Gharama za kufunga ndoa mkoani Arusha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za kufunga ndoa mkoani Arusha.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kipindupindu, May 26, 2011.

 1. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Habari za jioni wanajamvi.
  Mimi ni kijana wa makamo na nimedhamiria kuchukua 'jiko' yaani mke mwakani.kwa wale wenye majiko au wazoefu wa kamati za harusi naomba msaada wenu katika hili.
  Ukizingatia mimi ni mtumishi wa umma mwenye kipato cha wastani ningependa kujua ni kiasi gani cha fedha(makadirio) ninahitaji kuwa nacho mimi kama mimi kabla sijaenda kujitambulisha ukweni?
  Naomba tuelezane kuhusu gharama za ukumbi,vyakula,vinywaji,mavazi ya maharusi,usafiri,mc,n.k

  ningependa harusi ifanyikie mjini arusha lakini kama kuna sehemu ambayo gharama zake ni cheaper naweze kuangalia uwezekano wa kufanyia huko.
  N.B ndoa itakua ya kikristu.

  Naamini michango yenu itasaidia wadau wengi walioko kwenye mchakato wa kufunga ndoa.
   
 2. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwani wewe budget yako ikoje?.

  Kuna harusi ya 3m, 5 m, 8m, 10m, 20m, 30m, 40m, 50m.

  In which category do you fall?

  Itasaidia sana kukupa ushauri, ili usije pewa ushauri ya 3m wakati budget yako ni 30m.

  Just thinking aloud....
   
 3. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hiyo 3m naomba mchanganuo!
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  1) Ukumbi ni darasa au hall la kanisa. 2) Vinywaji ni maji ya Uhai madogo na soda (hakuna hard drinks). 3) chakula kinapikwa na wanakamati hakuna catering, gari la maharusi linatolewa na wasamalia wema, e.t.c
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuna Kijiji kimoja kule Singida kinaitwa Kintinku! Kule hata laki moja unafunga harusi, vinywaji ni togwa na pombe za kiasili. Chakula ni rahisi pia vya kiasili, unaondoka na mkeo. Hongera kwa kuikimbia kambi ya makapela
   
 6. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Labda sijaeleweka vyema,swali langu mimi nijiandae na sh ngapi ili niwaite wanakamati?mfano hapo kwenye 3M ina maana nijiandae na nusu au robo yake.
   
 7. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mh !!tatizo liko kwa mwenzi wangu,si unajua lazima ajulikane kaolewa!
  Nimemshawishi tumchukue padre na mashahidi tumalizane amekataa katakata.
  Baba mchungaji hiyo laki inawezekana kweli si itaishia kwa wapiga mdundiko na mwanamama wa sasambua?!
   
 8. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama unataka ya kifahari kwamba wanakamati wakuchangie kuanzia 100,000/= hivi basi wewe hakikisha unayao at least 5,000,000/= na siku ya kuwaita hao jamaa angalau "upoteze" 300,000/= hadi 500,000/= kuwakirimu!! Kumbi nzuri ni kuanzia 1,000,000/= na kuendelea na mara nyingi ni gharama yako..
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ukumbi mzuri upi?NAURA SPRINGS AU?
   
 10. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Fuata taratibu za kwa unayetaka kumuoa ukikamilisha kulipa zile gharama zao wanaita sijui bride price... harusi hata laki tano unafanya inadepend tu unataka kuiweka namna gani...ushaambiwa kuna harusi za 3m, up 2 150m watu wanapiga sherehe...
  kama hauko vizuri ichakachue iwe ya kichina nenda kaanze kusaka pesa na mkeo...usijali watasema ooh! sherehe ilikuwa mbaya sijui nn the most important is that u have your wife......halafu experience gani unayotaka hapa sasa maana kama ni ndoa ya kikristu ni mke mmoja na mie naamini ili uwe na experience lazima uwe umefanya hicho ki2 kwa zaidi ya mara mbili tatu hivi sasa hiyo experience tutaitoa wapi? mie nilioa mara moja tu so sina experience..

  Son – How much does it cost to get married dad?
  Father – I don't know, I'm still paying for it.

  All the best...
   
 11. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nashukuru mkuu ila nategemea wanakamati wangu wengi watakua watumishi wa umma,nadhani michango yao mingi itakua around 50000/=
   
 12. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  thanks mkuu!experience ninayosema ni ya kuwa mwanakamati uliyebobea!
   
 13. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwanza hongera sana kwa hatua hiyo! Suala la kujitambulisha ukweni inategemea unaoa mtu wa kabila gani na ni kwa kiasi gani wanazingatia mambo ya mila zao katika zoezi hilo. Kwa mfano ikiwa ni mmasai utatakiwa kwenda na kitu wanaita mbavu na mwaka jaza kuna rafiki yangu alinunua hizo mbavu kwa laki tatu na nusu, na gharama zingine alitumia fedha mkuu, na kama ni uchagani pia unatakiwa kuandaa mshiko wa kutosha zaidi manake kuna suala zima la mbege na engagement costs!!!!. Kiasi cha kutumia kwa harusi inategemea sura ya harusi unayotaka mwenyewe ila ni vema uandae mshiko wa kutosha baba. All in all hakuna fedha zinazolingana na thamani ya kujenga familia ndugu yangu so take a step and u will get experience in the long run.

   
 14. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  kaka hiyo nimeipenda, yani hapo na change inabaki ya kwenda honey moon kwa wiki nzima Msisimko Guest House
   
 15. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
   
 16. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />


  Ha ha ha ha ha ha,Kaka umenivunja mbavu!!
  Lakini kweli,ya nn kujipa msongo wa mawazo kwa kutaka mbwembwe nyingi!!
   
 17. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu unataka kujua gharama kabla ya kupata confirmation ukweni?
   
 18. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ni muhimu!ili ujue wakwe watachukua bei gani
   
 19. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  bachela mi napunguza gharama za hiyo harusi kwa kukutolea bonge la single,:A S 103::dance:"aiyaiyaa kuolewa utarudi nyumbani kutembea..kwaheri ndugu zangu kuonana majaliwa... aiya iyaaa kuolewa tarudinyumbani kutembea.......:A S 103::dance:
   
 20. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Lolz! :biggrin:
   
Loading...