Mleta mada fanya hesabu zako vizuri. Gesi gani unatumia muda mfupi hivyo na hauna familia? Sisi wenye familia kuna muda tunatumia mtungi mkubwa hadi tunasahau.
Gesi ni bora zaidi, Kama una ka uwezo nunua gesi, jibane bane nunua pressure cooker kwaajili ya maharage, makande, nyama etc.
Kinachofanya watu wang'ang'ane na mkaa si unafuu bali ni upatikanaji wa hela, Watz wengi wanafanya vibarua na wanalipwa kwa siku, bajeti ya siku inaanza baada ya hela kupatina siku hiyo, ndio mambo ya mkaa wa 1500 yanaanzia hapo.
Lakini kama mtu unapata pesa ya mara moja gesi is cheap.