Usalama wa Taifa wengi wanatoka kwa PK(Kagame)Hawawezi unga sentensi mbili zikawa fasaha mpaka nilipokuja ongea na mbongo ila wako friendly ukijua namna ya kuzungumza nao
Hii umenikumbusha mwaka 2011 tulipita na jamaa yangu kule ufukweni kisha tukaona hakuna watu tukakojoa pembezoni mwa bahari! Aisee ile siku sitaisahau maishani mwangu.. Nikipindi cha utawala wa msoga daahhNakumbuka siku moja niliingia matatani na jamaa wa suti nyeusi wale nakuaga kule nyuma ya ikulu beach kule wanao jifanyaga nao eti wanapanga upepo na hata mashati unaweza kuta wamevua.
Alikuja jamaa yangu kutoka mkoa hivyo nikaamua nimpeleke akaone bwana mkubwa wa wakati huo NKAPA anapoishi. Sasa kwa uzoefu wangu wa ule ukuta unaozunguka nyumba nyeupe kila baada ya mita tano au sita Kuna nguzo ya taa pamoja na vioo/camera ambavyo kazi yake wote twaijua.
Wakati tunapita kule upande wa beach nikawa namuelezea mgeni wangu juu ya hivyo vioo viliyo uzunguka ule ukuta wa nyumba nyeupe.katika hali isiyotarajiwa nilikuta mtu ananishika bega na kuanza nihoji vioo gani hivyo navyo zungumzia. Nilifikiria anatania tuu kumbe jamaa alikua kazini hasaaa.
Ashukuliwe mungu sikua na nia mbaya na Ile nyumba nyeupe, japo ilikua mbinde sana hadi kuwa huru.
Zama hizi za jiwe sio busara kabisa unapopita mitaa Ile kujaribu kukodolea macho eneo lile.
USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
Umenifanya nikumbuke home kwetu daahhMkuu usidhani kila kitu ni lazima kifanane na kingine, wale ni wamarekani sisi ni watanzania, kiufupi hata utaratibu wa nyumbani kwako hauwezi kufanana na utaratibu wa nyumba nyingine, ngoja nikupe kisa kimoja, mimi ni mzaliwa wa nyanda za juu kusini lakini katika kuhangaikia maisha nikajikuta nimedondokea Tanga maeneo ya Korogwe.
Sasa basi mara yangu ya kwanza kuishi hapo mahala nilishangaa vitu vingi sana, mfano kuna miiko ya kwetu ambayo huku kwa wenzetu iko tofauti, kule kwetu mama mkwe hawezi kuingia chumbani kwenu, lakini wenzetu anaruhusiwa kuingia na kukaa kitandani kwenu hata kulala kama mkwewe haupo!!
Sasa vitu kama hivyo sisi kwetu haviruhusiwi kabisa ni mwiko, ndiyo maana nikasema siyo kila kitu lazima kifanane na kingine.
Anza kusoma kutoa chini:imeandikwa Muhammed rasulu llah = Muhammed mjumbe wa Mwenyezi MunguNaweza kupata tafsiri ya maneno yaliyomo kwenye avatar yako!?
Mkuu pole kwa yaliyokupata kipindi hicho, inaonekana uli toil vya kutosha.Hii umenikumbusha mwaka 2011 tulipita na jamaa yangu kule ufukweni kisha tukaona hakuna watu tukakojoa pembezoni mwa bahari! Aisee ile siku sitaisahau maishani mwangu.. Nikipindi cha utawala wa msoga daahh
Sent using Jamii Forums mobile app
Eheee, ikawaje?Hamkuambiwa muuzoe kweli?😀😀😀😀Hii umenikumbusha mwaka 2011 tulipita na jamaa yangu kule ufukweni kisha tukaona hakuna watu tukakojoa pembezoni mwa bahari! Aisee ile siku sitaisahau maishani mwangu.. Nikipindi cha utawala wa msoga daahh
Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe unatamani kusikia maumivu ya huyu jamaa aliyekojoa ufukweni? Haaahaha ngoja ajeEheee, ikawaje?Hamkuambiwa muuzoe kweli?[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Naskia watu wanarushwa kichura kisa kushangaa sana ukuta...hivi wakikukuta unarekodi video ya jengo si unaweza kupewa uhaini kabisa
Wewe ndio jesca??[emoji23][emoji23]Mbona waoga karibuni sana nyumbani ukifika pale ulizia moto wa maji utanikuta
Kama unakuja njoo utanifahamu vizuri ukifika wala usihofie
Wewe nae ulizidi ukaamua kukojoa kabisa, tena ushukuru ilikua ni kipindi cha mzee wa Msoga.Hii umenikumbusha mwaka 2011 tulipita na jamaa yangu kule ufukweni kisha tukaona hakuna watu tukakojoa pembezoni mwa bahari! Aisee ile siku sitaisahau maishani mwangu.. Nikipindi cha utawala wa msoga daahh
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaito wale kk security hawakukaa getini waliwapisha hao jamaa kwa muda???Siku moja nilikuwa naelekea pale MWALIM NYERERE INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE...SIKUJUA KAMA KUNA EVENT PALE RAIS ANAENDA...
SASA MIMI NIKAWA NAPITA ILE NJIA KAMA NATOKEA JIMKHANA SIJUI KAMA SIO EXIM BANK(HQ)...
SASA SIWAKAWEKA BARRIER KWENYE KONA YA KUINGIA WIZARA MALIASILI NA UTALII...JAMAA MMOJA MWENYE SUTI NYEUSI AKANIFUATA...
USTADH UNAENDA WAPI BHANAH...NIKAMWAMBIA NAENDA WAPI...NILIJUA TU LABDA NI SEHEMU YA ULINZI WA ENEO LILE LA KIMATAIFA LILIVYO KILA SIKU...AKANIRUHUSU KUFIKA PALE...NIKAONA NJIA ZOTE ZIMEFUNGWA...KASORO MOJA TU...NDO TUNAPITA WATU...NIKAZIANGALIA BEJI ZAO ZINAFANANA...WAKANIULIZA KITAMBULISHO...UNAENDA WAPI KUFANYA NINI?
KITAMBULISHO SIKUWA NACHO...WAKANIKAZIA...TENA ALINIKATA JICHO AKANIAMBIA NENDA KAFUATE KITAMBULISHO URUDI...TENA ALIKUWA MKALI ALIYE SERIOUS...
NIKADHANI NI ULINZI WA KAWAIDA KILA SIKU...BAADAE NIKAKUMBUKA ZILE BEJI ZAO...NIKAPATA AKILI KUWA NI USALAMA NA RAIS ALIKUWA ANAFIKA MUDA SI MREFU...
Ivi kwa mfano ndio unapita na gari inamaana unapifishwa push up wewe na gari lako??Sitosahau hii, siku moja natokea zangu jengo lile utumishi naenda zangu hospital ya Aga khan ilikuwa siku ya J2 mida ya saa kumi hivi.
Nikapita kule nyuma ya ikulu, sasa wakati napita nikawa napita upande wa katikat jamaa mmoja akanisimamisha na kuniambia nisipite pale nikamjibu mbona wale wanapita akaniacha nikaendelea kufika mbele nikaitwa na wale waliovaa za mabaka baka, nikaanza kupigishwa push up ila siku pekee yangu niliyekuwa nikipewa adhabu tulikuwa kama sita hivi.
Bahati nzuri akatokea mwana tunayefahamina naye katika wale walio mabaka baka ndo wakaniacha jioni yake baada ya kuonana na jamaa aliyenitetea kwa kwa ushauri alionipa sikutamani kupita njia ile tena na mpka leo sijarudia kupita njia ile japo nilikuwa napenda sana kuitumia..
Sent using Jamii Forums mobile app
eeh,aise pole sana,mie hapo nilipita one day na jamaa yangu aisee sikugeuka nyuma kabisa,jamaa yangu yeye alikwa anashangashangaa tu.mie mwaka jana tu ndo ilikuwa mara yangu ya mwisho kupita eneo lile maana niliruka kichurana push ups zaidi ya 200,mwisho kabisa nikaambiwa niimbe wimbo wa taifa dah yani ilikuwa maneno ya mbele naimba nyuma ya nyuma mbele jamaa walikuwa serious mpka wakanionea huruma wakanipa mpka na maji ili presha initulie ihope hata wao walijistukia maana zile bunduki wanazobeba tu ni mashakabtosha
Sent from my iPhone using JamiiForums