Ghana: Mwendesha Mashtaka ya Ufisadi ajiuzulu akidai jitihada zake zinakwamishwa. Amtuhumu Rais kwa kuingilia kazi yake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwendesha Mashtaka Maalum wa kupambana na ufisadi nchini humo, Martin Amidu ametangaza kujiuzulu akisema mamlaka na jitihada zake zinakwamishwa.

Katika taarifa yake ameeleza kukosa uhuru katika kutekeleza maujukumu yake huku akimshutumu Rais Nana Akufo-Addo kwa kuingilia kazi yake, japokuwa Ofisi ya Rais bado haijajibu tuhuma hizo.

Aidha, amesema kumekuwa na ushirikiano hafifu kutoka Taasisi nyingine za Serikali na kudai yeye pamoja na Watumishi wengine wa Ofisi hiyo hawajalipwa tangu wateuliwe.

Amidu aliteuliwa na Rais Addo mwaka 2018 na wananchi wengi walitarajia makubwa, lakini matokeo yake yamekuwa sio ya kuridhisha huku wengi wakisikitishwa na uamuzi wake wa kujiuzulu.

=====

Ghana’s anti-corruption special prosecutor, Martin Amidu, has resigned saying his mandate and efforts had been compromised.

Mr Amidu’s appointment in 2018 by President Nana Akufo-Addo was greeted with great expectation in the country but the results were disappointing.

In a statement announcing his resignation, the former attorney general cited a lack of independence and freedom to execute his mandate.

He also accused President Akufo-Addo of interference although the president's office has not responded to the claim.

Mr Amidu claimed that some staff members at his office, including himself, had not been paid salaries since their appointment.

He had previously cited a lack of co-operation from other state agencies, and attempts to compromise his staff who were pursuing corruption claims against public officials.

Among some of the high profile cases he was working on included an alleged $5m (£3.8m) scandal linked to an aircraft manufacturer, and a damning assessment of the government’s attempt to engage in a controversial gold royalties deal.

Many Ghanaians have expressed disappointment at his resignation.
 
Vita dhidi ya ufisadi katika Afrika ni kazi ngumu sana kwa sababu ufisadi katika Afrika inahusisha marais waandamizi.

Tunashuhudia hapa Tanzania rais anadai kupigana vita dhidi ya ufisadi huku yeye mwenyewe akitoa fedha kununulia wapinzani ili wahamie chama chake.

Pia ananunua ndege huku akificha bei yake wananchi wake wasifahamu na wala hataki kabisa kuona mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali-CAG akikagua mahesabu ya shirika la ndege la Atcl.
 
Back
Top Bottom