Gerezani sio sehemu nzuri

Gerezani sio sehemu nzuri

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
330
Reaction score
1,244
1000243077.jpg

Gerezani ni mahala ambapo kila Mtu apendaye Uhuru anapaona bora uwe hospital umelazwa hata kama hujui ni lini utapa ahueni ila utakuwa na tumaini la Uhuru na kukutana na wapendwa wako kwa wakati.

JeLa ni mahala panapozima Furaha na Matumaini ya Mwanadamu hata wale Wategemezi wake au Maisha yake Binafsi huwa yanayumba kama sio kutawanyika kabisa

Gerezani ni mahala ambapo andazi moja linaweza kuliwa na watu kumi ni kwa sababu ya Upendo.

Gerezani ni mahala ambapo ujamaa na ubinafsi huishia kwenye lango la Gereza ila ukiingia Gerezani mnakuwa Ndugu wa Damu

Gerezani yupo Baba au Mama wa Mtoto au watoto baada ya kufungwa tu Watoto wake walipoteza tumaini la kesho yao njema bila uwepo wa baba au mama yao waliyeamini uwepo wake katika Maisha yao ungekuwa daraja na mafanikio ya Ndoto za hatma zao

Gerezani zipo Ndoto kubwa zimezimwa kama mshumaa ulioko juu ya kaburi ambao hauna mtu wa kuuzingatia tena kuuwasha ukizimika

Gerezani wapo watu wema sana ambao wapo hapo si kwa sababu walitenda ila mazingira tu yaliwatia hatiani. Waliotamani Mungu Baba afunue ushahidi kwa sababu wao walipojitetea hawakuaminika wakahukumiwa Kwa sababu ya Mazingira, Huruma zao, Wema au majitoleo yao

Gerezani wapo Watu ambao Maisha ya Uraiani hawana uhakika nayo tena Kwa sababu maisha yao yote yameshaamuriwa yataishia gerezani

Gereza limebeba sauti nyingi ambazo zina mengi sana.

Ukitaka ujue zipo sauti nyingi zinazohitaji huruma nenda ukawasalimie Wafungwa au ukamatwe uende Gerezani/Selo
 
Kila mwanaume alie hai probability ya kwenda jela inasoma 70/30 Either Kwa kutenda kosa au kusingiziwa

Tumuombe Mungu sana
 
Mwanangu huko sio pazuri hata kidogo
 
Magereza yapo ya aina nyingi: kuna wanaodhani wako huru kumbe kiuhalisia ni wafungwa, tena wa vifungo vibaya!
Lakini pia Unaweza kuufunga mwili ila huwezi kamwe kuzifunga imani, fikra na utashi wa mtu.
 
Back
Top Bottom