Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,883
- 5,270
Ninasikiliza Kipindi cha 'zilipendwa', basi nimesikia Mkasa ulio nyuma ya wimbo wa Georgina wake Marijan Rajab.
Wimbo huu ni mkasa wa kweli. Mapenzi shuleni.
Marijan yaelezwa alikuwa akisoma Tambaza na rafikiye mmoja. Huyo Rafiye alikuwa na uhusiano na binti aitwaye Georgina Mahiga; Mtoto wa kaka yake Marehemu Balozi Augustine Mahiga. Binti huyo alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha Pili pale Azania Secondary school. Bahati mbaya akapata ujauzito. Kuepusha dhahma, wazazi wa Georgina walimtoa Azania na kumpeleka Iringa.
Rafikiye Marijan hakuwa anajua kuwa Mwanamke wake ameondoshwa Dar. Alikuwa akimtafuta pasi na kujua amekwenda wapi. Aliteseka na kuondoka kwake.
Katika hangaiko lile, ndipo Marijani akapata fursa ya Kutunga wimbo huo miaka ya 1970.
Kilichofuata ni wimbo ambao umeishi hadi leo. Masherehe mengi wimbo huu huwa haukosi.
FM Academia waliufanyia live performance wimbo huu.
www.boomplaymusic.com
Source: [emoji343] Kahama FM

Live Georgina | Boomplay Music
Boomplay focuses on African and international music, you can stream and download Live Georgina.
Source: [emoji343] Kahama FM