Gharama ya kutengeneza kisima Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama ya kutengeneza kisima Dar

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by LadySwa, Aug 5, 2011.

 1. L

  LadySwa Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wana JF Naomba kama kuna anayefahamu gharama za kuchimba kisima kwa Dar
  anipe picha kamili,ikiwa nikuanzia kupima mkondo maji,Site ni Bunju karibu na mpiji
  natanguliza shukrani.
   
 2. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nenda pale nyuma ya chuo cha maji (Rwegalulira) jirani na university of dar es salaam. Kuna kampuni inajihusisha na uchimbaji wa visima inaitwa dams constructions co. Ltd, utapewa mchanganuo wote.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nilipotaka kuchimba kisima changu na kuona haya makampuni yanavyochimba mikwara ya utafiti tu nilichoka na kuishiwa nguvu. Nikakumbuka jana yake jirani yangu aliponiambia kuna kikundi cha vijana wajasiri mali wanachimba kisima kwa gharama nafuu na wana uzoefu wa kujua kama maji yanapatikana au laa katika eneo hilo. Nikaamua kurudi niwatafute hao vijana, na kweli walipofika eneo hilo wakafanya utafiti kutokana na visima vilivyochimwa awali na wakasema 90% maji yapo chini ya ardhi Ft 80 - 100.

  Ingwawa ilikuwa risk nilijilazimisha kuwaamini kutokana na majirani wa hapo kuwa na visima vingi tu vya maji. Bila ajizi vijana wali-drill kisima cha maji kwa zana zao za kimachinga na walipofikia Ft 55 dalili za maji zilianza na wakanihakikishia wanataka wafikishi ft 80 ili kupata maji baridi bila chumvi.

  Nikuhakikishie hadi leo napata maji safi baridiii toka Ft 80 chini ya ardhi kwa gharama nafuu sana, kwani gharama zote za kuchimba kisima na kukamilika kuweka pump ilinigharibu Tz Shs 1,200,000. Gharama hii ni tofauti na ile waliyoniambia wataalamu maana wao utafiti tu zaidi ya laki tatu zingenitoka.
  • Mambo ya msingi yanayotakiwa uyaandae ni kujaribu kuangalia waliokutangulia maeneo hayo kama wana maji ya visima na pia kujirishisha kwamba eneo lako haliko kwenye mwinuko zaidi ya wenzako walio na visima eneo lako.
  • Ukubwa wa kisima chako ni diameter ngapi kulingana na mabomba mengi yanayopatikana ambyo kwa kawaida ni mabomba magumu ya Plastic yatakayozamisha ili kuhifadhi maji ndani ya kisima chako.
  • Kuna mchanga wa pekee wa kutiwa kwenye basement ya kisima chako na kando ya bomba ili kuchuja maji yawe maangavu zaidi, wachimbaji wa visima wanajua wapi kwa kupata mchanga huo hasa kandokando ya vijito vya maji, na kuna wauzaji mitaani wa mchanga huo ila hakikisha umehakikiwa na wazoefu wa visima vya maji usijechukua mchanga unaotoa vumbi k uchafua tena maji yako zaidi.
  • Mabomba yatakayounganishwa hadi chini ambayo ni ya plastic ya kuhifadhi maji tokana na chemchemi.
  • Kifuniko cha juu kwenye kisima chako ili kulinda na kuhifahdi kisima kisiharibiwe na maji machafu yasiingie tena.
  • Pump ya maji na tank la maji.
  Maelezo hayo ni kwa kisima ambacho ni drilled ambacho pia ni salama kwa familia yako tofauti na kisima chenye shimo kubwa la kuchimbwa ambalo pia si salama kwa famili na huweza sababisha mmommonyoko wa ardhi.

  Kama nafasi inakuruhusu kuwatumia wataalamu zaidi ni bora tu ila ujue gharama nazo zinaendana na kiwango cha ukubwa na elimu ya mtu.
   
 4. u

  ureni JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,273
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mimi ninavyoelewa kuchimba kisima chini ili kupata maji ni lazima uwe na kibali,haina tofauti sana na kuchimba madini.

  Na katika kibali hicho kitakua kimeandikwa full details ya utaratibu wa uchimbaji.

  Mimi nakushauri kama unataka kuchimba maji ardhini ni lazima utumie wataalamu ambao wanavifaa vya kisasa vitakavyoeleza kama kweli maji yako chini na yako umbali gani na kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

  Wakishakuchimbia kisima na maji kutoka sio kwamba utaanza kuyatumia hayo maji moja kwa moja,itabidi wayachukue wayapeleke labolatory kwa ajili ya kupima contents ya madini yaliopo kama yako kwenye normal range ya matumizi ya binadamu.Wakati mwingine maji yanaweza kupatikana kumbe yana madini fulani ambayo ni sumu ndani ya mwili wa binadamu,kwa hiyo kwa upande wa maji ni lazima ukubali kuingia gharama kwa kutumia wataalamu kwa ajili ya maisha yako na familia yako.

  Pia wataalamu wataweza kukuambia una maji kiasi gani ardhini,hivyo utaweza kupanga mipango yako,kama kuyatumia kwa biashara au matumizi ya nyumbani.

  Nawasilisha.
   
 5. k

  kakolo Senior Member

  #5
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Wachangiaji hapo juu wote wako right, huyu wa kwanza ni kuhusu gharama, huyu Wa pili alichosema ni kweli kabisa usalama wa Maji huwa lazima upimwe na kisima kinapewa certificate ambayo unalipia si hela nyingi niliambiwa lkn nimesahau. Kama sikosei unalipa hiyo hela kila mwaka. Hiyo ndio sheria unaweza kufanya bila kufuata sheria na mambo yakawa sawa miaka yote ILA kikitokea cha kutokea labda mtu amekunywa gongo zake huko akaja akanywa Maji then akafa. Hapo shughuli zako zitasimama Kama unavyojua hata forensic hamna utaambiwa umeua. Unaweza watumia hao wachimbaji then ukakisajili Kama kawaida. Mchangiaji Wa kwanza tupatie contact za wachimbaji maana mimi pale Samora wameniambia mara Tatu ya hiyo hela ya kuchimbia. Na Kama unajua aina ya PUMP tafadhali nipatie pia.Asante.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280

  Naomba anuani au contacts zao.
   
 7. L

  LadySwa Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 25, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwanza kabisa nawashukuru wote kwa mchango wenu.Mwenzetu wewe uliyechimbiwa na wajasilimali
  ullichimbiwa maeneo gani? je unaweza kutuunganisha na hao wajasilimali ?tutawapataje?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naomba mnipe muda niwape maelekezo namna ya kuwapata. Walichimba kisima eleno la Ukonga. Najua gharama zitakuwa zimepanda maana ni miaka 4 iliyopita, ndo maana nahitaji kuwapa maelekezo maana wakati huo hawakuwa na namba za simu. Na bila shaka mtawapata kwa urahisi tu kwa vile wanajulikana sana. Maskani yao yalikuwa Mbagala. Cha msingi utakapowapata andaa sembe la nguvu maana kazi hiyo inahitaji sana shibe na ni motisha kwa kazi yao.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sipingani nawe, hilo ni jambo la msingi, ila kumbuka mtu anapochimba kisima ndani ya kiwanja chake ni tofauti na anapochimba sehemu ambayo haimiliki. Kwa usalama zaidi inafaa kusajili kisima na kuhakikiwa maji kwa usalama, lakini wengi wanakwepa hilokutokana na kwamba huwezi kuhakikiwa usalama wa maji bila kuwa na ownership certificate ambayo itakulazimu kulipia kodi kila mwaka. Sidhani kama ni big issue maji kama yatatumika na familia, lakini kama ni kwa ajili ya biashara kuongeza kipato hapo hakuna ujanja, taratibu za kisheria hapana budi zifuatwe.

  Kwa usalama wa afya ya watumiaji wa maji hata kama ni familia ni bora kupima usalama wa maji.
   
 10. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Bado unaweza kuchukua sample ya hayo maji ya kisima chako ukapeleka maabara ya private ukapimiwa maji yako kuangalia ubora wake kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu. Ardhi University (Department of Environmental Engineering) wana maabara inayotambuliwa na serikali, na wala huhitaji kuwa na hiyo ownership certificate.
   
 11. N

  Ngo JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu ahsanteni kwa info hii ya kuhusu visima. Kwa mwenye current rate price ya kuwatumia hao wataalamu wa uchimbaji wa visima tafadhari atujuze.
  Ahsante
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vijana hao wamechimba visima vingi maeneo ya Ukonga, Gongolamboto, Pugu, Chanika nk. Sikuwa na namba yao ya simu kwa vile ni mtu fulani aliyeniambia na akaenda kuwaita wakaja kufanya kazi. Nakushauri uende Gongolamboto Mwisho Stand ya Daladala wengi pale wanawafahamu sana vijana hao. Kwa sasa niko mbali na huko siwezi kutoa msaada wa karibu, niko mbali na dar, na ujuavyo mawasilino ya huku Kipili mwambao wa Ziwa Tanganyika ngumu. Ningekuwa Mazwi au Kantalamba ingekuwa rahisi kuwasilliana nao maana kuna mikongo ya wamawasiliano ya simu.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Nami naomba nipate contact zao....jamani hao vijana ni assets sana!!
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Na kweli vijana wamejiorganize na kufanya kazi nzuri na bei zao maelewano, ya nini kuwajaza mifuko wenye makampuni wenye nafasi kufanya kwa wenye nazo. Bora tunatumie vijana hawa baadaye waweze kupata zana nzuri zaidi.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Aina nzuri ya pump ni ile inayovuta maji badala ya ile inayosukuma maji.
  Pump ya kusukuma maji huzamishwa ndani ya kisima na husukuma maji yaje juu, aina hii ya pump ina matatizo mengi utahitaji kubadilisha vipuli kila kukicha na pengine kama kisima hakikuwekewa mchanga wa kutosha utashtukia tobe limeingia kwenye tank lako la maji.
  Pump ya kufuta maji ni nzuri zaidi kwa vile huwekwa nje ya kisima hivyo haikumbani na dhoruba ya maji kama ilivyo kwa ile ya kusukuma maji inayozamiswa ndani ya maji.

  Pumb hizi ziko nyingi tu Kariakoo na ule mtaa wa bei mbaya kule Samora Ave. Lakini fanya utafiti wa kutosha kupata pump inayofaa maana siku hizi zipo nyingi ambazo ni fake.
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  DDCA pale maji Ubungo ndio kazi yao lakini nisingekushauri uende huko kwani ni shirika la umma na utaletewa mizengwe. Kuna makampuni mengi binafsi wana drilling rig na wanachimba tena kwa muda mfupi; Gharama za uchimbaji kwa bei ya hivi karibuni ni kati ya 30,000 - 50,000 kwa meta moja; kutegemea na eneo, kisima huenda kati ya mita 45 na 60 kupata maji ya kutosha.
  Kadiria 3,000,000 za uchimbaji, pampu zipo za mchina 350,000 zinadumu hadi miaka 3 bila kukorofisha. Kuna gharama za bomba na viungio vyake, pia usisahau tanki pamoja na jukwaa lake.

  Kuwatafuta, nenda Kariakoo mtaa wa Msimbazi karibu na stendi ya daladala za Ubungo ulizia watakuonyesha mojawapo. Vinginevyo ulizia jirani zako wenye visima watakuelekeza waliowachimbia.
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Pampu za kukaa juu ya maji zina mapungufu yake; mojawapo ni 'suction' yaani kuvuta maji yaliyochini ambapo huipunguzia uwezo wa kupeleka maji mbali. Wakati mwingini suction pipe ikiingia upepo hushindwa kuvuta maji na kuleta usumbufu usio wa lazima.

  Pampu za kuzamisha ndani ya maji zinaitwa 'submersible' na mara nyingi hufungwa angalau mita moja toka chini ya kisima kuzuia isivute matope, vilevile hufungiwa sensor ya kukata moto kila maji yanapoisha, hivyo matumizi yake ni rahisi na mara chache sana kukuta zimeharibika.

  Zinapatikana Mtaa wa India, bei kuligana na mfuko wako.
   
 18. m

  mkumbamasaka Member

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachangiaji wote wako sawa, nami ni mmoja wa wapenda maendeleo nilipata kuwasiliana na jamaa mwenye namba 0787292917 wao gharama za kuchimba ni Tshs 2,500,000 wanakukabidhi kisima kilicho tayari, lakini wanakushauri kwanza ufanye survey ya kuhakiki kama sehemu uliyokusudia ina maji katika umbali gani na kama ni baridi gharama za survey ni Tshs 250,000 kwa takwimu nilizozipata mwezi July 2011.
  Ahsante naomba kuwasilisha
   
 19. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hapo pekundu mkuu: Bila kusahau hashish, ganja, bhangi!!!!!!!!!
   
 20. k

  kakolo Senior Member

  #20
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Jamani kupima uwepo na umbali wa maji nedeni chuo cha maji karibu na geti la Chuo Kikuu walinipimia kwa 150,000 tu. Hiyo ni bei ya mwezi wa 6, 2011. Kuhusu pump naona kuna challenge kuna wanaosema za juu nzuri na wanaosema za chini. Well nilienda pale nyuma ya duka la kuuza silaha Samora jamaa akanionyesha na sample zote za hizo mashine lakini unapokuwa huna utaalamu sana huwa haisaidii.

  Maji yangu yapo umbali wa mita 70 jamaa pamoja na pump yaani anikabidhi kisima aliniambia 3,200,000. Kuhusu Pump alisema ya kuweka ndani ya kisima na ni made in China lakini akasema pump zake eti zina classes kama vile 1 na 2 so vitu vyake ni uhakika na anafuata yeye mwenyewe. Nika mwambia fine nipe guarantee basi jamaa akaanza oo umeme hauaminiki nikamwambia vipi nikiweka stabilizer utanipa guarantee jamaa alikataa so pump bado issue kwelikweli.
   
Loading...