Huyu ndiye Marijani Rajabu

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
Marijani Rajabu

Umahiri mkubwa wa kupiga ala tofauti tofauti za Muziki kutoka kwa magwiji wa muziki Africa kipindi hicho kama; Sory Kandia Koutare toka huko guinea na Tabu Ley Rochereau (Tabu ley) aliye kuwa kiongozi wa Orchestre Afrisa International.

☆ Ulimvutia zaidi kijana mdogo wa umri wa miaka 15 tu, mwenye mapenzi na muziki na kipaji kikubwa ndani yake. Mzawa wa Kariakoo Dar es Salaam akiwa na asili ya Kigoma (kwa maana ya chimbuko la wazazi wake). Tarehe ya 23, mwezi March mwaka wa 1955, ndiyo siku ambayo.

☆ Mtoto huyu wa Africa alizaliwa katika familia ya kawaida kabisa ya mchapakazi na mchapishaji wa majarada mzee Rajabu, vijana wa sasa wangesema (Rajabu Sr). Ilipofika mwaka 1970 tu, akiwa bado mwanafunzi Marijani alifanikiwa kujiunga na bendi ya STC Jazz Band (The jets).

☆ Chini ya bendi hii ambayo ilikuwa ikiongozwa na mkongwe Raphael Sabuni ilipata mualiko kwenda katika tamasha huko Nairobi Kenya, safari iliyo zaa tungo kadhaa zilizorekodiwa chini Phillips record ambazo inasadikika ni mchango mkubwa wa utunzi wa marijani ulifanikisha hilo.

☆ Ikumbukwe Marijani alikuwa bado kijana mdogo, hivyo kutokana na umri wake kufanya shughuli hizo ilileta shida katika bendi ile ambayo kimsingi ilikuwa ya umma hivyo ililazimu akae mbali kwa katazo la kutojihusisha nalo, kwa hofu ya kuvunja sheria.

☆ Baadae mwaka 1972, Marijani alijiunga na bendi ya The Trippers Band (trippers kwa lugha ya kikwetu ni wasafiri) kwa mnaochanganyikiwa kidogo na lugha 😁😁. The Tripper ikiongozwa na David Mussa kama Mkurugenzi (muimbaji), na muimbaji kiongozi kwa jina la Ali Rajabu.

☆ Walifanikiwa kuachia vibao kadha wa kadha maarufu kama;
● Rosa Nenda Shule
● Mkuki Moyoni
● Georgina
● Olilla

Ambapo kwa taarifa Bwana David Mussa alikiri kuuzwa kwa nakala takribani 10,000 za santuri, jambo lililo pelekea waweze kununua vyombo vya bendi (Pichani, J Mussa).

☆ Palipo na wengi basi mambo huwa mengi vilevile (waswahili wanasema). Baada ya kupata mafanikio hayo wanahisa (wazee wa bendi), kati yao kukatokea mtafaruku ambao ulipelekea kutokuelewana kabisa na hatimaye bendi ikasambaratika. The trippers au Safari Band ikatoweka.

☆ Hata hivyo huo ulikuwa mwisho wa Trippers Band na siyo mwisho wa safari ya muziki ya gwiji Marijani rajabu. Ambaye ilipofika mwaka 1976, alipata wazo la kuanzisha band ambapo ilipidi kwanza kupata wadhamini, hapo ndipo anaingia Mzee Zakaria Ndabemeye kuokoa jahazi.

☆ Sasa kilichobaki ilikua ni kutengeneza kikosi cha mashambulizi (eeh ndiyo), maana bendi kwa wakati ule ushindani wake ulikuwa mkubwa mnoo kama Simba na Yanga hivi sasa.

Basi usajiri ukaanza (usiniulize dirisha kubwa au dogo 😁😁) na Kikosi kikawa hivi 👇
● Abel Baltazar (toka Msondo)
● Kassim Mponda ( toka Trippers)
● Said Mohamed (toka Polisi Jazz)
● C, Chimule (toka Urafiki)
● Balesa Kakere (toka Biashara Jazz)
● Joseph Bernad (Toka Trippers)
● Ali Rajabu (Toka Trippers)
● King Michael (Dar Jazz)

☆ Baada ya kuwa na mtafaruku na mmoja ya waimbaji wenziwe aliyefahamika kama Abel Baltazar juu ya kile kilicho itwa ubishi. Chidumule anasimulia kuwa kuna moja ya tungo ambayo iliimbwa na ikatokea kufanana sana na moja ya tungo huko congo, hivyo ililazimu Marijani.

☆ Abadili namna ya uimbaji huo kusudi usishabihiane, jambo ambalo marijani hakulihafiki, hivyo kupelekea kufukuzwa katika bendi, ambapo baadae alirudishwa baada ya waimbaji wengi kuikimbia tena bendi hiyo

☆ Baada ya kurudi tena Dar es Salaam International hiyo ilikuwa 1978 inaenda 1979, yule hasimu wake bwana Abel Baltazar alitimka na baadhi ya waimbaji wenzake na kwenda kuanzisha bendi ya Ochestra MLlimani Park.

☆ Hama hama ile ya waimbaji kama walivyo pendwa kuitwa na siyo (wasanii), Marijani alikutana na watu wapya kabisa katika bendi baada ya ujio wake mara ya pili, wakongwe kama, Chistopher Kasongo, Mohammed Tungwa, Hamis Milambo, Athumani Momba na Alex Kanyimbo.

☆ Ni katika kipindi hiki hiki baada ya ujio huu Marijani aliweza pia kushika mkono wasanii waliokuwa wachanga ambao baadae wakaja kuwa wakubwa sana katika uwanda huu. Wasanii kama Fresh Jumbe ambaye kwa sasa makazi yake ni Japan Tokyo, akiendelea na shughuli za muziki katika kumbi.

☆ Alifanikisha pia kutoa album iliyokuwa na vibao kama Zuena na Mwanameka, vibao vilivyokuwa gumzo na vingine vikifanyiwa sample mpaka leo hii na wasanii wa Bongo Fleva, lakini katika kazi kubwa yote hiyo pesa aliyo ambulia ilikuwa ni 2500/= Th toka RTD

☆ Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), ambao ndiyo walihusika na recording nzima hiyo ilikuwa ni mwaka 1983 na ilipofika mwaka 1987. Bend ya Dar International ilikufa na hii ni kutokana na sababu za uchakavu wa vyombo na malipo yasiyoridhisha.

☆ Nyota wetu wa mchezo wa leo anaingia katika kundi lile lile la masikini wenye majina makubwa mpaka pale umauti ulipo mfika. Na kwa ushahidi wa wazi kabisa Marijani alianza kutembeza kanda za nyimbo zake mitaani ili kujipatia chochote kutokana na ugumu wa maisha.

☆ Zipo bendi kadhaa ambazo gwiji huyu alipita japo siyo kwa mafanikio makubwa kama;
● Arusha jazz
● Mwenge Jazz

Pia akiambatana na Muhidin Maalim Ngurumo, mwaka huo wa 1987 katika kuhadhimisha miaka 20 ya azimio la arusha la 1967, waliongoza jopo la waimbaji zaidi ya 50 na kuunda Tanzania All Stars kwa mara ya kwanza (huu umekuwa utamaduni ambapo kila maadhimisho).

Basi waimbaji wa aina tofauti za muziki hujumuika pamoja na kuhamasisha uzalendo kupitia uimbaji.

Huyo ndiyo MARIJANI RAJABU (marijani wa zuwena)

Imeandikwa na ChizzoDrama

a890e2403d80da6625ef487c2e4dc642.jpg
Tabu_Ley_Rochereau.jpg
 

Attachments

  • images - 2023-05-24T013802.624.jpeg
    images - 2023-05-24T013802.624.jpeg
    21.8 KB · Views: 7
  • Screenshot_20230524-020639_Chrome.jpg
    Screenshot_20230524-020639_Chrome.jpg
    100.3 KB · Views: 14
  • Marijani_Rajabu (1).jpg
    Marijani_Rajabu (1).jpg
    10.3 KB · Views: 12
  • images - 2023-05-24T022621.785.jpeg
    images - 2023-05-24T022621.785.jpeg
    9.6 KB · Views: 13
  • David_Mussa_na_Marijani.jpg
    David_Mussa_na_Marijani.jpg
    24.2 KB · Views: 11
  • images - 2023-05-24T022616.128.jpeg
    images - 2023-05-24T022616.128.jpeg
    10.1 KB · Views: 9
  • images - 2023-05-24T025337.542.jpeg
    images - 2023-05-24T025337.542.jpeg
    11.3 KB · Views: 9
  • images - 2023-05-24T031541.927.jpeg
    images - 2023-05-24T031541.927.jpeg
    10.3 KB · Views: 12
  • 440px-Fresh_Jumbe.jpg
    440px-Fresh_Jumbe.jpg
    21.7 KB · Views: 13
  • images - 2023-05-24T031415.262.jpeg
    images - 2023-05-24T031415.262.jpeg
    37.2 KB · Views: 9
  • images - 2023-05-24T013222.179.jpeg
    images - 2023-05-24T013222.179.jpeg
    31.9 KB · Views: 11
Mkuu unapomzungumzia mtu anaeitwa Marijani Rajabu, hapo unakuwa umeuzungumzia mziki mzima wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

There's no way unaweza kuuzungumzia mziki wa Tanzania bila kumtaja Marijani Rajabu. Pamoja na kwamba mziki wake haukuwahi kumsaidia yeye kimaisha kama ilivyo kwa kina Diamond, Konde boy nk, lakini ukweli ni kwamba mziki wake umeweza kulisaidia taifa kimaadili na kitabia hasa kwa wale ambao wamekuwa wakizingatia kile kinachoimbwa na msanii huyo. Nyimbo kama vile:

1. Usia wa baba
2. Masudi
3. Mwanameka
4. Ndoa ya mateso
5. Zuwena
6. Dunia ni uwanja wa fujo

Na nyingine nyingi ni kielelezo cha ubora na umahiri wa msaanii huyo. Ndio maana wahenga wenyewe waliamua kumpachika jina kumwita Jabali la mziki Tanzania.
 
Mkuu unapomzungumzia mtu anaeitwa Marijani Rajabu, hapo unakuwa umeuzungumzia mziki mzima wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

There's no way unaweza kuuzungumzia mziki wa Tanzania bila kumtaja Marijani Rajabu. Pamoja na kwamba mziki wake haukuwahi kumsaidia yeye kimaisha kama ilivyo kwa kina Diamond, Konde boy nk, lakini ukweli ni kwamba mziki wake umeweza kulisaidia taifa kimaadili na kitabia hasa kwa wale ambao wamekuwa wakizingatia kile kinachoimbwa na msanii huyo. Nyimbo kama vile:

1. Usia wa baba
2. Masudi
3. Mwanameka
4. Ndoa ya mateso
5. Zuwena
6. Dunia ni uwanja wa fujo

Na nyingine nyingi ni kielelezo cha ubora na umahiri wa msaanii huyo. Ndio maana wahenga wenyewe waliamua kumpachika jina kumwita Jabali la mziki Tanzania.
True
 
Kouyate Sori Kandia nilikuwa nauimba wimbo wake "Malisadio" wote ingawa sijui hata maana ya neno moja
 
Fresh Jumbe bado yuko Japan? Aling'oa toto moja kali sana ya kijapani sijui kama alizaa naye mwanadada wa zamani.

Marijani Rajabu usisahau wimbo wake wa Mwanameka. Ule wimbo unakonga moyo wangu mpaka hivi leo.
 
Fresh Jumbe bado yuko Japan? Aling'oa toto moja kali sana ya kijapani sijui kama alizaa naye mwanadada wa zamani.

Marijani Rajabu usisahau wimbo wake wa Mwanameka. Ule wimbo unakonga moyo wangu mpaka hivi leo.
Mwanameka ukatumika pia kwenye mtihani wa kidato cha nne. Kaka yangu alifanya mtihani huo wa Kiswahili, nafikiri fasihi
 
Nje ya mada kidogo.
Kuna wimbo sio wa kiswahili unaitwa mokolo nako kufa, na kuna wimbo wa kiswahili siujui jina ila nadhani ni "walau nafasi" mfano hiyo mokolo nakokufa nimezaliwa nimeikuta, baba alikuwaga na radio ya kuzungusha ndio niliijulia hapo.

Hizi nyimbo upigaji wa vyombo unaendana kwa 90%. Je, kuna uhusiano wowote?
 
Nje ya mada kidogo.
Kuna wimbo sio wa kiswahili unaitwa mokolo nako kufa, na kuna wimbo wa kiswahili siujui jina ila nadhani ni "walau nafasi" mfano hiyo mokolo nakokufa nimezaliwa nimeikuta, baba alikuwaga na radio ya kuzungusha ndio niliijulia hapo.

Hizi nyimbo upigaji wa vyombo unaendana kwa 90%. Je, kuna uhusiano wowote?
Kilwa Jazz walikopi Wakongo
 
Hata hivyo huo ulikuwa mwisho wa Trippers Band na siyo mwisho wa safari ya muziki ya gwiji Marijani rajabu. Ambaye ilipofika mwaka 1976, alipata wazo la kuanzisha band ambapo ilipidi kwanza kupata wadhamini, hapo ndipo anaingia Mzee Zakaria Ndabemeye kuokoa jahazi
Mzee Zakaria Ndabameye alianzisha bendi kwa ushawishi wa Abel Baltazar ambaye ni mpiga gitaa na wala sio muimbaji,Mzee Ndabameye na Abel Baltazar ni marafiki waliosoma shule moja na wametoka kijiji kimoja cha Mjesani Lushoto,Tanga na bendi ilipoanziashwa ni Abel ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta wanamuziki na yeye ndiye alikuwa kiongozi wa bendi.
Marijani Rajabu hakuwa na ukaribu wala kufahamiana na Mzee Ndabameye kabla.
 
Back
Top Bottom