Gesi tumetapeliwa, Ndege hasara tupu, Korosho vurugu tupu, Makinikia cha kike, nini wanaweza?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Ukiangalia kwa jicho la tatu ni kama serikali imeshindwa kwenye sekta ya uchumi, maana karibu kila mipango inayoanzisha ina feli, mfano wa karibu ni sera ya viwanda ni kama imekufa.

Kwangu mimi labda kitu tangible ambacho serikali inaweza kujivunia na ambacho kinaonekana wazi ni ujenzi wa SGR, ingawa huwezi kujua madudu ya ndani, ujenzi huu ukimalizika kwa ufanisi utasaidia sana kuinua uchumi wa nchi na wa wananchi wa hali ya chini.

Pamoja na ujenzi wa Stieglas Gorge kuanza lkn bado nina wasi wasi kama utakuwa sustainable, kwa sababu ni mradi unaotegemea majira, ni old fashioned technology.

Hii miradi ni mikubwa inatumia reserve yetu na kuongeza deni la taifa, kwahiyo Serikali haina budi kubuni miradi simple ambayo utekelezaji wake unaendana kulingana na uwezo wetu na siyo kila kitu kuiga kwa majirani, Ethiopia wakijenga bwawa na sisi tujenge, Rwanda wakinunua ndege na sisi tunanunua bila mpango stahiki, huwezi kujua wenzetu walijiandaa kwa muda gani kutekeleza miradi yao.
 
Hata SGR ni usanii mtupu, haijulikani inajengwa kwa fedha za ndani au mkopo. Steve Nyerere alienda kukagua mradi. Hii nchi ina vituko sana.
Nilivoona bashite kaenda na wasanii kukagua mradi was SGR, nikasema basi chaka lingine hili. Papo hapo imani ikanitoka kwa kiasi kikubwa.
Kibaki wa kenya alibadilisha sura ya Nairobi, hapakua mbwembwe kama kwetu huku. Kenya ina ndege nyingi, sijawahi ona rais akipokea ndege.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilivoona bashite kaenda na wasanii kukagua mradi was SGR, nikasema basi chaka lingine hili. Papo hapo imani ikanitoka kwa kiasi kikubwa.
Kibaki wa kenya alibadilisha sura ya Nairobi, hapakua mbwembwe kama kwetu huku. Kenya ina ndege nyingi, sijawahi ona rais akipokea ndege.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania mbwembwe nyingi, tuliambiwa siku gesi ya Mtwara ikikamilika umeme utakuwa bei karibu na bure, siku Rais anaongea na yule mzungu wa makinikia alituambia wamekubali kutulipa, siku Rais anapokea ndege alituambia Boeing wametupa na ndege ya nyongeza, yaani nchi hii ni pasua kichwa.
 
Hata SGR ni usanii mtupu, haijulikani inajengwa kwa fedha za ndani au mkopo. Steve Nyerere alienda kukagua mradi. Hii nchi ina vituko sana.
Hahahaha ni Taifa lenye vioja kuliko Taifa lolote Duniani kwa sasa, kwenye ujenzi wa Reli tenda zote za Ku-supply Kokoto mchanga na cement ni kampuni binafsi za mtukufu malaika na Bashite huku kukiwa na idadi kubwa ya Wasukuma ndugu na rafiki zake Bashite wakiwa ni waajiriwa kwenye Ukaguzi wa Ujenzi wapambe wa Bashite wote huenda kukagua Ujenzi hata Cyprian musiba na Le mutuz huenda kukagua kuna vituko vingi huko.
 
Hata kujenga jengo LA makao makuu mmeshindwa kazi yenu kupanga kwenye frame kama mnauza maharagwe, je MNA uhalale wa kuhoji mambo makubwa kama mambo madogo hivyo mmeshindwa?
Ufipa mmeshindwa teyari kabla hamjaanza
 
Back
Top Bottom