Gharama kitambulisho Cha wajasiriamali iangaliwe upya

Gharama kitambulisho Cha wajasiriamali iangaliwe upya

jaruri

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2014
Posts
717
Reaction score
459
Nimekaa nikatafakari kuhusu gharama ya sh 20,000/= wanayolipia wafanya biashara wadogo ambao mitaji yao Ni chini ya Shilingi milioni nne,naona haina uhalisia.

Wafanya biashara ambao mitaji yao ni chini ya milioni 4 Ni kundi kubwa mno ambalo linahitaji kuchanganuliwa zaidi,Kuna wenye mtaji ambao Ni chini ya 10,000/= hawa ukiwaambia walipie kitambulisho Cha 20000/= kwa mtazamo wangu naona Kama unawaumiza

Kungefanyika utafiti ili ikiwezekana kuwekwe matabaka zaidi katika kundi hili,Kama itabidi hili kundi la chini zaidi lishushiwe na wale wenye mtaji unaoridhisha kdg Basi wapandishiwe iwe hata 30000/= kwa mwaka ili kufidia gap hili.
 
mimi nasema wakamuliwe zaidi ili 2020 kila mtu ajue maslahi yake yako kwenye 'line'.
 
Hivi kwann watanzania mnapenda kulalama kila siku mnataka rais awafanyeje jaman awabebe mgongoni ndio muone anawapenda

20,000/ mnaona ni kubwa kwa mwaka mzima?? Aisee! Kuongoza tanzania kweli yataka moyo namuonea hiruma sana mh. Rais kuongoza hiki kizazi. Mnatakaje sasa jaman

Ada hamlipi mashuleni kodi nying zimendolewa bado hilo hamlioni !? Yaan 20,000/ kwa mwaka bado mnalama? Hii ni nchi ya ajabu sna
 
Unasema 20,000 ni kubwa kwa mwaka mzima?
Hiyo 20,000 inalipwa kwa mkupuo mmoja. Ndio shida ipo hapo.
 
Hivi kwann watanzania mnapenda kulalama kila siku mnataka rais awafanyeje jaman awabebe mgongoni ndio muone anawapenda

20,000/ mnaona ni kubwa kwa mwaka mzima?? Aisee! Kuongoza tanzania kweli yataka moyo namuonea hiruma sana mh. Rais kuongoza hiki kizazi. Mnatakaje sasa jaman

Ada hamlipi mashuleni kodi nying zimendolewa bado hilo hamlioni !? Yaan 20,000/ kwa mwaka bado mnalama? Hii ni nchi ya ajabu sna

...ndg yangu unaishi nchi hii au wewe ni familia ya vigogo ambao mchicha na nyanya mnanunua super makert?..muuza mchicha au mihogo ya kutembeza au karanga kwenye sinia mtaji wake hauzidi elfu 7mpaka elfu 10. Mtu huyu anafamilia amepanga akiugua/kuuguliwa anategemea iyo biashara alafu unamwambia alipie kitambulisho elfu 20. Eti umemsaidia!! Kwanini asipewe bure kama unaitaji kumsaidia?

Hiyo unayosema elimu bure ndio bomu kabisa kwa watoto wetu michango ya madawati ujenzi mlinzi tunadaiwa kila siku...tokea January mwanangu alipoti shule wanakaa chini na wamejazana mpaka mlangoni..wazazi tumeambiwa tutoe elfu 50 ya dawati elfu 10 ujenzi elfu 18 kila mwezi ya majaribio ya watoto. Je iyo ni elimu bure au nikuwaadaa wananchi?

Leo mnahuburi elimu bure wakati mnatukamua wananchi watoto wanateseka manashindwa ata kuwanunulia madawati na kujenga madarasa..kwenye majukwaa ya kisiasa mnajipa sifa kwa jasho la wanyonge
 
Ada hamlipi mashuleni kodi nying zimendolewa bado hilo hamlioni !? Yaan 20,000/ kwa mwaka bado mnalama? Hii ni nchi ya ajabu sna
Hahaha umechekesha, sana
 
Hivi kwann watanzania mnapenda kulalama kila siku mnataka rais awafanyeje jaman awabebe mgongoni ndio muone anawapenda

20,000/ mnaona ni kubwa kwa mwaka mzima?? Aisee! Kuongoza tanzania kweli yataka moyo namuonea hiruma sana mh. Rais kuongoza hiki kizazi. Mnatakaje sasa jaman

Ada hamlipi mashuleni kodi nying zimendolewa bado hilo hamlioni !? Yaan 20,000/ kwa mwaka bado mnalama? Hii ni nchi ya ajabu sna
Hahaha umechekesha,
 
Wewe utakuwa sio mtanzania,,haya niambie muuza karanga za kukaanga,ananunua karanga kwa sh 2500/=,dumu mbili 5000/= anauza apate faida ya sh 3000/=,,haya unataka akupe 20000/= Ni zaidi hata ya mtaji wake ,unataka afanye Nini akafe na njaa au???
 
Ada hamlipi mashuleni kodi nying zimendolewa bado hilo hamlioni !? Yaan 20,000/ kwa mwaka bado mnalama? Hii ni nchi ya ajabu sna
Hahaha umechekesha, sana
...ada za shule zipi unaongelea ndg!? kama ni shule za kata tunapeleka watoto kukua sio kusoma hali ni mbaya sana kwenye shule hizi watoto wanarundikana kama wako zizini wanakaa chini kama ndo nchi inapata uhuru leo....kwenye kodi ndio usiseme kila kitu sasa kimewekewa kodi zaidi...
 
Wewe utakuwa sio mtanzania,,haya niambie muuza karanga za kukaanga,ananunua karanga kwa sh 2500/=,dumu mbili 5000/= anauza apate faida ya sh 3000/=,,haya unataka akupe 20000/= Ni zaidi hata ya mtaji wake ,unataka afanye Nini akafe na njaa au???
....uyu atakua hajui ata bei ya godoro analalia la nyumbani...iyo elfu 20. Anayoizarau yeye uku mtaani tunaisaka miezi kabao bila kuipa watu wanashinda bila kula ili kidogo anachopata wakakile na familia usiku...unauguliwa mtoto unakosa ata buku ya dawa alafu anatokea mtu analazimisha kukuuzia kitambulisho elfu 20 kibabe...tumevichukua lakini mioyo inanungunika
 
Kama wapo humu waambie nimeliona Hilo,mimi Niko huku chini,najua shida za watanzania kuliko wao,,na hawa wanaopinga hii hoja nadhani hawajui maisha wanayoishi watanzania wanyonge,,
 
Yaan 20,000/ kwa mwaka bado mnalama? Hii ni nchi ya ajabu sna
Kwa kweli Tanzania bado tupo mbali.

Hebu jaribu kuibadilisha hiyo 'madafu' iwe kwenye pesa yenyewe halisi. Kwa mfano hiyo 'madafu 20,000/, ni dolali ngapi hivi? tsh 20,000 /2,300/Tsh/$ = $ 8.70 kwa mwaka!

Mtu anajipinda mwaka mzima asiweze kuizalisha hiyo $8.7 mara dufu na faida juu yake?

Lakini ukweli ni kuipata hiyo Tsh 20,000/ kabla ya kuanza shughuli. Hapo ndipo palipo na shida; na huku mtaji wenyewe wa kuanzisha biashara hata Tsh30,000 haifiki! Hili ndilo tatizo. Na mtu bado hajala na matumizi mengine mhimu.

Nadhani tusitazame hiyo Tsh20,000/ pekee. Kuna mnyororo mrefu unaoambatana na kukosekana kwa hicho kiasi.
 
...ndg yangu unaishi nchi hii au wewe ni familia ya vigogo ambao mchicha na nyanya mnanunua super makert?..muuza mchicha au mihogo ya kutembeza au karanga kwenye sinia mtaji wake hauzidi elfu 7mpaka elfu 10. Mtu huyu anafamilia amepanga akiugua/kuuguliwa anategemea iyo biashara alafu unamwambia alipie kitambulisho elfu 20. Eti umemsaidia!! Kwanini asipewe bure kama unaitaji kumsaidia?...iyo unayosema elimu bure ndio bomu kabisa kwa watoto wetu michango ya madawati ujenzi mlinzi tunadaiwa kila siku...tokea January mwanangu alipoti shule wanakaa chini na wamejazana mpaka mlangoni..wazazi tumeambiwa tutoe elfu 50 ya dawati elfu 10 ujenzi elfu 18 kila mwezi ya majaribio ya watoto. Je iyo ni elimu bure au nikuwaadaa wananchi? Leo mnahuburi elimu bure wakati mnatukamua wananchi watoto wanateseka manashindwa ata kuwanunulia madawati na kujenga madarasa..kwenye majukwaa ya kisiasa mnajipa sifa kwa jasho la wanyonge
Mkuu Michaelmakene,
Bila shaka unaelewa ulaghai mwingi uliozuka hapa jukwaani JF siku hizi. Ni vigumu kuamini mengi yanayowekwa hapa jukwaani bila ya kuhoji.

Lakini sijui kwa nini inanifanya nikuamini wewe kwa hayo uliyoandika hapo juu kuwa ni kweli yanatokea huko vijijini kwetu. Kama hali ndio hii, basi safari yetu ya maendeleo bado ni ndefu!
 
...ada za shule zipi unaongelea ndg!? kama ni shule za kata tunapeleka watoto kukua sio kusoma hali ni mbaya sana kwenye shule hizi watoto wanarundikana kama wako zizini wanakaa chini kama ndo nchi inapata uhuru leo....kwenye kodi ndio usiseme kila kitu sasa kimewekewa kodi zaidi...
Hahaha hayakuwa maneno yangu ni ya mchangiaji mmoja hivi, nadhani nilikosea ku quote, hivyo kuonekana kama nimeandika Mimi.
 
Back
Top Bottom