Miguel255
Member
- May 13, 2020
- 35
- 111
Girishoni hajaongea kitaaluma, bali ameongea kisiasa. Nguli wa taaluma ya habari, Walter Lippmann aliwahi kusema "In opinion we seek two sides, but facts have no two sides" Akimaanisha Maoni yana pande mbili, lakini uhalisia hauna pande mbili. Mvua ikinyesha, huhitaji pande mbili ili kuandika imenyesha. Watu wamepigwa risasi na maiti zimezagaa mtaani, ni mwendawazimu pekee atakuambia usiandike watu wamekufa hadi upate maoni ya upande wa pili. Je upande wa pili ukitoa maoni itabadilisha fact kuwa hawajafa?
Hata hivyo serikali ilipewa nafasi lkn ikagoma kutoa ushirikiano (kwa mujibu wa CNN). Katika taaluma ya habari, upande mmoja ukigoma kutoa ushirikiano, habari haifi. Habari itaandikwa na ule upande uliogoma utatajwa. Hiyo ni kanuni ya Fairness and Objectivity (SPJ Code of Ethics). Inafundishwa mwaka wa kwanza, kwenye Introduction to News Reporting. Girishoni sijui alikua amesinzia? Amesahau hata mahakamani, kesi inaweza kusikilizwa upande mmoja ikiwa upande wa pili umegoma kutoa ushirikiano (Ex parte).
Swali ambalo Girishoni anatakiwa kujibu ni kwanini Polisi waliua waandamanaji wasio na silaha? Duniani kote waandamanaji hutawanywa kwa mabomu ya machozi (tear gas), maji ya kuwasha, au risasi za plastiki – siyo risasi za moto. Hilo ni kosa kisheria (Crime Against Humanity) kwa mujibu wa Rome Statute 7(1)(a).
Soma Pia: Gerson Msigwa: CNN imechapisha taarifa zenye tuhuma kwa Serikali pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu
Girishoni amelaumu CNN kwa kutoipa serikali nafasi ya kujibu, lakini na yeye amefanya press ya kulaumu CNN bila kuipa nafasi ya kujibu wala kuialika kwenye press. Ama kweli nyani haoni kundule.
Na tangu mauaji yatokee hadi leo mlikuwa wapi mpaka CCN ilipowakurupusha? Ina maana CNN isingeripoti mngeendelea kukaa kimya wakati roho za watu zimepotea?
Halafu Girishoni wewe ni wa kuwafundisha CNN Principle of natural justice kweli? Hivi unajua Benjamin Strick, mtaalamu wa uchunguzi wa CNN, ana degree ya sheria (LLB) na Masters ya Investigative Journalism. Ana tuzo nyingi ikiwemo OSINT Champion of the Year. Unafikiri huyu atashindwa kuona "loopholes" kwenye habari halafu wewe uone? Wakati Strick akiwa Mkuu wa dawati habari za uchunguzi pale BBC mwaka 2014 wewe ulikuwa unaripotia TBC kutokea Namtumbo, leo unamfundisha Natural Justice? Hebu punguza Futuhi.!
Imeandikwa na Malisa G.J