Gesi ya Mtwara imeishia wapi?

Gesi ya Mtwara imeishia wapi?

dafity

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2008
Posts
1,882
Reaction score
2,092
Lilijengwa bomba la gesi toka Mtwara kwa gharama kubwa, tukaambiwa kutumia kuni na mikaa itakua mwisho. Kwamba watu watapika kwa kutumia gesi ya bei nafuu.

Pia Umeme mwingi utazalishwa kwa gesi hio mpaka tutauza nchi za nje. Sisikii tena kuhusu hio gesi, watu wanaendelea kukata mikaa, kutumia kuni na kuharibu misitu.

Serikali inawaza Umeme wa maji Stiggler's na ule wa gesi hausemwi tena.

Anayejua kuhusu hii gesi utujuze wandugu. Isije kuwa inavunwa na wageni kwa mikataba ya kimya kimya tusiyoijua. Na sikumbuki kama kuna kamati ya gesi iliyoundwa mithili ya ile makinikia.
Karibuni wanajamvi....
 
Gesi ya Mtwara haijafika dar wala yale mabomba hayajifika hadi mtwara.. mengine jiongeze
 
Lilijengwa bomba la gesi toka Mtwara kwa gharama kubwa, tukaambiwa kutumia kuni na mikaa itakua mwisho. Kwamba watu watapika kwa kutumia gesi ya bei nafuu.

Pia Umeme mwingi utazalishwa kwa gesi hio mpaka tutauza nchi za nje. Sisikii tena kuhusu hio gesi, watu wanaendelea kukata mikaa, kutumia kuni na kuharibu misitu.

Serikali inawaza Umeme wa maji Stiggler's na ule wa gesi hausemwi tena.

Anayejua kuhusu hii gesi utujuze wandugu. Isije kuwa inavunwa na wageni kwa mikataba ya kimya kimya tusiyoijua. Na sikumbuki kama kuna kamati ya gesi iliyoundwa mithili ya ile makinikia.
Karibuni wanajamvi....
Iko Njiani Mkuu,
Si wajua Mtwara Mbali,
Itafika tu
 
Gesi ipo inatumika kuzalisha umeme tu nao kidogo haina presha ya kujaza bomba inatumika 16% ya bomba zima haiwezi kutumika kwa matumizi mwngine
 
1967 tuliambiwa tunakuwa Taifa la Ujamaa na kujitegemea!, aliehubiri hayo kwa 23 years kafia Ughaibuni St Thomas kwenye hospital ya Kipebari

Mwanasiasa sio Mtu wa mchezo
[emoji87] [emoji87] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
1967 tuliambiwa tunakuwa Taifa la Ujamaa na kujitegemea!, aliehubiri hayo kwa 23 years kafia Ughaibuni St Thomas kwenye hospital ya Kipebari

Mwanasiasa sio Mtu wa mchezo
Aliyefia hospitali hiyo ya kibepari alitaka kutibiwa huko au waliompeleka ndio walioamua akatibiwe huko?
 
Gesi ipo inatumika kuzalisha umeme tu nao kidogo haina presha ya kujaza bomba inatumika 16% ya bomba zima haiwezi kutumika kwa matumizi mwngine
Kwahiyo walitudanganya kwa kutupa matumaini ambayo hayakufanyiwa tathmini ya kutosha kabla.
 
Back
Top Bottom