Gharama ya Contemporary House Ghorofa Moja

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
852
1,159
Wakuu habari za weeknd!!

Kama kichwa cha habari.kinavyoeleza, naomba kudeclare interest kwamba my dream nyumba ya ghorofa moja.

Na nimefikia kuchagua contemporary house maana nimesikia zinaunafuu kwenye suala la kuezeka paa hivyo kupunguza gharama za ujenzi.

Ukiwafuata hawa architure bei zao mara nyingi watakupa makisio ya square metre, kitu ambacho mara nyingi inaleta gharama kubwa ya kuogopesha. Japo hutofautiana kutoka eneo hadi eneo.

Nina eneo.la square metre elfu moja ambalo nataka kujenga dream house ya dizaini hiyo maeneo ya kigamboni, Dar Es Salaam. Atleast Nyumba ya Vyumba Vinne Minimum.

Mwenye uelewa na haya mambo ya makadirio ya ujenzi. Naomba msaada wa kujuzane ili tujipime kama tunaweza. Nategemea kujenga.kwa kutumia Mshahara, hivyo nitajenga polepole na kusimama huku nikivuta pumzi. Kwa kuwa nipo kwenye makazi.yangu binafsi, ninaweza kwenda polepole hata for 5 to 8 Years kulamilisha Hii dream house.

Naomba kuwasilisha kwa maelekezo kutoka kwenu wanajamvi.
View attachment 1786590
 
Makadirio ya gharama za ujenzi yanategemea na ramani ya nyumba.

Unazo structural drawings za nyumba unayotegemea kujenga?

Hiyo ndiyo hatua ya kwanza na ya muhimu kuliko hatua zote za ujenzi.

Uwe na michoro. Bila hivyo itakuwa ni porojo.
 
Tafuta ramani ndipo itajua gharama za makadilio.

Kwa maana utajua muundo wa nyumba, materials ya kutumika kujengea, ukubwa wa jengo, idadi ya vyumba, urembo etc.
 
Wakuu habari za weeknd!!

Kama kichwa cha habari.kinavyoeleza, naomba kudeclare interest kwamba my dream nyumba ya ghorofa moja...
Karibu

Screenshot_20210403-120119.png

nikujengee gharama nafuu sana

IMG_20210515_141726_209.jpg
 
Makadirio ya gharama za ujenzi yanategemea na ramani ya nyumba.

Unazo structural drawings za nyumba unayotegemea kujenga?

Hiyo ndiyo hatua ya kwanza na ya muhimu kuliko hatua zote za ujenzi.

Uwe na michoro. Bila hivyo itakuwa ni porojo.
bado sina drawings mzee. Nataka nijikadirie kwanza ili nijipime. Nikiona naweza ndio nichukue drawings.

Sitaki kubeba drawings halafu baadae nikashindwa kwenye ujenzi ikanibidi kutafuta ramani nyingine.
 
Mbona eneo unalo?

Kinachofuata hapo ni drawings. The earlier, the better.
Labda kama unataka kujenga kienyeji.

PS: Michoro ya mjengo wa ndoto zako unaweza kukupatia mwanamke mzuri na mwema. Bora hata usiwe na gari.
Mwanamke mwema yupo tayari kukusindikiza maana hujiangalia ndani ya mjengo.

So go ahead bruh, do it!
 
Huwezi kupata makadirio bila kuwa na ramani. Mimi nimejenga ghorofa ila mwanzo nilikuwa na ramani ambayo walinikadiria milioni 400 nikaona sitoweza.

Ilibidi nikae na mchoraji tukapunguza baadhi ya vitu nikapata nyumba nayoweza kuimuda nikajenga na ninaishi. Ingawa mpk leo naendelea na ukarabati na kujenga jenga yaani ujenzi hauishi
 
Kighorofa changu nilikichora mwenyewe miaka michache iliyopita na nikaanza na ujenzi. Sikutaka kukadiria saanaa maana sikutaka kuogopa gharama. Baada ya muda mfupi hali ilibadilika sana ikabidi nisimame. Bado kiko kwenye msingi ila hopefully nitaanza tena mwaka huu.

Ushauri wangu na kama wa wengine juu. Tafuta ramani. Itapendeza zaidi ukipata architect anayeweza kufika kwenye eneo lako na kukupatia design kali inayoendana na wewe na 'lifestyle' yako. Pili Structural drawings usipuuze. Mimi zimeniokoa sana. Step ya tatu ni kupata quantity surveyor, ingawa hii step mimi niliiruka.

Usiogope kutumia wataalam. Wengi wanakimbia gharama e.g. laki 5 za kupata structural drawings na kuamini mafundi wa mtaani wanaotegemea uzoefu ila ujuzi hawana na mwishowe wanajikuta wanaingia gharama kubwa mbeleni (mfano pa kuweka nondo ya 10mm fundi akakuwekea 16mm ukaingia gharama za juu au pa kuweka 16mm fundi akakuwekea 10mm ukakosa uimara, nk).

Kwa sasa naona niseme hayo tu.
 
Ahsante sana, naomba tupe summary ya ujenzi ulipofikia na gharama ulizotumia mpaka sasa. Ikikupendeza kutuonyesha na picha tutashukuru sana.
 
Niatajaribu kuweka picha nikizipata. Ni kucheki back up kama zipo maana simu yangu iliharibika. Mara ya mwisho nadhani msingi ulinigharimu kama 6.5 -7m. ingawa bado haujaisha viuri. Gharama kubwa zilikuwa kwenye labour pia. Hii ni sababu sikuweza kusimimamia ujenzi vizuri kwa ukaribu kwa sababu ilinibidi niwe kazini na kiwanja kiko mbali na eneo la kazi. Maji hakuna hivyo yanunuliwe. Matenki ya maji yawepo. Vifaa vingine mafundi wengi hawana (kama matoroli) hivyo inabidi uingie mfukoni na mafundi wengine wanatumia vibaya na kuharibu vifaa na kukurudisha aidha makusudi (mafundi kuiba cement , nondo, nk.) au kwa bahati mbaya (tairi la toroli kuvunjika). Kwa hiyo kuna vigharama vilikuwa vinajirudia rudia kiholela.
 
Aiseeee, msingi tu 7Mil...Mmmmmh hii ni hatari
 
Back
Top Bottom