Germany's gold lost secrets discovered in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Germany's gold lost secrets discovered in Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by bagamoyo, Apr 5, 2011.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  • Central Tanzania in Dodoma Region
  Video hisani ya Hildebrandshayo wa Youtube

  Habari za ziada kuhusu madini bwerere Tanzania toka Raiamwema Toleo namba 180 la tarehe 6-12 ,Aprili 2011:
  Mahojiano ya Godfrey Dilunga wa gazeti la Raiamwema na Dr.Mselly Nzotta mtaalamu wa Metallurgy anayetamba kitaaluma Sweden anatoa data za ziada:

  Dr. Nzotta: Kuna ramani niliyompa inayoonyesha kwamba kuna gold belt (mkondo/mkanda wa dhahabu) kutoka Ziwa Victoria umepitia katikati ya Tanzania, mkoani Dodoma mpaka kufika Afrika Kusini, lakini chimbuko lake ni Bukoba.
  Nikamwuliza inakuwaje mwananchi wa Bukoba ana mali ya thamani kubwa chini ya ardhi kama hiyo, lakini hata kununua chumvi hawezi? Akanijibu kwamba; nimuandikie na akanipa anuani yake binafsi ili watu wengine wasinizubaishe katika ufuatiliaji wa mpango wangu.

  Raia Mwema: Baada ya hapo nini kilifuata? Ulisaidiwa kuhamisha vifaa vya maabara kutoka Sweden?

  Dk. Nzotta: Baada ya miaka kadhaa, wakaja (Kikwete) wakiwa na Mkapa (Rais) pale Sweden. Walivyokuja nikapata nafasi pia ya kujieleza kwa Mkapa. Tatizo lililokuwapo kwa wakati ule nilipokuwa najieleza nilimwita Mkapa "Mtukufu Rais". Sasa kumbe huku nyumbani alikuwa amekwishakataza kuitwa hivyo. Mimi sikuwa na hizo taarifa, kwa hiyo nilikuwa kila mara nikimwita hivyo.
  Alichukia sana nilipomwita "Mtukufu Rais". Alikasirika kiasi cha maelezo yangu kutokuwa na maana tena kwake, na hakuna alichojibu zaidi ya kukasirika na kueleza kuwa watu wa Sweden "hatuna heshima". Nilimweleza tena Waziri (Kikwete) lakini naye akasema hana cha kufanya tofauti na msimamo wa mzee (Rais).

  Raia Mwema: Je, ulikata tamaa?

  Dk. Nzotta: Hapana, sikukata tamaa. Kuna siku moja tukiwa ubalozini (Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden) nilishauri kwamba kwa nini ubalozi wa Tanzania usianzishe database (hifadhi ya taarifa) ya Watanzania watalaamu? Unajua India ndiyo wanavyofanya, wanayo database ya wataalamu wao wote walioko nje ya nchi.

  Hiyo inasaidia sana kwa sababu serikali inapokuwa na uamuzi wa mradi au jambo fulani unaohitaji watalaamu wa aina fulani, basi, inakuwa rahisi kwao kujua nani yuko wapi, na kumuita kwa sababu huyo ni Mtanzania; hata kama amechukua uraia wa nchi za nje.

  Sasa pale ubalozini kulikuwa na ofisa mmoja ambaye kwa sasa yuko Ikulu (Dar es Salaam). Balozi hakuonyesha kuvutiwa sana na wazo hilo la database lakini huyo ofisa ubalozini pale alivutiwa na kuthamini. Ofisa mwenye anaitwa Mwaipaja kwa wakati ule alikuwa katibu wa balozi wetu Sweden.

  Sasa, nilisahau kukueleza kuwa baada ya kumaliza masomo mwaka 1999 niliajiriwa na kiwanda cha chuma kule kule Sweden kinaitwa Uddeholm Tooling AB. AB ni kama Limited kwa hapa Tanzania.

  Sasa yule Ofisa wa Ubalozi Mwaipaja akaja kunitembelea pale kiwandani kwetu na kukagua shughuli zangu, na kwa kweli mpaka leo yeye ndiye anayenihimiza; vinginevyo ni kama nilianza kukata tamaa.

  Mwaka 2004 nikaja kwa nauli yangu wakati ule kulikuwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia, nikapangiwa nikutane na watu wa DIT (Dar es Salaam Institute of Technology) ili tuzungumzie suala la kuanzisha Steel Complex Tanzania (SCT) kwa ajili ya kutoa taaluma ya metallurgy kwa vijana wetu ili tunufaike zaidi na raslimali zetu.

  Tukazungumza na mkuu wa DIT akaandika barua ili tuombe msaada SIDA (Shirika la Maendeleo la Sweden) kwa ajili ya kutafuta watalaamu, lakini nasikitika kwamba hapakuwa na msukumo au dhamira ya kutosha ya kisiasa.

  Baadaye tena safari ya pili binafsi nikaja mwaka 2008. Nilikuja kama mwakilishi wa kampuni yangu ya Sweden nilikoajiriwa. Nikazungumza na watu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Unajua katika tunachokusudia kuanzisha (SCT) tumepanga katika maeneo tofauti ya utekelezaji au uendeshaji. Tumeona kwamba ili Tanzania iendelee watu au wanafunzi wafundishwe katika makundi makuu mawili.

  Soma nakala kamili: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=3072 Dr.Mselly Nzotta mtaalamu anayetamba kitaaluma Sweden.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ziko hazina nyingi tu zilifichwa na hhawa wakoloni. Waliko wanajua walivyozificha michoro wameihifadhi, wajukuu zao watakuja kuzitafuta wakijifanya ma boy scout/girl guides. Hapa ni kuwawahi tu. Someni alama kwenye miti mikubwa na kufuatilia!
   
 3. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Utajiri tunao lakini tunaukalia, ni matumaini wawekezaji wa Kitanzania wataanza kwenda kuomba mikopo ktk mabenki na kuingia kwa kasi ktk sekta ya madini huku serikali ikiwawezesha kutekeleza miradi yao(wazawa) kwa ufanisi baada ya kusoma 'ushuhuda' huo hapo juu.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Tukiendelea kukaa na kufikiri utajiri ni maliasili tutakufa maskini, hata hao waarabu wameanza ku diversify kutoka kwenye mafuta. Sie ndio kwanza tunafikiri maliasili ndio utajiri.

  Nyerere alishawahi kutoa mfano, unaweza kuwa na almasi, akaja mtu na kichupa, akakwambia "hiyo si almasi ya kweli, hicho kichupa tu, almasi ya kweli hii hapa, tubadilishane" ukampa almasi ya kweli, yeye akupe kichupa.

  Tatizo ni kwamba, tumejiandaa vipi kuitumia maliasili yetu ili kupata mtaji wa kujiendeleza sio tu katika kufaidika na maliasili hii, bali hata ku diversify katika mengine?

  Kama mpaka leo mapato yetu yanayotokana na madini hayazidi 5% ya thamani ya kweli ya madini hayo kuna haja ya kuongelea madini kama mkombozi wa mtanzania?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Jamaa anakwambia Wajerumani wamechimba mashimo mwaka 1952, with all confidence ! Au nimemsikia vibaya? First video circa 0:29. Absurd.

  Wajerumani wameweka alama kwenye miti, how absurd .

  Jamaa kiingereza kingi hata muheshimiwa katibu wa kijiji inawezekana hamnyaki.

  Halafu watu wanakamata Zebaki kwa mikono, hamna hata swali kuhusu usalama wa afya zao wanapofanya hivyo.
   
 6. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mkuu inawezekana kabisa wala hakuna haja ya wawekezaji wa kutulaghai na utajiri wetu.
  Pendekezo: kuanzishwe public limited companies na kila mwananchi kuwa na fursa ya kumiliki hisa, then we shall see tricle down effect.
  Nawasilisha

  Thanks.
   
 7. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Serikali ikubali kuwamilikisha maeneo yenye madini Watanzania kupitia SACCOS, Vijiji n.k kama ambavyo Mh. Abdallah Kigoda kupitia umiliki wa ki-ploti cha ardhi atapata US$ 2.0 million cash na royalties ya 0.02 Corporate Update kutokana na mapato ya kampuni ya Canada kwa kaeneo kadogo huko Handeni mkoani Tanga, Tanzania. Hiyo ni hatua ya mwanzo kuwawezesha watanzania.

  Hatua inayofuata ni kuwapa ujuzi wa-Tanzania kusimamia miradi mikubwa ya madini ili kuongeza mapato kwa serikali na wananchi bila kutegemea makampuni ya uwekezaji toka nje ya nchi ili kuweza kuchambua hata mchanga wa dhahabu au madini ya chuma bila ya kuusafirisha nje kupata maximum return toka ktk migodi iliyopo Tanzania.

  Corporate update: http://www.sonoragoldcorp.com/corporate/management/65-corporate-update.html
  Sonora Gold & Silver Corp. (the "Company" or "Sonora") The Company has been informed that subsequent to the order of the Commissioner for Minerals of the United Republic of Tanzania (see the Company's December 2, 2010 press release), Abdallah Omary Kigoda was served with a default notice dated December 15, 2011 for, among other things, failure to comply with such order to surrender its ML 413/2010 for cancellation. The Company has further been informed that the Commissioner issued a cancellation of ML 413/2010 held by Mr. Kigoda,effective February 1, 2011. Canaco has reported by news release dated today that the Minister for Energy Mines and Minerals has directed Canaco to provide compensation to Mr. Kigoda and that Canaco and Mr. Kigoda have entered into an agreement for such compensation, consisting of $2.0 million cash and a 2 percent net smelter royalty for minerals recovered from the 0.07 square kilometre areaof the former PML 0010145. The Company has not received any notice of any of the foregoing from the Tanzanian government or a copy of this agreement and is in the process of verifying the accuracy of this information. The Company is consulting with its legal counsel in Tanzania and Canada and expects that it will take all legal steps available to appeal the orders and to seek full redress on these matters and protect its contractual rights to the Handeni property."

  ON BEHALF OF THE BOARD OF DIRECTORS
  Signed:
  "Ken Churchill"
  Ken Churchill, President & CEO, Director
   
 8. P

  Percival JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,566
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Kama haya ndio maneno ya huyu 'doctor' - endeleeni na ndoto. Huyu hana lolote la maana ndio maana Mkapa hakumsikiliza.
   
Loading...