Gharama ya Wivu wa Mapenzi hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama ya Wivu wa Mapenzi hii hapa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PMNBuko, Jun 10, 2012.

 1. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja (Mhasibu) amejikuta akilazimishwa na mume wake kuacha kazi kwa kisa cha wivu mkubwa wa mwanaume anayehofia kuwa mkewe anaweza kutongozwa na wanaume. Je, hii ni halali? Wanaharakati wa haki za binadamu na wanawake mnasemaje?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  wala hii haihitaji harakati za haki za binadamu, huyo mwanamke kiazi. Anatakiwa afanya harakati za haki ya mhasibu.
   
 3. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  huyo mke kama kaacha kazi, nitamshangaa sana........... ulisomeshwa na huyo mume? ya mbele huyajui, huyo mume kesho aki-dead?
  huyo kaka anafikiri nyumbani hakuna wanaume wa kuweza kumtongoza huyo mkewe, watongozaji wapo ofisini tu?
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Naye akaacha kweli?:eek: Bora wazazi wake wasingemsomesha, bora asingesoma.
   
 5. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  na huyo kaka angetaka kuoa mama wa nyumbani si angeenda kutafuta wale waliomaliza shule za Kata? wamejaa kibao hawana pa kwenda, tunawafanya maHG
   
 6. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  of course why not............kasoma kupata maarifa bana not kuajiriwa acha alee watoto
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mwanamme ndo kasoma kuajiriwa?

  Kwa hiyo yeye ndo akatongoze wasichana huko ofisini?

   
 8. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Kama Mumewe anakipato kizuri na anaweza kumfungulia biashara sioni tatizo lakini wivu halafu mivuko inatumandu,atokomee zake.
   
 9. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Chaguo lake lilikuwa mwanamke msomi, muhasibu na mwenye experirnce ya miaka........ndo huyo sasa not from Kata Sec bana Fixed Point.............fixed mmmh...ndo mana Rigid eenh
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  hiyo biashara itakayomkutanisha na wanawake tu ni ipi?

  Wateja, saplayaz, mikopo?

   
 11. DERICK2000

  DERICK2000 JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaa ana wivu gani huo??..ila wahasibu wazuri hao..ukimkuta mwanadada wa benk au popote pale,lazima atongozwe..Pesa inatema,na ukute anakua kujiremba,lazima utupe nyavu.kama kaoa,aache ujinga.Amwamini mkewe.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo sasa. . .
  Kidogo kidogo ataona hata kuwa mama wa nyumbani haitoshi, itabidi aache kwenda sokoni, then dukani na mwisho asotoke kabisa bila mume maana hata akikaa barazani tu anaweza akatamaniwa na kutongozwa.
   
 13. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  huo usomi na experience ya uhasibu alitaka kwa ajili ya kuhesabia hela za kununulia nyanya sokoni? maana ukiwa mama wa nyumbani cha zaidi hela utakazokuwa unahesabu mara kwa mara ni zile za kununulia matembele
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Eti ehhh?
  Safi kabisa. . .na wewe usisite kusomesha mabinti zako ili wapate elimu yakukalia nyumbani.
   
 15. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Hakuna lakini sio sawa na Bank kama anaona hapo kuna watu wenye pesa zao anaonananao kila siku.
   
 16. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watu wengine bana, sasa huyo mwanaume alitongozaje huyo mke kama anahisi kutongoza ni kosa la kuachishwa kazi?
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  unongea kwa kusikia ama kwa kuona?

  Ukitaka kujua, jichanganye na wafanyabishara wa kike ndo utajua kama bank ndo sio waaminifu sana.

   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa hili mwanaharakati mkubwa ni mwanamke mwenyewe! Kwani iwapo anatimiziwa kila kitu ana haja kweli ya kufanya kazi ya kuajiriwa?
   
 19. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Hivi karne hii bado kuna wanawake wajinga kiasi hicho??siamini!
   
 20. a

  amazon Member

  #20
  Jun 10, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Looh, jamani shule ilivokuwa ngumu na mikikimikiki kibao mara supplementary, mara umenusurika ku disco..Leo hii uniambie niache kazi ntakuelewa? Huyo mwanaume ana wivu wa kijinga..
   
Loading...