Gesi iliyopo Tanzania kutumika kwenye magari badala ya petroli

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
415
359
Kwanini Gesi inayo zalishwa Tanzania kwasasa isitumike kwenye Magari ??,

Tanzania tukiamu kwenye hili tutajigemea kwa kiasi kikubwa katika nishati ya usafirishaji (Transportation fuel).

Kwasasa Tanzania tuna magari yanayo kadiriwa kama 700,000 yaliyo sajiliwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2014 ambapo asilimia sitini (60) ya hayo magari yanatumia mafuta ya Petroli au Gasolini.

Ambapo magari haya yanayotumia Petroli ndio yanaweza kubadilishwa kiurahisi ili yatumie gesi asilia iliyogandamizwa (CNG=Compressed Natural Gas). Yapo magari machache ambayo tiari yamebadirishwa na yanatumia gesi asilia iliyogandamizwa hapa Tanzania.

Zipo nchi nyingi zilizo na Gesi asilia mpaka sasa ambazo asilimia kubwa ya magari yao yanatumia gesi asilia.

Mimi hua nasema siku zote kuwa nchi inayo jitegemea kwenye swala la nishati ndio nchi tajiri. Hatuna haja ya kuendelea kutegemea Petroli kutoka nchi za nje wakati tunayo gesi ambayo inaweza kubadirishwa ili itumike kwenye magari. Mimi najua tukiamua tunao uwezo wa kujitegemea kwenye nishati ya usafirishaji (transportation fueli).

Hizi ni faida tutakazo zipata endapo kama tutatumia gesi asilia iliyo gandamizwa kwenye magari (CNG= Compressed Natural Gas)

Kwanza tutajijengea uwezo wa kujitegemea katika nishati ya mafuta ya petroli, ambapo kama huko mbele litatokea tatizo lolote la kukosekana kwa nishati ya petroli au bei kupanda sana hatuta athiliwa.

Pili tutaingiza kipato kikubwa kwa taifa letu, kwa makusanyo ya Kodi na kwa kuwauzia wananchi wetu gesi yetu ambao ni wengi kwasababu magari yanayo tumia Petroli mengi.

Tatu tutapata wateja wa gesi yetu kiurahisi tu kwa kujiuzia gesi sisi wenyewe. Ambapo magari tiari tunayo ya kutosha yataitumia gesi hiyo.

Nne tutatengeneza fursa nyingi za ajira katika nchi yetu.

Hizi ni baazi ya nchi na mabara yanatumia gesi asilia iliyo gandamizwa kwenye magari ni Iran, Pakistan , Maeneo pasifiki uko Asia, India, Amerika ya Kusini, Ulaya na Amerika ya kaskazini.
 
Tatizo siyo gesi,ila bei itakuwa juu au itauzwa bei ya soko,kwa sababu Serikali siyo yenye gesi ila ni mbia kwa hiyo itauzwa bei ya soko,halafu mtambo wa LPG itakuwa ni ya kampuni ingine hivyo watataka faida pia,ukilinganisha na Lpg y a qatar ambayo yote ni mali ya serikali,hivyo usishangae gesi ya nje ikawa rahisi.
 
Hii nchi viongozi ni makapi kwakweli.......yaani wametuingiza mamikataba ambayo mwisho wa siku yanakujatufanga sisi wenyewe tunahisi tunakwepa gharama kumbe tunazifuata shenzi kabisa
 
Miye nilikuwa nasubiria kwanza hilo ya kusambazwa huku majumbani sijaiona, sijui imeota mabawa. Navyojuwa mimi kama magari yataitaji kubadilishwa mfumo kuweka huo mtungi wa gesi.

Pili miundombinu kwenye stations za kujazia mafuta itabidi waweke na sehemu ya kujazia gesi.

Kwahiyo hii itakuwa big investment kwa wenye magari kubadilisha mfumo na wenye vituo vyao itabidi waongeze hiyo miundo mbinu. Hata huko ambako wanatumia gas kwenye magari kunachangamoto manake hakuna anayetengeneza magari yakawa na mfumo wa lpg moja kwa moja.
 
Miye nilikuwa nasubiria kwanza hilo ya kusambazwa huku majumbani sijaiona, sijui imeota mabawa. Navyojuwa mimi kama magari yataitaji kubadilishwa mfumo kuweka huo mtungi wa gesi. Pili miundombinu kwenye stations za kujazia mafuta itabidi waweke na sehemu ya kujazia gesi. Kwahiyo hii itakuwa big investment kwa wenye magari kubadilisha mfumo na wenye vituo vyao itabidi waongeze hiyo miundo mbinu. Hata huko ambako wanatumia gas kwenye magari kunachangamoto manake hakuna anayetengeneza magari yakawa na mfumo wa lpg moja kwa moja.
Penye nia pana njia, tukiwa na nia hata jambo liwe gumu kiasi gani, linawezekana
 
Hili limeongelewa muda mrefu utekelezaji uko slow sana kuna nchi za Asia matumizi ya gas ni makubwa kuliko petrol na kuna nafuu kubwa kufananisha na bei ya petrol na diesel
 
Haya mambo sio kwa serikali ya CCM jaribuni akili nyingine yatawezekana kwa hawa tuliowapa nchi ni porojo tyu ndio kwanza wanasainisha mikataba feki ya kuuza gesi
 
Gas ilikuwa priority ya JK! Magufuli haoneshi kama uzalishaji wa gas ni kipaumbele chake! Na ndio maana, wakati JK alijenga bomba la gas lenye uwezo mkubwa maradufu ili liweze kutumika at full capacity wakati uzalishaji wa gas utakapoongezeka, JPM ndo kwanza hata umeme anaomba kutoka Ethiopia huku pia akijaribu kufufua mradi wa Stigler's Gorge... ni kwa sababu, inaonekana matumizi ya gas kama chanzo cha nishati sio tena kipaumbele labda hadi atakavyomalizana na makinikia
 
Kwanini Gesi inayo zalishwa Tanzania kwasasa isitumike kwenye Magari ??,

Ambapo magari haya yanayotumia Petroli ndio yanaweza kubadilishwa kiurahisi ili yatumie gesi asilia iliyogandamizwa (CNG=Compressed Natural Gas). Yapo magari machache ambayo tiari yamebadirishwa na yanatumia gesi asilia iliyogandamizwa hapa Tanzania.

Mkuu, inawezekana, lakini sio rahisi kama unavyofikiria. Kwanza kuna suala la magari yenyewe. Kumbuka kwamba kama utabadili itabidi unadilishe mfumo mzima wa nishati (fuel system) ambapo gesi na petroli ni tofauti sana. Kuna sehemu ambazo seals za petroli kama liquid haziwezi kuwa effective kama seals za gesi. Na pia kumbuka kwamba gesi inawaka kwa joto kubwa zaidi ya petroli, kwa hiyo kuna vitu ambavyo lazima ubadilishe ili gari yake isije ikakulipukia.

Pia kuna suala la tenki za gesi, ambapo lazima ziwe na ukuta (walls) mnene sana ili kuwa salama. Na mara nyingi zinatakiwa ziwe sehemu ambayo hata gari ikigongwa nyuma au mbele haziwezi kupasuliwa kwa ajali, la sivyo ni hatari sana. Fikiria unaendesha gari ya gesi halafu ukapiga mzinga huo mlipuko utakaotokea! Kwa hiyo tenki zinakuwa ni nzito sana, na hivyo kubadili kwa gari ndogo utakuta ukiwa na tenki zimejaa gesi tayari una mzigo mkubwa huwezi kubeba abiria na mizigo tena! Kwa hiyo mara nyingi gari kubwa zenye kubeba mzigo mkubwa ni rahisi kuziwekea tenki za gesi kuliko gari ndogo.

Na changamoto nyingine ni kuwa na sehemu za kujazia gesi. Kumbuka gesi utakayojaza sio rahisi ikumbe umbali wa kusafiri sawa na petroli hivyo unahitaji sehemu nyingi za kjazia hasa kwa safari za mikoani.

Na zaidi basi, kubadilisha mfumo toka petroli kwenda gesi ni gharama sana, ukitaka hilo lifanyike kwa usalama. Nani atakubali na kuibeba hiyo gharama? Ukifanya na gereji za mitaani itakuwa sawa na kutembeza mambomu barabarani, muda wowote kitalipuka! La sivyo itabidi tupige marufuku sigara nchini.Nilishangaa sana siku moja waziri mmoja akiongea bungeni eti gesi yetu itatusaidia kwenye magari! Viongozi yeboyebo wasiojua wasemalo.

Angalia hapa chini gari ililipuka baada ya kubadilishwa mfumo wa petroli kwenda gesi bila kuzingatia mambo ya usalama. Unafikiri watu walipona? Mkuu ukibadilisha gari yako naomba usinipe lift:D:D:D

upload_2017-11-14_14-7-17.png
 
Kwanini Gesi inayo zalishwa Tanzania kwasasa isitumike kwenye Magari ??,

Tanzania tukiamu kwenye hili tutajigemea kwa kiasi kikubwa katika nishati ya usafirishaji (Transportation fuel).

Kwasasa Tanzania tuna magari yanayo kadiriwa kama 700,000 yaliyo sajiliwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2014 ambapo asilimia sitini (60) ya hayo magari yanatumia mafuta ya Petroli au Gasolini.

Ambapo magari haya yanayotumia Petroli ndio yanaweza kubadilishwa kiurahisi ili yatumie gesi asilia iliyogandamizwa (CNG=Compressed Natural Gas). Yapo magari machache ambayo tiari yamebadirishwa na yanatumia gesi asilia iliyogandamizwa hapa Tanzania.

Zipo nchi nyingi zilizo na Gesi asilia mpaka sasa ambazo asilimia kubwa ya magari yao yanatumia gesi asilia.

Mimi hua nasema siku zote kuwa nchi inayo jitegemea kwenye swala la nishati ndio nchi tajiri. Hatuna haja ya kuendelea kutegemea Petroli kutoka nchi za nje wakati tunayo gesi ambayo inaweza kubadirishwa ili itumike kwenye magari. Mimi najua tukiamua tunao uwezo wa kujitegemea kwenye nishati ya usafirishaji (transportation fueli).

Hizi ni faida tutakazo zipata endapo kama tutatumia gesi asilia iliyo gandamizwa kwenye magari (CNG= Compressed Natural Gas)

Kwanza tutajijengea uwezo wa kujitegemea katika nishati ya mafuta ya petroli, ambapo kama huko mbele litatokea tatizo lolote la kukosekana kwa nishati ya petroli au bei kupanda sana hatuta athiliwa.

Pili tutaingiza kipato kikubwa kwa taifa letu, kwa makusanyo ya Kodi na kwa kuwauzia wananchi wetu gesi yetu ambao ni wengi kwasababu magari yanayo tumia Petroli mengi.

Tatu tutapata wateja wa gesi yetu kiurahisi tu kwa kujiuzia gesi sisi wenyewe. Ambapo magari tiari tunayo ya kutosha yataitumia gesi hiyo.

Nne tutatengeneza fursa nyingi za ajira katika nchi yetu.

Hizi ni baazi ya nchi na mabara yanatumia gesi asilia iliyo gandamizwa kwenye magari ni Iran, Pakistan , Maeneo pasifiki uko Asia, India, Amerika ya Kusini, Ulaya na Amerika ya kaskazini.

Serikali inamiliki asilimia ngapi? Tofauti ya bei kati ya petrol na gas yaweza kuwa ndogo ukijumlisha gharama za conversion kits kwenye bei ya gas, labda serikali iwe na umiliki wa asilimia kubwa kwenye gas itakayozalishwa.
 
Mkuu, inawezekana, lakini sio rahisi kama unavyofikiria. Kwanza kuna suala la magari yenyewe. Kumbuka kwamba kama utabadili itabidi unadilishe mfumo mzima wa nishati (fuel system) ambapo gesi na petroli ni tofauti sana. Kuna sehemu ambazo seals za petroli kama liquid haziwezi kuwa effective kama seals za gesi. Na pia kumbuka kwamba gesi inawaka kwa joto kubwa zaidi ya petroli, kwa hiyo kuna vitu ambavyo lazima ubadilishe ili gari yake isije ikakulipukia.

Pia kuna suala la tenki za gesi, ambapo lazima ziwe na ukuta (walls) mnene sana ili kuwa salama. Na mara nyingi zinatakiwa ziwe sehemu ambayo hata gari ikigongwa nyuma au mbele haziwezi kupasuliwa kwa ajali, la sivyo ni hatari sana. Fikiria unaendesha gari ya gesi halafu ukapiga mzinga huo mlipuko utakaotokea! Kwa hiyo tenki zinakuwa ni nzito sana, na hivyo kubadili kwa gari ndogo utakuta ukiwa na tenki zimejaa gesi tayari una mzigo mkubwa huwezi kubeba abiria na mizigo tena! Kwa hiyo mara nyingi gari kubwa zenye kubeba mzigo mkubwa ni rahisi kuziwekea tenki za gesi kuliko gari ndogo.

Na changamoto nyingine ni kuwa na sehemu za kujazia gesi. Kumbuka gesi utakayojaza sio rahisi ikumbe umbali wa kusafiri sawa na petroli hivyo unahitaji sehemu nyingi za kjazia hasa kwa safari za mikoani.

Na zaidi basi, kubadilisha mfumo toka petroli kwenda gesi ni gharama sana, ukitaka hilo lifanyike kwa usalama. Nani atakubali na kuibeba hiyo gharama? Ukifanya na gereji za mitaani itakuwa sawa na kutembeza mambomu barabarani, muda wowote kitalipuka! La sivyo itabidi tupige marufuku sigara nchini.Nilishangaa sana siku moja waziri mmoja akiongea bungeni eti gesi yetu itatusaidia kwenye magari! Viongozi yeboyebo wasiojua wasemalo.

Angalia hapa chini gari ililipuka baada ya kubadilishwa mfumo wa petroli kwenda gesi bila kuzingatia mambo ya usalama. Unafikiri watu walipona? Mkuu ukibadilisha gari yako naomba usinipe lift:D:D:D

View attachment 630751
Duuh hili ni bonge LA bomu
 
Hahaha! Mkuu nikibadili mfumo wa gari yangu naweza kukupa gari ukatanue na shemeji yangu, sina pressure na gari yangu mie:)
Kubadili huu mfumo kwenye starlet ni mzigo tosha mkuu
BTW naweza badili pia kwenye power tila yangu!??
 
Kumbe unazungumzia kujitegemeaa???
Hilo sahau mkuu..
Tumeshindwa miaka 50 iliyopita..hapa mpka upinzani ipite ndo hayo mnayoyasema yatatokea
 
Kwanini Gesi inayo zalishwa Tanzania kwasasa isitumike kwenye Magari ??,

Tanzania tukiamu kwenye hili tutajigemea kwa kiasi kikubwa katika nishati ya usafirishaji (Transportation fuel).

Kwasasa Tanzania tuna magari yanayo kadiriwa kama 700,000 yaliyo sajiliwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2014 ambapo asilimia sitini (60) ya hayo magari yanatumia mafuta ya Petroli au Gasolini.

Ambapo magari haya yanayotumia Petroli ndio yanaweza kubadilishwa kiurahisi ili yatumie gesi asilia iliyogandamizwa (CNG=Compressed Natural Gas). Yapo magari machache ambayo tiari yamebadirishwa na yanatumia gesi asilia iliyogandamizwa hapa Tanzania.

Zipo nchi nyingi zilizo na Gesi asilia mpaka sasa ambazo asilimia kubwa ya magari yao yanatumia gesi asilia.

Mimi hua nasema siku zote kuwa nchi inayo jitegemea kwenye swala la nishati ndio nchi tajiri. Hatuna haja ya kuendelea kutegemea Petroli kutoka nchi za nje wakati tunayo gesi ambayo inaweza kubadirishwa ili itumike kwenye magari. Mimi najua tukiamua tunao uwezo wa kujitegemea kwenye nishati ya usafirishaji (transportation fueli).

Hizi ni faida tutakazo zipata endapo kama tutatumia gesi asilia iliyo gandamizwa kwenye magari (CNG= Compressed Natural Gas)

Kwanza tutajijengea uwezo wa kujitegemea katika nishati ya mafuta ya petroli, ambapo kama huko mbele litatokea tatizo lolote la kukosekana kwa nishati ya petroli au bei kupanda sana hatuta athiliwa.

Pili tutaingiza kipato kikubwa kwa taifa letu, kwa makusanyo ya Kodi na kwa kuwauzia wananchi wetu gesi yetu ambao ni wengi kwasababu magari yanayo tumia Petroli mengi.

Tatu tutapata wateja wa gesi yetu kiurahisi tu kwa kujiuzia gesi sisi wenyewe. Ambapo magari tiari tunayo ya kutosha yataitumia gesi hiyo.

Nne tutatengeneza fursa nyingi za ajira katika nchi yetu.

Hizi ni baazi ya nchi na mabara yanatumia gesi asilia iliyo gandamizwa kwenye magari ni Iran, Pakistan , Maeneo pasifiki uko Asia, India, Amerika ya Kusini, Ulaya na Amerika ya kaskazini.
Pale oilcom Kijitonyama wapo wachina wanafunga konvetor ya kuwezesha gari kutumia gas.
Pale ubungo Chibuku kuna gas filling station kwa magari yanayotumia gas
 
Yaani magari ya watu afu tubadilishe
So mtengenezeni magari yenu
 
Back
Top Bottom