Georgina Mahiga aliyetungiwa wimbo wa “Georgina” ulioimbwa na Marijani Rajabu afariki Dunia

Hao wengine kwenye picha ni wakina nani. Kama una visa na Mikasa ya hawa jamaa naomba utuporomoshee. Maneti, Kingki, Kasaloo, Kanga, Makassy, Remmy nk
Usijali mkuu n
Hao wengine kwenye picha ni wakina nani. Kama una visa na Mikasa ya hawa jamaa naomba utuporomoshee. Maneti, Kingki, Kasaloo, Kanga, Makassy, Remmy nk
Nitakuletea story ya maneti,binti yake anaitwa komweta yuko south sasa hivi alijaribu kufuata nyayo za baba yake ila kaacha kuimba ,mbaya maneti,marijani ,mbaraka hawa wote walikufa wakiwa vijana sana,makasi na remmy story zao zinaendana,kasaloo kyanga na kyanga songa pia zinaendana hawa ni mapacha walianzia tancut almas ya iringa wakiwa na john kitime.ngoja nianze na ya remmy na makasi leo jioni
 
BURIANI GEORGINA MAHIGA!


BONGOLANDERS wengi wanaufahamu vizuri wimbo maarufu wa GEORGINA ulioimbwa na mmoja wa waimbaji bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania aitwae MARIJANI RAJAB "JABALI LA MUZIKI" akiwa na bendi yake ya Safari Trippers. Ni wimbo ambao hupendwa sana na Wahenga na wala hauchuji licha ya kwamba uliimbwa miaka ya mwanzoni ya 70.

GEORGINA MAHIGA ambaye amefariki wiki hii, alikuwa ni mtoto wa kaka mkubwa wa Mh. AUGUSTIN PHILLIP MAHIGA, Waziri wa Katiba na Sheria.

Je, ilikuwaje hadi JABALI LA MUZIKI kumtungia wimbo Bi. GEORGINA?
Ni kwamba Bi. GEORGINA alikuwa akisoma shule ya sekondari ya Zanaki, Dsm. Akiwa kidato cha pili mwaka 1974 alipata mimba. Mimba hiyo alipewa na Boy friend wake aliyekuwa akisoma kidato cha pili pia shule ya sekondari ya Tambaza na rafiki mkubwa wa JABALI LA MUZIKI ambalo pia lilikuwa likisoma shuleni hapo.

Mama Mahiga akaamua kumpeleka GEORGINA Iringa bila ya akina JABALI LA MUZIKI kujua aliko GEORGINA. Ilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa rafiki yake JABALI LA MUZIKI aliyempa uja uzito huo kwani alikuwa akimpenda kwa dhati ila alikuwa hajui yuko wapi na kila siku alikuwa akilalamika kwa JABALI LA MUZIKI ambalo likaamua kuichangamkia fursa hiyo na kutunga wimbo huo uliotokea kuwa moja ya nyimbo bora za wakati wote Bongo!.

Bi. Georgina alijifungua mtoto wa kiume ambaye bahati mbaya alifariki mwaka juzi.

Mashairi ya wimbo GEORGINA:

"Ooh Georgina, siku uliyoondoka uliniacha nalia na machozi, umekwenda kuishi mbali nami, Georgina wa mamaa" X 2

"Sipatii usingizi nikikumbuka tulivyoishi mi na we Georgina" X 2

"Umeondoka Georgina umeniachia masikitiko, ooh nauliza Georgina ni lini utarudi, uniondoe wasiwasi, Georgina wa mamaa" X 2

Katika hii picha hapa chini yenye wamama wanne waliovalia nguo nyeupe, Bi. GEORGINA ni wa kwanza kushoto wakati wa uhai wake alipokuwa kwenye msiba wa baba yake mwaka juzi.

Bi. GEORGINA amezikwa leo jioni ya Jumapili tarehe 4 Agosti 2019 kwenye makaburi ya Kinondoni, Dsm.

Bwana alitoa Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!View attachment 1174103View attachment 1174104

Georgina na familia yake walikuwa majirani zetu miaka ya 69/70 pale Chang'ombe Govt Qtrs.
 
Hii habari ilinipita.

Mimi ni Shabiki Mkubwa wa Marijani Mwana wa Rajabu a.k.a Jabali La Muziki.

Ila sidhani kama Marijani alikuwa Mtunzi wa huu wimbo, yeye alipewa auimbe na ikasemekana Mtunzi mwenyewe akamvulia Marijani Kofia kwa kazi aliyoifanya.
 
Usijali mkuu n

Nitakuletea story ya maneti,binti yake anaitwa komweta yuko south sasa hivi alijaribu kufuata nyayo za baba yake ila kaacha kuimba ,mbaya maneti,marijani ,mbaraka hawa wote walikufa wakiwa vijana sana,makasi na remmy story zao zinaendana,kasaloo kyanga na kyanga songa pia zinaendana hawa ni mapacha walianzia tancut almas ya iringa wakiwa na john kitime.ngoja nianze na ya remmy na makasi leo jio
 
Hii habari ilinipita.

Mimi ni Shabiki Mkubwa wa Marijani Mwana wa Rajabu a.k.a Jabali La Muziki.

Ila sidhani kama Marijani alikuwa Mtunzi wa huu wimbo, yeye alipewa auimbe na ikasemekana Mtunzi mwenyewe akamvulia Marijani Kofia kwa kazi aliyoifanya.
Ni kweki alitungiwa na uvuruge mpiga solo ila aliutendea haki huo wimbo tena akiwa na miaka 18
 
Ningependa kufahamu yafuatayo...

Mwamba alimpa mimba Gorgina wakati wapo Form II, na mwamba walikuwa wanasoma pamoja na Marijani Tambaza...

Kwahiyo ni kwamba Marijan aliimba huo wimbo wakati yupo mwanafunzi back in 1970's, au?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom