Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,353
- 26,194
Imekuwa kawaida kwa siku za karibuni,viongozi wa kiserikali na wa kisiasa,walioko madarakani na wastaafu,kutoa matamko juu ya suala la gesi Mtwara. Matamko yanajaribu kutoa maoni na hisia za wahusika ili waonekane nao wamesema. Kiukweli,suala hili la gesi Mtwara halihitaji matamko.
Suala la gesi asilia la Mtwara limebeba ujumbe fichwa tofauti kabisa na unaoonekana. Wapo wanaoona kana kwamba suala hili ni la kisiasa na linatumika kama turufu ya wanasiasa kujijenga. Wapo pia wanaoamini kuwa suala hili limejawa na taswira ya uchoyo ya watu wa Mtwara kukataza rasilimali za nchi moja zisitumike na wananchi wengine. Wapo wanaodhani kuwa hili ni suala la muda tu na mambo yatapoa punde...ni upepo tu utapita!
Binafsi,sikubaliani hata na kundi moja hapo. Nalitafuta kundi linalotafsiri suala hili kama nafasi adhimu ya wana-Mtwara kuiambia Serikali kuwa 'na sisi ni raia wa nchi hii na tunahitaji huduma za kijamii'. Katika masomo yangu ya sheria,Wahadhiri wangu walinifunza 'principle' moja iitwayo 'last straw doctrine'.Hapa hutokea mtu aliyehifadhi maudhi toka kwa mwingine kwa muda mrefu,kwa aina mbalimbali za matendo ya huyo mwingine,anapoibuka na kufanya jambo kubwa hata kama linatokana na jambo dogo.
Kwa mfano,mtu aweza kuua eti tu kwasababu aliyeuawa alimzaba kibao tu! Hivi ndivyo wana-Mtwara wanavyofanya. Gesi asilia ni turufu adhimu ya wana-Mtwara kusikilizwa.Kile kilio cha muda mrefu, kuwa mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara imetengwa kimaendeleo,sasa kitasikilizwa.Watu wa Mtwara,katika vuguvugu hili,hawailengi gesi tu.Wanalenga kupata huduma bora za kijamii kama maji,barabara,elimu,huduma za afya nk.
Serikali na isikie. Iende kuwaonesha kimatendo watu wa Mtwara kuwa ipo pamoja nao. Iwaoneshe kimatendo kuwa huduma za kijamii zinagawanywa sawa kwa mikoa yote 30 ya Tanzania. Matendo yaseme kuwa anachokipata mkazi wa Dar es Salaam ndicho akipatacho wa Mtwara.....barabara za Kilimanjaro ndio hizohizo za Mtwara.
Matamko na maoni yanaichelewesha Serikali.Isije ikawa Serikali ikageuka Tume ya kupokea na kuratibu maoni na kuchelewa kuchukua hatua.Watu wa Mtwara hawatakubali kurudi nyuma kiurahisi hata kama watasalitiwa na wanaoonekana kuwa ni viongozi wao. Sababu kuu ni moja:hawatakubali kupoteza nafasi yao pekee iliyobaki kutetea ustawi wao.
Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania!