuwa ni undezi.
 
quier

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
399
1,000
hospital zenyewe zinatosha nchi nzima Mana Kuna sehemu nyingi hata vituo vya afya hakuna.
Mi nadhani hii ya kujifungua gharama ziendekee kuwepo Mana Mungu ametupa miezi 9 yote hiyo unajua Kuna siku lazima nishushe mzigo so ni lazima kujiandaa lakini mtu mpaka siku anaingia leba hata 10 hana anategemea msaada.
Tunazalisha taifa la ajabu uzae bure, mtoto atibiwe na kusoma bure wewe mzazi utakua na kazi gani sasa?
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
192,176
2,000
Elimu iliwekwa bure kinachotokea masikitiko magumu. Bora hizo gharama kuliko iwekwe bure mpate huduma gharama mara tatu ya hizi zilizopo wakati huu
 
Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,430
2,000
Kweli ni changamoto lakin naimani ni suala dogo sanaa ambalo linahitaj ufumbuzi na kuliwekea kipaumbele

Mfano tukiweka sh.30 kwa kila vocha unayonunua au kila mafuta unayonunua au kwa kila ushuru tunaolipa ,lazima tutafanikiwa

Mzee TZ ni donor country..kama tunapata billions za kununua wapinzani, tutashindwaje kuhudumia watu wetu..akina mama wajawazito inclusive?

Pesa ipo ni swala la utashi na vipaumbele vya wanasiasa!

Masanja,
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,128
2,000
Wazo zuri, lakini pia bure ni gharama....
Kinachoendele kwenye elimu bure hata kwa muujiza hatutoboi.
Nafikiri kwenye elimu ada zirejeshwe hata kama ni ndogo, kuweza ku-sustain zile gharama za uendeshaji wa shule. Tusiwafanye wananchi wetu ni mafukara kiasi kwamba hawawezi kugharamia kitu chochote, tuweke mazingira kwamba shughuli za kiuchumi wanazojishughulisha nazo au bidhaa wanazozalisha iwe kwenye kilimo, madini, uvuvi, ufugaji nk. zinatoa tija kwao na kwa taifa kiujumla.
 
Saul goodman

Member
Aug 22, 2014
38
125
Nianze na salamu kwenu wana JF

Nikiwa kama mwanaume ambae nimeoa na kubarikiwa watoto wa 2 niseme tu naheshimu hali ya ujauzito kwa mwanamke kwan mateso ya uchungu nimeyaona

Na pia nawapongeza madaktari kwa kazi kubwa wanazofanya kutusaidia kulete viumbe hivi duniani vikiwa salama kwa uangalizi wao wa karibu

Kero kubwa ambayo kama taifa inabidi tuifanyie ufumbuzi ni hizi gharama za kujifungua kwa upasuaji na kawaida baadhi ya hospital ambacho kiwango ni laki moja mpaka laki mbili na nusu

Tuone namna ya kuliweka liwe bure kwani nimeona wamama wengi wakilalamika

Nikiwa kama mtumishi wa umma na bima ya afya pamoja na familia yangu ningeomba kiasi fulan cha pesa ninachokatwa kipelekwe kwenye account binafsi ili wamama hawa waweza kuhudumia bure.

Pia kwa wale wanaharakati wa wanawake pazeni sauti ili uzazi iwe bure na sio kikwazo kwa wanawake ,kwan sio wote wanaweza lipia hizo gharama kwani mimba inapatikana popote na wengine hutelekezwa na wenza wao hivyo kutomudu gharama na pengine wengine huona bora kutoa mimba .

Naiomba serikali yangu iliangalie hili.na pia naomba kuwe hata na kampeni ya kuchangia uzazi ili hawa wanawake ambao ni mama zetu, wake zetu, Dada zetu wahudumiwe bure

Okoa maisha ya mama mzazi ,ajifungua salama na awe na uzazi wenye furaha kwa kutoa maoni yako yanayojenga ....nini kifanyike?
Umeongea ukweli mtupu, kuongezea ifike kipindi serikali Ione umuhimu wa kuwapongeza wamama wanaojifungua kwa kuongeza raia wapya wawafirie kuwapa chochote, bila kusahau waumezao.
Kuna watu wanapinga wajawazito wasijingue Bure wakidai nchi hai fedha, upande wapili kila will haikosi habari ya upigaji wa fedha serikalini,
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
2,156
2,000
Serikali ihakikishe vifaa vya kujifungulia vipo vya kutosha kila hospitali na vituo vya afya, siyo mama mjamzito anaambiwa apeleke gloves, unakuwa ni undezi.
Kama serikali haileto hivyo vitu unataka mtoa huduma azitoe wapi ,consumables supplies Kama gloves na gauze ni ghali mno , kwa sasa zimepanda kwa zaidi ya asilima 100
 
baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,267
2,000
Kama serikali haileto hivyo vitu unataka mtoa huduma azitoe wapi ,consumables supplies Kama gloves na gauze ni ghali mno , kwa sasa zimepanda kwa zaidi ya asilima 100
Hapa inabd tuliangalie hili kama taifa ,hawa watu wanaotuletea vijana wapya duniani wapewe kipaumbele .hizo consumables zote ikibid ziwepo at AdLib .
 
Sera park

Senior Member
Feb 21, 2021
153
250
Nianze na salamu kwenu wana JF

Nikiwa kama mwanaume ambae nimeoa na kubarikiwa watoto wa 2 niseme tu naheshimu hali ya ujauzito kwa mwanamke kwan mateso ya uchungu nimeyaona

Na pia nawapongeza madaktari kwa kazi kubwa wanazofanya kutusaidia kulete viumbe hivi duniani vikiwa salama kwa uangalizi wao wa karibu

Kero kubwa ambayo kama taifa inabidi tuifanyie ufumbuzi ni hizi gharama za kujifungua kwa upasuaji na kawaida baadhi ya hospital ambacho kiwango ni laki moja mpaka laki mbili na nusu

Tuone namna ya kuliweka liwe bure kwani nimeona wamama wengi wakilalamika

Nikiwa kama mtumishi wa umma na bima ya afya pamoja na familia yangu ningeomba kiasi fulan cha pesa ninachokatwa kipelekwe kwenye account binafsi ili wamama hawa waweza kuhudumia bure.

Pia kwa wale wanaharakati wa wanawake pazeni sauti ili uzazi iwe bure na sio kikwazo kwa wanawake ,kwan sio wote wanaweza lipia hizo gharama kwani mimba inapatikana popote na wengine hutelekezwa na wenza wao hivyo kutomudu gharama na pengine wengine huona bora kutoa mimba .

Naiomba serikali yangu iliangalie hili.na pia naomba kuwe hata na kampeni ya kuchangia uzazi ili hawa wanawake ambao ni mama zetu, wake zetu, Dada zetu wahudumiwe bure

Okoa maisha ya mama mzazi ,ajifungua salama na awe na uzazi wenye furaha kwa kutoa maoni yako yanayojenga ....nini kifanyike?
Kumbe kujifungua ni gharama kubwa hivi, hapo bado maudhi ya mimba, kuumwa uchungu, kunyonyesha na kulea mbona shughuli pevu
 
Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,577
2,000
hospital zenyewe zinatosha nchi nzima Mana Kuna sehemu nyingi hata vituo vya afya hakuna.
Mi nadhani hii ya kujifungua gharama ziendekee kuwepo Mana Mungu ametupa miezi 9 yote hiyo unajua Kuna siku lazima nishushe mzigo so ni lazima kujiandaa lakini mtu mpaka siku anaingia leba hata 10 hana anategemea msaada.
Tunazalisha taifa la ajabu uzae bure, mtoto atibiwe na kusoma bure wewe mzazi utakua na kazi gani sasa?
Kama wewe ni mwanamke na umeandika haya!!! Ule usemi wa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake unazidi kuthibitishwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom